Ubaguzi: Machotara Hizbu, Zanzibar ni nchi ya Waafrika

Cha kushangaza hao viongozi wote wa CCM karibia wote wake zao ni machotora na watoto wa ni machotora.
kumbe mnachukia ubaguzi? nyie humu huwa hamuachi kuaneza chuki za udini na mtoa mada mnaona sawa....ona sasa zenji karibia 99 ni waislam lakini wakaona haiwezi tosha kujibagua wakagunduz kuwa kati ya hao waislam kuna machora na wazenji halisi.....ubaguzi mbaya mjifunze
 
Siasa za kishenzi ambazo chama kimeendekeza matokeo yake hayo sasa. Kuna vijana wa ccm manazi wa kutisha na wengine huku bara wameanza kupewa mpk vyeo. Ni tabia iliyodekezwa tangu siku nyingi. Ya kubagua upinzani unafikiri wewe baba ukionyesha ubaguzi mtoto wako anaweza kumuua huyo mpinzani. Wamo uvccm humuhumu jf wazandiki kuliko kawaida siyo binadamu tena. Znz ni matokeo ya ccm kulea vibaya vijana wake na unganganizi wa madaraka unafikiri wao wasemeje kama ccm inamuona maalimu hafai kutawala. Wametusaidia kujua kilichojificha ccm imepoteza sifa ya kuwa chama cha siasa wao ndiyo hao madharimu na madikiteta. Unapindisha ushindi ili ninj harafu mnaanza mazungumzo ya nini waseme hapewi nchi.
 
...

Tatizo lako wewe umeangalia athari ya ubaguzi kwenye siasa tu! Hilo ni dogo ndugu! Tatizo ni kubwa zaidi ya hapo mara elfu kumi!

Wanawajua na kuijua zanzibari vizuri wanafahamu.

Kama unatafuta kisingizio kuhalalisha kauli ya kibaguzi hutakosa. Ubaguzi ni hulka ya kawaida ya binadamu katika karibu jamii zote. Hata Tanzania bara (Tanganyika) wapo watu wengi tu wanajiona bora kuliko wengine kwa rangi, Kabila, dini, n.k.

Siku zote ni jukumu la msingi la uongozi wa nchi (serikali ya watu) kutengeneza mazingira ya kufisha mitazamo ya kibaguzi na kuwajengea wananchi umoja. Na hayo ni mapambano ya kudumu. Hayana mwisho. NA SIASA SAFI NDIO NYENZO YA MSINGI YA KUZIMA UBAGUZI WA AINA ZOTE! SIASA IKIENDESHWA KIHUNI NI KAMA KUMWAGA PETROLI KWENYE HISIA ZA KIBAGUZI.

Tunachokishuhudia leo hii ni viongozi wanaotarajiwa kusimamia misingi ya umoja wa kitaifa wakifanya juhudi za kustaajabisha kutuaminisha kuwa kuna jamii za watu miongoni mwetu ambazo hazifai - tuzipinge na kuzikandamizia mbali! Kisa? Zinahatarisha uwepo wao madarakani! HALAFU watu mnahangaika kutafuta hoja za kuhalalisha (justify) ujinga huo!
 
Siishangali kabisa hiyo sentensi, ila nachojua sio wanafiki wanachowaza na wanachoamini ndicho walichokiandika. Huku bara nadhan tupo hivyo hivyo ila hatubebi mabango na ni hawa hawa ndg zetu CCM wanatuhubiria hii dhambi. Huku bara tunaita ukanda, watu wa kaskazini mara wachaga, na humu jf wako wengi tu wabaguzi. Na leo hii hao hao wanawashangaa wanzanzibar! Kweli?
 
Wakati wanambagua Dr.Saln Ahmed Salmu kuwa ni Hizbul na wengine kama akina Jr Ulimwengu, Mama Castico, Ibrahim Bashe na wakati wanaendesha siasa za ubaguzi juu ya Maalim seif na Kuwait's waarabu walikuwa hawafanyi makosa, kwani itikadi yao ya ukanda, ukabila na udini

Hii ni moja ya Sera ya ccm
 
Huu ni zaidi ya uzandiki ni fitina na ubaguzi uliopitiliza hawa wasifumbiwe macho kamata wote weka ndani haraka sana.

Hii sio tz ya mwalimu nyerere.
Hatutaki ubaguzi.
 
Endapo maalim atatangazwa kuwa rais wa Zanzibar kauli hii itakuwa ya mbeba bango otherwise message sent indirectly and delivered
 

 
Kwa Neno Hili (MACHOTARA HIZBU ZANZIBAR NI NCHI YA WAAFRIKA) kwa neno Hili CCM Zanzibar ni Wabaguzi kitendo hicho kinafaa kulaaniwa kinaleta Ubaguzi wa Rangi.
 
Kwa Neno Hili (MACHOTARA HIZBU ZANZIBAR NI NCHI YA WAAFRIKA) kwa neno Hili CCM Zanzibar ni Wabaguzi kitendo hicho kinafaa kulaaniwa kinaleta Ubaguzi wa Rangi.
Wazinzabar wanaitwa wa Hizbu!?
 
Mkuu kunakitu kinaitwa positive discrimination.
Ulikuwa ukiandika kwa kina "kuwaenzi " waislamu kwa juhudi za uhuru katika " mfumo Kristo"
Ulichokuwa unafanya ni discrimination all the same.
Ulimponda sana Mwalimu kwa kukukandamiza wewe binafsi kama mwislamu na waislamu kwa ujumla.
Na hayo ndiyo leo tunayaona Zanzibar, ubaguzi si wa kidini tu, bali wa rangi.
Ubaguzi ulioenziwa na watu kama ninyi.

Usituchagulie aina ya ubaguzi unaoupendelea wewe, ubaguzi ni ubaguzi tu.
Na kwa Zanzibar wewe na wengine mnavuna ubaguzi mlioupanda.
 
Last edited:
Nimemkumbuka Luqman Maloto kwenye moja ya makala zake aliwahi kuandika, "Zanzibar hakuna ugomvi wa kisiasa. Zanzibar kuna chuki."
 
Endapo maalim atatangazwa kuwa rais wa Zanzibar kauli hii itakuwa ya mbeba bango otherwise message sent indirectly and delivered
Mm huwa nawatahadharisha sana ccm zanzibar,wakimaliza kuwapoteza machotara wa zanzibar kibao kitageuga na wa kutoka mrima hawatobaki salama zanzibar.
 
WAAFRICA WAKOJE? NINAVYOJUA WEUSI, WAZUNGU, WARABU, NA WOTE WENYE ASILI YA ASIA, WOTE NI WAAFRICA KAMA NI RAIA WA MOJA YA NCHI ILIOMO AFRICA HILI BANGO LINAMANISHA MACHOTALA WA BARA GANI WANAOITAKA ZANZIBAR, KAMA NI WANZABAR { TZ } NI WAAFRICA. HII INAONYESHA KUA CCM IMEJAA MAZOMBI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…