Freeland
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 14,481
- 10,227
sio Zanzibar tu..huku bara CCM Wanafanya sana siasa hizoBila ya ubaguzi CCM kamwe haiwezi kushinda Zanzibar , kampeni za marejeo ya uchaguzi zimeanza
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sio Zanzibar tu..huku bara CCM Wanafanya sana siasa hizoBila ya ubaguzi CCM kamwe haiwezi kushinda Zanzibar , kampeni za marejeo ya uchaguzi zimeanza
Itakuwa una tabia za kishenzi ndio ulidharaulika. Ulikuwa unatongoza watoto wa jirani zako, unalewa mpaka unajisahau mchana kweupe, unabadilisha wanawake kila siku humo kwenye kijichumba ulichokodi, unafanya kijichumba chako ulichokodi kama bar, unatukana tukana ovyo na una tabia za kitapeli. Huo ndio utakuwa wasifu wako inavyoonesha.
Ndugu zangu!
Ubaguzi zanzibari ni jambo la kihistoria! Ni jambo linalohusisha mambo yaliotokea katika historia ya zanzibar.
Na bahati mbaya sana athari hizo za kihistoria na kijamaii bado zinaendelea leo zanzibari tena kwa kasi kubwa sana!
Kwa uoni wangu:
tatizo hili ni kubwa ambalo halitakikani kuachiwa wanasiasa! Kwani hawana uwezo wa kulimaliza peke yao!
Kinachotakikana ni jamii kwa ujumla ikiongozwa na viongozi wa kidini zanzibar kuanzisha kampeni ya nyumba kwa nyumba na katika nyumba za ibada na kwenye viwanja na mashuleni ya maridhiano na kufuta athari za ubaguzi za tangu zamani!
Ni jambo la kushangaza baadhi ya taasisi za dini zanzibari kun'gan'gania kwenye mambo ya kisiasa na kuacha jamii ikiendelea kupasuka!
Taasisi kama uamsho na baraza la maimamu la zanzibar kujikita kutoa matamko ya kisiasa na kuacha kuhudumia jamii kufuta ubaguzi wa kihistoria ni jipu chungu sana ambalo wanahitaji wajitumbue wenyewe!
Ndugu zangu!
Zanzibari kumekua na nadharia za kiubaguzi kijamii hadi kizazi cha sasa kuambukizwa kwa kiasi kikubwa sana! Unadhani hayo hayawezi kuathiri kwenye siasa? Tena kwenye vyama vyote?
Nadharia za kibaguzi kijamii zanzibar zimekua zikikuzwa siku hadi siku, kutokana na wazazi kuwarithisha watoto wao!
Baya zaidi nadharia hizo hazikuishia kubaguana wazanzibari tu! La hasha! Bali kuna kundi kubwa la wazanzibari wameathirika na nadharia hiyo na kufikia hata kuwabagua wasio wazanzibari kwa hoja za kipuuzi kabisa!
Hayo yanashuhudiwa katika jamii na miji mbali mbali pamoja na mashuleni na vyuoni!
Miongoni mwa mifano ya kushangaza kabisa ya athari za nadharia hiyo: ni unapokuta watanzania bara kuwaozesha kwa moyo mmoja tu dada zao na watoto wao kwa wazanzibari kwa kuzingatia sheria halisi za kindoa bila kujali kama huyu mume anatoka zanzibar.
Lakini wengi mwa wazanzibari wamekua wakikataa kata kata kwa mtoto wa kiume wa kitanzania bara kuoa mtoto wa kike wa kizanzibar, hususan kutoka pemba!
Na hata kama mtoto wa kike amekubali, lakini anapewa vitisho na wazazi na kuambiwa maneno yanayomjenga chuki na ubaguzi dhidi ya wabara, kama vile kusema: utaolewaje na mtwana?
Utaolewaje na libara?
Na mfano wa hayo!!
Nasema haya nikiwa na ushahidi kamili wa yaliotokea na kushuhudia kwa macho na masikio yangu yakisikia!
Hii ni nadharia ilioanzia mbali ambayo kizazi hiki cha sasa cha wazanzibari kimekua wahanga wakubwa sana!
Akina mzee muhammed saidi na wengine, wallaahi ningefurahi sana kama mtajikita kutoa juhudi zenu za kiuandishi na ushauri na kuunda mabaraza ya usuluhishi ili kuinusuru hii hali!
Ni aibu kubwa sana kwa wazanzibari kuwa katika hali hiyo!
Na hilo bango la kibaguzi hapo juu mimi siliungi mkono, lakini linaelezea hali halisi ya jamii ya zanzibari katika swa hili.
Na haina maana kama hilo bango lisingenyanyuliwa basi tatizo la ubaguzi lisingekuepo.
Lazima tujue asili ya tatizo na jinsi ya kulimaliza.
Sio kila kitu tukiegemeze kwenye siasa tu!
Itakuwa labda ulilewa mpaka kupindukia vijana wakakufanyia mchezo wa Kizanzibar, ndio ikakufanya ukawa na chuki na Wazanzibar, sio bure.Ubaguzi utawaua.
Mlianza na watu wasio wa Zanzibar sasa mmeanza kunyosheana vidole wenyewe kwa wenyewe.
Nimezungumzia juu ya ubaguzi wewe unaleta habari za kudharaulika,una akili kweli?
Nasema baguaneni tu mpaka mtoboane macho ndo mtaheshimiana wala msianze kusingizia hao vijana wa CCM maanake hiyo ndo tabia ya wazanzibar wote.
Hapo ndipo ujue kuwa chama kikongwe kabisa cha siasa hapa nchini kimefikia mwisho na hicho wanachokifanya CCM naweza kukiita kuwa ndiyo the last kicks of the dyeing horse.Kweli CCM znz mmechoka. Ujinga huu mbele ya rais? Kweli viongozi wa ccm znz ni wajinga kiasi hiki? 2016?
Itakuwa labda ulilewa mpaka kupindukia vijana wakakufanyia mchezo wa Kizanzibar, ndio ikakufanya ukawa na chuki na Wazanzibar, sio bure.
Ubaguzi ni kujiona jamii yako ni bora kuliko nyengine = Kuidharau jamii nyengine juu yako. Ni mbwa kumwita jibwa.
Nakubaliana nawe kwa asilimia 98 kuhusu vijana hao kuweka bango hilo. Lakini lazima pia tuwe wakweli. wale waarabu waliondoka Zanzibar baada ya mapinduzi au waarabu hao waliopinduliwa bado wanadai (siyo rasmi) kuwa Zanzibar ni yao na kwamba kwa kuwa waliondolewa kwa mtutu wa bunduki watarejea kupitia sanduku la kura. Sasa hapo ndipo tatizo. Kinachoonekana hapa ni kuwa waarabu hao wanatumia baadhi ya viongozi wa CUF kutaka kurejea Zanzibar kwa njia ya kura...
Ndugu zangu!
Ubaguzi zanzibari ni jambo la kihistoria! Ni jambo linalohusisha mambo yaliotokea katika historia ya zanzibar.
Na bahati mbaya sana athari hizo za kihistoria na kijamaii bado zinaendelea leo zanzibari tena kwa kasi kubwa sana!
Kwa uoni wangu:
tatizo hili ni kubwa ambalo halitakikani kuachiwa wanasiasa! Kwani hawana uwezo wa kulimaliza peke yao!
Kinachotakikana ni jamii kwa ujumla ikiongozwa na viongozi wa kidini zanzibar kuanzisha kampeni ya nyumba kwa nyumba na katika nyumba za ibada na kwenye viwanja na mashuleni ya maridhiano na kufuta athari za ubaguzi za tangu zamani!
Ni jambo la kushangaza baadhi ya taasisi za dini zanzibari kun'gan'gania kwenye mambo ya kisiasa na kuacha jamii ikiendelea kupasuka!
Taasisi kama uamsho na baraza la maimamu la zanzibar kujikita kutoa matamko ya kisiasa na kuacha kuhudumia jamii kufuta ubaguzi wa kihistoria ni jipu chungu sana ambalo wanahitaji wajitumbue wenyewe!
Ndugu zangu!
Zanzibari kumekua na nadharia za kiubaguzi kijamii hadi kizazi cha sasa kuambukizwa kwa kiasi kikubwa sana! Unadhani hayo hayawezi kuathiri kwenye siasa? Tena kwenye vyama vyote?
Nadharia za kibaguzi kijamii zanzibar zimekua zikikuzwa siku hadi siku, kutokana na wazazi kuwarithisha watoto wao!
Baya zaidi nadharia hizo hazikuishia kubaguana wazanzibari tu! La hasha! Bali kuna kundi kubwa la wazanzibari wameathirika na nadharia hiyo na kufikia hata kuwabagua wasio wazanzibari kwa hoja za kipuuzi kabisa!
Hayo yanashuhudiwa katika jamii na miji mbali mbali pamoja na mashuleni na vyuoni!
Miongoni mwa mifano ya kushangaza kabisa ya athari za nadharia hiyo: ni unapokuta watanzania bara kuwaozesha kwa moyo mmoja tu dada zao na watoto wao kwa wazanzibari kwa kuzingatia sheria halisi za kindoa bila kujali kama huyu mume anatoka zanzibar.
Lakini wengi mwa wazanzibari wamekua wakikataa kata kata kwa mtoto wa kiume wa kitanzania bara kuoa mtoto wa kike wa kizanzibar, hususan kutoka pemba!
Na hata kama mtoto wa kike amekubali, lakini anapewa vitisho na wazazi na kuambiwa maneno yanayomjenga chuki na ubaguzi dhidi ya wabara, kama vile kusema: utaolewaje na mtwana?
Utaolewaje na libara?
Na mfano wa hayo!!
Nasema haya nikiwa na ushahidi kamili wa yaliotokea na kushuhudia kwa macho na masikio yangu yakisikia!
Hii ni nadharia ilioanzia mbali ambayo kizazi hiki cha sasa cha wazanzibari kimekua wahanga wakubwa sana!
Akina mzee muhammed saidi na wengine, wallaahi ningefurahi sana kama mtajikita kutoa juhudi zenu za kiuandishi na ushauri na kuunda mabaraza ya usuluhishi ili kuinusuru hii hali!
Ni aibu kubwa sana kwa wazanzibari kuwa katika hali hiyo!
Na hilo bango la kibaguzi hapo juu mimi siliungi mkono, lakini linaelezea hali halisi ya jamii ya zanzibari katika swa hili.
Na haina maana kama hilo bango lisingenyanyuliwa basi tatizo la ubaguzi lisingekuepo.
Lazima tujue asili ya tatizo na jinsi ya kulimaliza.
Sio kila kitu tukiegemeze kwenye siasa tu!
Safi well said mkuu Mwenyewe Magu hana uhalali wa kuwa pale na anajua hilo........
hapo msimtegemei Makufuli kuleta muafaka,hapo tegemeeni Makufuli kuzidisha mtafaruku kwa kuwa upande wa ccm na ndio mtakubaliana nami kwamba, Makufuli hana ubavu wa kuongoza nchi hii kwa haki
Nimecheka sana kuona anayelalamika ni mohamed said. huyu ambaye amakeuwa na ubaguzi kwa wakristo , ubaguzi kwa tanganyika na hata kuwabagua watu wengine kwa misingi ya imani yao.
zanzibar UBAGUZI UPO SANA hasa kwa WABARA NA WAZANZIBAR. ukifanyika hivyo mohamed said haoni kama ni unabaguz. ukifanyika ubaguzi wa dini haoni kama ni ubaguzi. ubaguzi ni mbegu ukiipanda itaota na itakua. asilimia 99 ya wazanzibar ni waislamu....wakiwabagua wakristo mi naelewa na wala siwezi walaumu ila wasidhan watabaki salama .....na sasa ndo tunaona kuwa kumbe ubaguzi huwa unakua,unasambaa UBAGUZI NI KANSA. USIPOKATA SEHEMU ILIYOATHIRIKA INASAMBAA MWILI MZIMA.... kumbe nako zanzibar pamoja ya kuwa wote ni wazanzibar ila kuna wahizbullah na weusi tii. kuna machotara na waafrika halisi. na bado ubaguzi huu utashuka tu. na muishukuru sana TANGANYIKA MAANA NDO INAWASAIDIA OTHERWISE HALI INGEKUWA MBAYA ZAIDI.
Zanzibar mmetuchosha jamani. Kila uchwao ni keleleeeeeeee hadi kero. Hivi ccm si wampe huyo maalim seif huo uraisi hizi kelele ziishe. Kwani kuna aliyezaliwa kuongoza milele? Arghhhh mwisho wa siku mtajiletea maafa bure mfe nyie na watoto wenu.
Miafrika sijui ikoje