Ubaguzi: Machotara Hizbu, Zanzibar ni nchi ya Waafrika

Kwani uongo jamani, chotara hawezi kupewa hii nchi, atarudisha mabwana zake.
 
Catch 22
Muajemi wa kizazi cha kumi na.mbili na
Mnyamwezi kizazi cha tatu
Fumbo
wanyamwezi wa kizazi cha tatu kivipi ina maana Waajemi walipokuja Znz hawakukuta watu? au ndo mkuki kwa Nguruwe?
 
Last edited:
Hilo bango (UJUMBE) limerudiwa tena leo katika kilele cha maadhimisho ya mapinduzi matukufu. Lakini kuna afisa mmoja wa CCM ameomba msamaha kuwa ni "mwananchi" mmoja pengine kichaa (au adui wa CCM, pengine mwana CUF) ndiye ameliingiza uwanjani ili kuwapaka matope CCM!! Kwa hivyo na Bw (maana kumwita dr ni kujisuta) Shein jana alijigeuza kichaa kwa kukubali kupokea bango hilo!
Niikiri kuwa sio tu nimewadharau ma-CCM, bali pia hili limeongeza chuki yangu dhidi ya haya matarahamwe. Nimemchukia Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, nimemchukia makamo wa Znz na mgombea wa urais (CCM) huyo Shein, nimewachukia mantarahamwe yote ya bara na visiwani.Hamuwatendei haki wananchi wa Zanzibar (weusi, weupe, wabluu, wamanjano, wekundu, nk). Hamwezi kuleta ubaguzi wa rangi wazi wazi katika karne ya 21. Shame on you! Sasa mkisikia weusi wanabaguliwa huko Marekani au weupe wanabaguliwa huko Afrika ya Kusini mtalaani au mtaunga mkono huo ubaguzi? nyambaf Kikwete na Shein & Co
 
CCM NA UNAFIKI ULIOKUBUHU.

Na Kilawa the Iron.

Chama cha mapinduzi kimedhihirisha unafiki wake kwa vitendo. Chama hiki kimekuwa kikijinasibu kuwa ni chama cha watu maskini, wakulima na Watanzania wote kinyume na matendo ya chama hiki.

Bila aibu wala haya leo katika sherehe zinazosherekewa kila mwaka kukumbuka mapinduzi ya kishujaa yaliyafanyika Tr 12/01/1964
Kijana wa CCM ambaye hadi sasa haijajulikana kama ni mwanachama tu au ni kiongozi wa chama hicho ameonekana akiwa ameshikilia bango kubwa la kibaguzi na linalojenga chuki kwa wananchi wa Zanzibar na ulimwengu mzima.

Kijana huyo alishika bango kubwa liloandikwa kwa ustadi na likionekana limefanyiwa maandalizi ya mda mrefu linasomeka hivi
"MACHOTARA HIZBU ZANZIBAR NI NCHI YA WAAFRIKA" je huu sio unafiki wa watu hawa waliotawala kwa miaka yote hii.

Kwanini nasema CCM ni wanafiki? nasema hivi kwa sababu kuu zifuatazo:-

Bango hili linaonekana limeandaliwa kwa umakini likiwa na lengo mahususi kisiasa ndani ya CCM hivyo linadhihirisha kuwa watu hawa wanapenda ubaguzi, na wametudhihirishia kwamba wao ni watu wasiopenda haki, usawa na utawala bora.

Kama bango hili halikuwa kimkakati ni kwanini waliruhusu kijana huyu aingie na bango hili na hata likatumiwa kwa mda wote? je Greenguard, polisi na viongozi wao waliridhishwa na bango hilo hadi kuacha litumike katika sherehe ya kishujaa?

Lakini kama hawakuridhisha au kulipenda bango hilo kwanini viongozi wa CCM walikaa kimya hadi walipoona matamko ya wapinzani kulaani kitendo hicho? ndipo mtu anayeitwa Daniel Chongolo alipoamua kuomba radhi

Kiujumla ni kwamba CCM inakwenda kinyume na imani ya chama chao ambayo inahubiri kuwa "Binadam wote ni sawa" hivyo kwa mktadha huo hakuna usawa badala yake ni ubaguzi unaopandikisha chuki za kudumu vitendo hivi vilaniwe na wapenda haki wote duniani.

Mwisho nimemsikia Dr Shein katika hotuba yake akisema kuwa serikali yake imefanikiwa kulinda na kudumisha demokrasia nchini Zanzibar, pia kudumisha na kuulinda muungano ilihali yeye hadi sasa yupo madarakani kinyume na katiba na sheria za nchi yake

Haya yote yanadhihirisha unafiki wa chama hicho nchini, Kiujumla sisi tunalaani kwa nguvu zote ubaguzi wowote unaoendelezwa na ccm hali itakayojenga chuki za kudumu miongoni mwetu.

Sote ni wanadamu, sote tumeumbwa na Mungu mmoja tuache kuyafanya mambo kwa maslahi binafsi zaidi tuangalie maslahi mapana ya Taifa.
Ahsante.
Msema kweli mara zote huchukiwa na watenda mabaya
 





Mohamed Said nakupongeza kwa ujumbe wako murwa kabisa. japo naona kuna baadhi ya wajumbe humu ndani wamekuona mnafiki lakini ulichosema ni kweli kuwa vijana hawa hawajafanya jambo la kiungwa na sijui viongozi wao wana waza nini.
Ndani ya ccm wapo makaburu na kama wanafikiri Wapinzani wa ccm ndiyo pekee makaburu kama alivosema baba yetu mwalimu Nyerere, baada ya kuwaondoa hao makaburu walio nje ya ccm wataingia ndani ya ccm na hapo ndipo kutakuwa sherehe kubwa kwao.

Zanzibar ni nchi ya watu wote hakuna cha mweusi au mrangi wote ni wazanzibar. natumai viongozi wa ccm Taifa watatoa kauli kali juu ya kitendo kisicho cha uungwana kilichofanywa na vijana hao wa ccm.
 
Pia alisema 'kaburu ni kaburu tu, hata kama ni mweusi lakini una mawazo kama makaburu wa South Africa wewe ni kaburu tu'
 
Catch 22
Muajemi wa kizazi cha kumi na.mbili na
Mnyamwezi kizazi cha tatu
Fumbo
Naomba kuuliza Hizbu Chotara wanatambulikaje? Sura, rangi, nywele na macho. Hilo bango lingefafanua
 
Shein mwenyewe ni chotara .......................!!!
Shein ni chotara mweusi...wao wanazungumzia chotara weupe na sio chotara weusi wala chotara wa maji ya kunde. Wakati huo huo watahamia kwa wapemba dhidi ya waunguja...kisha watahamia Wazanzibari wenye asili ya Oman na wenye asili yaTabora.

CCM wasipofanya jambo la kusaidia mapema yatakuja tokea mabaya sana.
 
Nakuunga mkono kwa asilimia mia moja, na kuna siku Mungu atatenda maajabu mi ccm ianguke, kwa sasa anaipumbaza akili kwanza hii mi ccm kwa namna ili ijione yenyewe ndio yenyewe.
 
Naungana nawewe kwa kiasi kikubwa kabisa,na sababu ni kwamba umenifanya nikarecall na kurefer mambo mengi sana ambayo yamekuwa yakinenwa na kuandikwa na Viongozi flan wa zanzibar over the years pamoja na wadau wengine waliokuwa wakiitetea zanzibar na sasa wamegeuka Mamluki kwa unafiki. Kwa upande wa visiwa vingine sina uhakika.

Mwenyezi Mungu alisema bora uwe Moto au Baridi. Ukiwa vuguvugu atakutapika.

NIMEKUELEWA SANA MKUU.
 
Mkuu wewe hujuwi Asp imeanzaje ni mungano wa waafrica na washirazi hawa washirazi ndio machotara za naona wameshageukana sasa hawa kazi imeanza ukiwa kaburu ni kaburu tu kesho watageukana waafrica kwa waafrika itakuwa mmakonde na msukumal
 
Mkuu. Dunia yaleo hakuna muwarabu anaetaka kirudi znz kuitawala.
Na isitoshe waarabu wapo znz na haitatokea waarabu kufutika znz itachukuwa karne nyingi waarabu na silka za kiarabu kufutika znz.
Waarabu wapo ccm waarabu wapo cuf waarabu wapo mitaani znz.
Isitoshe hata tamaduni za znz nyingi ni za kiarabu.
Hao wanao sema chotara waondoke sio tu hawaitakii mema znz wajue pia hawazitakii mema ndoa zawatu.
Maana viongozi wengi wengi wa ccm znz wake zao ni machotara.
 
Kila siku UKAWA mnawaandama wahindi kuhusu kuishi kwao kwenye nyumba za NHC...Leo ndio mnajifanya kuwatetea!?

Kumbukumbu zangu Zinasema aliyegombea ilala Chadema alikuwa muhindi. Sijaelewa wanaandamwa vipi lini na wapi bwana Lizaboni.

😎😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…