Ubaguzi: Machotara Hizbu, Zanzibar ni nchi ya Waafrika

Ubaguzi: Machotara Hizbu, Zanzibar ni nchi ya Waafrika

Cha kushangaza hao viongozi wote wa CCM karibia wote wake zao ni machotora na watoto wa ni machotora.
Zanzibar ni machota,bila ya machotara hamna Zanzibar,Uchotara ni moja katika sifa za visiwa,sio Zanzibar tu Visiwa vyote duniani vina sifa ya kuwa na mchotara

Watu wanashindwa klufahamu hata hao masultani walikuwa machotara,,,,Huwezai kuwa mzanzibar halisi kama huna uchotara,alieandika hilo bango ndio hao wazanzibari wakuja,wahamiaji,koo zao hawana hata muongo mmoja katika Zanzibar,na ndio hao ambo wanagombania kung´ang´ania madaraka kwa kuogopa kuwa wazanzibari wenye nchi yao watatawala
 
Mbona sielewi hapa ?huyu anawajibu walionadika bango au watu wengine?kwa nini asirudi nyuma siku mbili tu zilizopita akaenda kuwauliza wenzake walioandika bango walikuwa wanamaana gani kuliko kutuletea utetezi hovyo ya kuwa "chama chetu hivi.... chama chetu vile...." ilihali bango limepita mbele ya mlinzi mkuu wa mapinduzi likiongea kinyume na mahubiri haya?Shaka tupishe tuendelee kutafakari hatma ya jamaa zetu machotara!
 
Tena na rais anapunga mkono.
 
DSC_2469.jpg

Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akipokea matembezi ya Vijana hao waliotembea katika Mikoa Minee ya Kichama katika kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyomalizia leo katika viwanja vya maisara Suleiman Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]

Picha hiyo hapo juu ni bango la Kikaburu katika mwaka wa 2016 bango linalotukuza ubaguzi wa rangi.

DSC_2827.jpg

Sitaki kuamini kama Ali Mohamed Sheni na uongozi wa juu wa CCM Zanzibar wamewatuma vijana hawa kufanya haya.

Akili yangu inanikatalia kabisa.

Sitaki kuamini kuwa tumeanza kuwatengeza akina Hendrik Verwoerd na Eugene Terre Blanche weusi katika visiwa vya Zanzibar.

CCM Zanzibar inamuiga nani katika hili?

Hitler na Manazi walikuwa na vijana wao waliojulikana kama Stormtroopers ukipenda waite Brown Shirts?

Zanzibar tumeshawashuhudia Ton Ton Macout mfano wa wale wa Papa Doc wa Haiti visiwani wanajulikana kama Mazombie.

Sasa tumefungua ukurasa mwingine wa Adolf Eichman.

Hilo bango mbona litawagusa wengi katika safu ya uongozi wa siasa katika Zanzibar na wengine walipatapo hata kuiongoza nchi?

Machotara?

Nani huyu chotara?

Tumehama kwa Waarabu sasa tuko kwa Machotara!

Lakini huyo chotara si ana wajomba, babu, bibi na mama wakubwa na wadogo Waafrika?

CCM imefilisika kiasi hiki?

Nini hiki ni kiwewe cha CCM kushindwa uchaguzi au ni kitu gani?

Nini khasa tafsiri ya mambo haya?

Tusubiri In Sha Allah wakati utatupa jibu.

Kasema Mwalimu Nyerere karne ya ishirini na moja kuna watu wanapanda basi la ukabila...

Hawa wanapanda jahazi la ugozi.
hahahahah! huyu fukara anachekesha sana na bango lake, mimi mwenyewe ni chotara nina hela maisha matamu nakula vitamu na mama anapata mahitaji yote muhimu, hata machotara wenzangu akina rostam, mo, bakhessa, nk tunakula mema ya nchi. sasa huyu fukara wa kipato na akili kutoka lumumba na hako kabongo kake anafikiri anaweza kutuzuia sisi tembi tusinywe maji?! afie mbali na umasikini wake
 
Ndomana muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar ni muhimu kwani huu muungano ukivunjika ndugu zetu wazanzibar nao watatengana tuu !
 
Unajua unapoona ujumbe unatolewa kwenye bango katika maandamano, tena katika siku maalumu kama hiyo basi ujue kwamba hayo yamekuwa yakiongelewa saana na wahusika katika maskani zao, vikao vyao vya chai na mikutano isiyokuwa na ajenda au rasmi. Kwa uwezo wao wa kufikiri walidhani wanajenga kumbe ndo wanadhihirisha jinsi ambavo wana myopic thinking.
 
...." Mtu akifilisika kisiasa as upon in a LaKisha kiudini atajihalalisha kiukabila..."

Dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu utaendelea kula tu, ccm imesahau kauli za muasisi wao, imezalisha kikundi cha magaidi wala si chama cha kisiasa, Ubaguzi huu kinaonyesha chama kikifikia kikomo chake na kikakosa mwelekeo na kikielekea kaburini, matumizi ya nguvu, ubaguzi na kila ubabe na kupora ushindi inakuwa kawaida

Ccm imeiba kiaina sasa haina tens maono
 
Mwl nyerere hata mzimu wake haufanyi kazi????maana yote aliyowakataza ndo mmeyabebea mabango,hao waarabu wakianza kukinukisha msianze kutafuta huruma,maana myafanyayo ninyi ndo yale yale ya Saddam
 
DSC_2469.jpg

Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akipokea matembezi ya Vijana hao waliotembea katika Mikoa Minee ya Kichama katika kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyomalizia leo katika viwanja vya maisara Suleiman Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]

Picha hiyo hapo juu ni bango la Kikaburu katika mwaka wa 2016 bango linalotukuza ubaguzi wa rangi.

DSC_2827.jpg

Sitaki kuamini kama Ali Mohamed Sheni na uongozi wa juu wa CCM Zanzibar wamewatuma vijana hawa kufanya haya.

Akili yangu inanikatalia kabisa.

Sitaki kuamini kuwa tumeanza kuwatengeza akina Hendrik Verwoerd na Eugene Terre Blanche weusi katika visiwa vya Zanzibar.

CCM Zanzibar inamuiga nani katika hili?

Hitler na Manazi walikuwa na vijana wao waliojulikana kama Stormtroopers ukipenda waite Brown Shirts?

Zanzibar tumeshawashuhudia Ton Ton Macout mfano wa wale wa Papa Doc wa Haiti visiwani wanajulikana kama Mazombie.

Sasa tumefungua ukurasa mwingine wa Adolf Eichman.

Hilo bango mbona litawagusa wengi katika safu ya uongozi wa siasa katika Zanzibar na wengine walipatapo hata kuiongoza nchi?

Machotara?

Nani huyu chotara?

Tumehama kwa Waarabu sasa tuko kwa Machotara!

Lakini huyo chotara si ana wajomba, babu, bibi na mama wakubwa na wadogo Waafrika?

CCM imefilisika kiasi hiki?

Nini hiki ni kiwewe cha CCM kushindwa uchaguzi au ni kitu gani?

Nini khasa tafsiri ya mambo haya?

Tusubiri In Sha Allah wakati utatupa jibu.

Kasema Mwalimu Nyerere karne ya ishirini na moja kuna watu wanapanda basi la ukabila...

Hawa wanapanda jahazi la ugozi.
Mkuu Mohamed Said , kesho wamesema watabeba bango lenye andiko lipi ?
 
Folks: huyu mjumbe kasema hataki Hizbu; ni haki yake. Kama wewe unataka Hizbu sema hivyo na wewe ni haki yako. Nani kakuzuia? Mbona majuzi tuliona machotara wakiona wanaume wao kwa wao na mwarabu kwani kuna mtu kalalamika.
Hivi Ali Karume au labda Mohamed Aboud wale si machotara ?

Siasa za ccm ni za kishamba sana !
 
hawa jamaa ni watu hatari sana,wanafiki,wauaji na sasa wanajionyesha waziwazi,kama mamba wanakutafuna huku wakilia
juzi tu kinondoni kwenye kampeni za UCHAFUZI wa marudio, wamemchezesha mtoto mdogo wa miaka isiyozidi mitano style za chura akibinua makalio wakimtayarisha kuja kutoa tigo miaka michache baadaye ila hadi leo hawajakemewa wala kuchukuliwa hatua,madai yao ni nchi yao wana hatimiliki
Capture.PNG
 
daaa hapa kweli balaa, tatizo hawa viongozi wetu wana ubaguzi hatari yaan wao ukiwapinga tu wanakuchukulia kama mhain wakati wanajua tulikubali mfumo wa vyama vingi ambao unahusisha mawazo tofauti katika kujenga nchi, hii sasa imepelekea chuki kubwa sana ambayo kwa hapa tulipofikia sidhan kama ccm watakuja kutuletea kiongozi atuunganishe wote kwa pamoja kama zaman maana hata marais wastaafu wako kimya kana kwamba hawayaon haya mambo sijui ni kwa sababu wanaogopa wakimkosoa jamaa atawadili na wao, wengine mpaka wanafika hatua wanataka jamaa aongezewe mda hii ni hatari kwa kweli.
 
Back
Top Bottom