gnassingbe
JF-Expert Member
- Jun 14, 2015
- 4,826
- 3,585
Marekebisho kidogo kwenye rangi isomeke mzungu nadhani.Machotara tumepata ujumbe.Kumbuka Muhindi na Chotara ni watu wawili tofauti.Chotara amechangia damu ya Uafrika na mwenye asili ya weupe yaweza kuwa Muarabu,Muhindi au Mungu.
Hongereni CCM kwa double standard.Hope angekuwa aliye weka bango hilo ni mwanachama wa CUF au Chadema toka Jana angekuwa jela akisubiria kesi yake kutajwa kesho.
Lakini kesi ya jinai iwe ameua,ameiba,ametukana nk nk husihia kuwekea kwenye mitandao ikisema CCM wa naomba radhi kwa kosa lililofanywa na watu wasio julikana au na mwananchi mmoja.
Kwanini msiseme UVCCM? Mnahofu ya nini??Machotara tumepata ujumbe.
Jaribu kuelewa ndugu, mimi nazungumzia tatizo la ubaguzi zanzibari na njia ya kulimaliza, na wala sitetei chama fulani cha siasa.
Kwasababu hata kikiingia chama kingine madarakani huu ubaguzi nilioueleza kua ni wa kihistoria na kijamii hauwezi kuisha.
Na hicho chama hakitaweza kulimaliza tatizo hilo bila kuwa na mikakati madhubuti ya kushiriki jamii nzima kama nilivyoeleza hapo juu.
Uzushi mtupu, kwa nini mnakawaida ya kukimbilia kutumia karata hii mambo yanapo waendea ndio sivyo?Nakubaliana nawe kwa asilimia 98 kuhusu vijana hao kuweka bango hilo. Lakini lazima pia tuwe wakweli. wale waarabu waliondoka Zanzibar baada ya mapinduzi au waarabu hao waliopinduliwa bado wanadai (siyo rasmi) kuwa Zanzibar ni yao na kwamba kwa kuwa waliondolewa kwa mtutu wa bunduki watarejea kupitia sanduku la kura. Sasa hapo ndipo tatizo. Kinachoonekana hapa ni kuwa waarabu hao wanatumia baadhi ya viongozi wa CUF kutaka kurejea Zanzibar kwa njia ya kura...
Kama ilivyo hata huku bara viongozi wengi wa CCM wameoa wachagga kama sio Kaskazini lakini ndio wakwanza kuwapandikizia majungu na kuwabagua watu wa huko..Cha kushangaza hao viongozi wote wa CCM karibia wote wake zao ni machotora na watoto wa ni machotora.
Tinta wacha kuwa biased na unachoandika. Mbona suluhisho ya huo ubaguzi tayari lipo kikatiba. Katiba ya kuanzishwa kwa vyama vya siasa inatamka wazi kabisa Vyama vya kisiasa viwe vya kitaifa na visiwe na mlengo wa dini ama ubaguzi wa aina yoyote. Tatizo letu liko kwenye kufuata hiyo sheria na katiba yenyewe. Linapokuja suala la kufuata sheria CCM ndio mvunjaji mkubwa wa sheria za nchi. Shein kashindwa uchaguzi hataki kuachia madaraka! CCM inaendeleza ubaguzi kwa vitendo na maneno lakini hakuna wa kuweza kuwachukulia hatua kwa sababu wana nguvu za dola. Mimi nakushauri usianze kuzunguka mbuyu wala kutafuna maneno, Kikatiba basi CCM inapaswa kufutwa na msajili wa vyama. Ona hata yeye yuko kimya kwa jambo hili.
Asante ni kweli inatakiwa kuwa MzunguMarekebisho kidogo kwenye rangi isomeke mzungu nadhani.
Nafikiri linaweza kupunguza sana tu.Sababu nazijua siasa za ZenjiKwani wewe unadhani maalim sefu akipewa nchi ubaguzi zanzibar utakua umekwisha?
Na je ubaguzi zanzibari uko kwenye siasa tu?
Na je ni sababu gani ya msingi iliojenga misingi ya ubaguzi zanzibari hata kabla ya kuwepo ccm?
Na unasemaji ubaguzi ambao nimetaja kua kuna kundi kubwa la wazanzibar limeathirika nao? Ikafika hatua ya kuwabagua hata wabara leo hii na kuwaita watwana?
Je dawa ya ubaguzi wa kijamii utaisha tu pindi sefu akichukua nchi?
Tatizo lako wewe umeangalia athari ya ubaguzi kwenye siasa tu! Hilo ni dogo ndugu! Tatizo ni kubwa zaidi ya hapo mara elfu kumi!
Wanawajua na kuijua zanzibari vizuri wanafahamu.
Mohamed Said has never and will never be consistent in his arguments.Mohammed Said usiwe mnafiki.
Wewe ni mmoja wa watu humu mtandaoni mlioendeleza ubaguzi, kwako ulikuwa wa kidini.
Mwalimu aliwaonya, na sasa utabiri wake unatimia.
Mwalimu alisema,
"Zanzibar ikianza kujibagua toka Bara hawatabaki salama maana slama ya Zanzibar ni umoja na Bara.
Wakiisha kuwabagua Bara watakuwa wamefanya dhambi kama wachawi wanaokuka nyama ya watu.
Ulila nyama ya mtu utaendelea kula nyama ya mtu.
Mwalimu aliendelea kuwa, baadaye Wazanzibari wataendeleza dhambi ile ile ya ubaguxi na kugundua kua Zanzibar kuna Wazanzibari na Wazanzibara, na kuna Wapemba na Waunguja, hawatabaki salama hata kidogo"
Leo Mohammed Said, ukiwa mtu mzima mwenye akili yako washangaa nini, umeuendekeza sana ubaguzi wa kidini na makala zako za kuwa sifia na kuwaenzi "wazazi wako waislamu" humu mtandaoni, kwamba ndo walileta uhuru.
Ulihusika moja kwa moja kupanda mbegu za chuki katika jamii.
Zanzibar walipoanza na sera za kujibagua, ili wapate kujitambulisha nani ni mzanzibari(kwa kuwabagua wabara) sikuwahi kuona makala zako za kuonya juu ya ubaguzi huu.
Wengi tulilaumu hili, lakini kwa vile wazanzibari kupitia Baraza La Wawilishi, ndo liliendeleza ubaguzi huu hadi kufikia hatua ya kumpiga mrufuku ya kukanyaga Zanzibara Waziri Mkuu Pinda, wengi walishangaa ubaguzi na umoja wa kibaguzi wa wazanzibari.
Lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kuonya juu ya hili.
Leo mbele ya kadamnasi u Hizbu na u ASP unaonyeshwa hadharani- tofauti zilizokuwepo hata kabla ya uhuru.
Halafu mtu mwenye akili unailaumu CCM.
HUU NI UNAFIKI MKUBWA.
Mnavuna mlichopanda, na Mwalimu was right, salama ya Zanzibar ni Tanganyika.
Cha kushangaza hao viongozi wote wa CCM karibia wote wake zao ni machotora na
watoto wa ni machotora.
Kwani wewe unadhani maalim sefu akipewa nchi ubaguzi zanzibar utakua umekwisha?
Na je ubaguzi zanzibari uko kwenye siasa tu?
Na je ni sababu gani ya msingi iliojenga misingi ya ubaguzi zanzibari hata kabla ya kuwepo ccm?
Na unasemaji ubaguzi ambao nimetaja kua kuna kundi kubwa la wazanzibar limeathirika nao? Ikafika hatua ya kuwabagua hata wabara leo hii na kuwaita watwana?
Je dawa ya ubaguzi wa kijamii utaisha tu pindi sefu akichukua nchi?
Tatizo lako wewe umeangalia athari ya ubaguzi kwenye siasa tu! Hilo ni dogo ndugu! Tatizo ni kubwa zaidi ya hapo mara elfu kumi!
Wanawajua na kuijua zanzibari vizuri wanafahamu.