Ubaguzi: Machotara Hizbu, Zanzibar ni nchi ya Waafrika

Ubaguzi: Machotara Hizbu, Zanzibar ni nchi ya Waafrika

Picha hiyo hapo juu ni bango la Kikaburu katika mwaka wa 2016 bango linalotukuza ubaguzi wa rangi.


Sitaki kuamini kuwa tumeanza kuwatengeza akina Hendrik Verwoerd na Eugene Terre Blanche weusi katika visiwa vya Zanzibar.

CCM Zanzibar inamuiga nani katika hili?


Kasema Mwalimu Nyerere karne ya ishirini na moja kuna watu wanapanda basi la ukabila...

Hawa wanapanda jahazi la ugozi.

Naungana na wewe kukemea aina yoyote ya ubaguzi, na ningependa kama itakupendeza kwenye makala zako nyingine za kukemea ubaguzi uongeze paragraph inayogusia 'machogo'.
 
Duh,hii ni dhambi kubwa sana,dhambi ya ubaguzi. Hivi watu huwa wanajitoa fahamu kiasi hiki? Inasikitisha sana..
vijana wa CCM wana shida. walishasema nchi haitatawaliwa na watu wa kaskazini!
 
Kwa Neno Hili (MACHOTARA HIZBU ZANZIBAR NI NCHI YA WAAFRIKA) kwa neno Hili CCM Zanzibar ni Wabaguzi kitendo hicho kinafaa kulaaniwa kinaleta Ubaguzi wa Rangi.

nikweli mkuu..ubaguzi haufai hata kidogo
 
Naungana nawewe kwa kiasi kikubwa kabisa,na sababu ni kwamba umenifanya nikarecall na kurefer mambo mengi sana ambayo yamekuwa yakinenwa na kuandikwa na Viongozi flan wa zanzibar over the years pamoja na wadau wengine waliokuwa wakiitetea zanzibar na sasa wamegeuka Mamluki kwa unafiki. Kwa upande wa visiwa vingine sina uhakika.

Mwenyezi Mungu alisema bora uwe Moto au Baridi. Ukiwa vuguvugu atakutapika.

NIMEKUELEWA SANA MKUU.

Fatma Maghembe,Hamadi Rashidi...na wengineo walikuwa viongozi wakuu CUF
wakiupinga muungano

Sasa wote wanasema Muungano ulindwe...waliokuwa CCM walisema muungano ulindwe
now wako CUF hawautaki.....wazanzibari unafiki ni culture
 
[QUOTE="Mohamed Said, post: 15074123, member: 12431"



Kasema Mwalimu Nyerere karne ya ishirini na moja kuna watu wanapanda basi la ukabila...

Hawa wanapanda jahazi la ugozi.[/QUOTE]
Uchaguzi au siasa za Zanzibar tunaambiwa ni mazungumzo. Kwa hili CCM ijitazame tena kama vijana inaowatengeneza wanaweza kuhimili demokrasia ya kweli. Je huo uchaguzi endapo utarudiwa na CUF wakasema tufe na mtu wakashinda. Bango hilo linaashiria vurugui, CCM wakishinda au CUF wakishinda. Lazima likemewe. Ubaguzi unapandikizwa si kwa basi la ukabila tu bali la udini, la ukanda na lolote linaloona kundi lao ndilo.
 
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Zanzibar anajisikiaje akisoma bango hili?
Anajisikia raja sana hao si ni vijana wao,CCM ndio miasisi was hayo mambo rejea kampeni za bara nazo zilitawaliwa na na ukabila sana,soon tutaanza kubaguana wafupi na warefu tukoka hapo, tutafuata wanywa soda na wanywa biabia nk.
 
ubaguzi umeota mizizi ndani ya ccm,mmesahau salim a salim alivyofanyiwa?
mara hii tumesahau makada wa ccm walivyotamka maneno ya kikaburu ktk bunge la katiba?
ccm ni ile ile, wana halmashauri zaidI ya mia lakini wapo tayari kumwaga damu kwa ajili ya halmashauri 4 tu walizoshindwa.hiki cjui ni kizazi gani?
 
Catch 22
Muajemi wa kizazi cha kumi na.mbili na
Mnyamwezi kizazi cha tatu
Fumbo
Na wewe unaleta ubaguzi wako kwa mafumbo yako uchwara.
Kwa maana hiyo Waajemi wana haki zaifi kuliko Wanyamwezi!?
Na hata kama Waajemi walitangulia hilo au hata kama wanyamwezi ndio walitangulia hilo hali halalishi ubaguzi wowote.
 
Machotara weupe na machotara wa kikabila kazi ipo ya ubaguzi.
Hakuna asiye chotara Zanzibar,ima atakuwa kachanganya rangi au kabila,hata huyo aliyeshika bango,huwenda akawa amechanganya umakonde na unyamwezi(pia ni uchotara).
Na pia ni ukosefu wa elimu,ziko nchi za kiarabu zilo ndani ya Afrika:
Tunisia
Libya
Sudan
Misri
Morocco
Sahara Magharibi
Nk
 
Hao kwenye iyo picha takriban wengi si wazanzibari ni watanganyika, waznz kati ya hao ni wachache mno nao wamechanganya na watanganyika. Znz machotara wapo kabla ata ya utawala wa kiarabu kwa hiyo wana asili, kama ni rangi wapo waznz waliokuwa hawana asili ya kiarabu wala ya kihindi na ni weupe pia. Kwa iyo musitufanye majuha hao ni watanganyika, ccm znz ni wachache kwa hiyo wakifanya mikutano kama hivi huleta watu wa bongo kuhudhuria ili kuongeza idadi waonekane wengi, habari ndo hiyo
 
Fatma Maghembe,Hamadi Rashidi...na wengineo walikuwa viongozi wakuu CUF
wakiupinga muungano

Sasa wote wanasema Muungano ulindwe...waliokuwa CCM walisema muungano ulindwe
now wako CUF hawautaki.....wazanzibari unafiki ni culture
Hiyo ndio siasa. Wapo kulinda maslahi yao na watoto wao zaidi.
 
Rais mwenyewe haramu unadhani wafuasi watakuwaje ?
 
Ahahahahahahahahah..safi sana wazenji waafrika.Leo ustadhi moody kalishwa fupa la nguruwe mpaka kamkumbuka mwalimu nyerere.Kumbe ubaguzi ni mbaya eenh..Na wewe u.kome kubagua wakristo.Sisi sote ni viumbe wa Mungu Mmoja.
 
Wadau suala la Ubaguzi Zanzibar halijaanza Mapinduzi day ya 2016,kwa.kifupi wazanzibar kwa ujumla wao ni wabaguzi sana,safar hii wamebaguana wenyewe kwa wenyewe tu,ila ukweli ni kwamba wanawabagua sana watanganyika,naposema sana namanisha sana hasaaa,sasa leo wamebaguana wenyewe kwa wenyewe inawauma kwelikweli,wazenj ISSUE YA UBAGUZI ITAWATESA SANAAAAA SANAAA SANAAAAA,Mkiwa kwenu huko mnawanagua watanganyika na mkija huku mnawabagua watanganyika,ila ni kwamba watanganyika huwa wanawapuuuza tu,na kingine watanganyika hawakuwah kupigia kelele ya dhahir juu ya ubaguz wenu huu.
Poleni sana ila jana umefunguliwa ukurasa mpyaaaa ZENJI

Maneno yako ni sahihi kabisa...na nakuunga mkono mia kwa mia kua hawa watu wenyewe wote au asilimia kubwa zaidi ni wabaguzi.

Watake wasitake ni wabaguzi.
 
Back
Top Bottom