Ubaguzi umezidi, hamu ya kurudi nyumbani inanijia kwa kasi

Nimekomaa sana. Nilisema labda niiende kuishi English speaking countries kama Canada au Australia mambo ni yale yale tu. Chuki na ubaguzi naskia huko Canada ubaguzi umetawala. Licha ya kutaka wahamiaji lakini wana deport sana hata ukiiba supermarket.
Kwanini unafikiri kuiba supermakert ni jambo dogo na la kuvumilika?

Unashangaza sana, au ndo tabia zako huko ughaibuni?
 
We mzee bangi uliyovuta leo umeitoa wapi😂😂😂😂😂
 
Mkuu upo sahihi. Lakini nadhani waswahili tuna shida ya attitude. Ukienda na akili ya maisha ya kibongo bongo lazima huko nje utafeli tuu. waAfrica wengi ambao nimekutana nao, kwanza tunapenda attention na recognition-tunapoyapatia maisha....

Mimi wakati naenda nje for the first time, nilijiwekea kichwani kwamba naenda kutafuta maisha. Maamuzi nimeyafanya mimi sikulazimishwa. Huwezi amini, kwa sababu mind yangu nili-iset, sijawahi kuhisi kwamba nabaguliwa kwa sababu ya ngozi yangu (na nimekaa some of the countries famous kwa ubaguzi both in North America and Europe). Hiyo attitude imenilinda mpaka leo.

Ukisikiliza media sana na story za vijiweni, utajikuta maisha unayachukia ghafla (kikubwa ni kutambua kwamba experience ya kila mtu ni tofauti). US kila mtu anajua kuna ubaguzi. SA, Germany, UK, France, kote huko ubaguzi upo. Lakini pia, ni nchi ambazo ukipambana utafanikiwa sana tuu. na wapo wengi ambao wamefanikiwa.

Siku zote nikiwa nje nilikuwa najiuliza, will I be better off nikirudi bongo? Jibu la hili swali lazima uwe nalo mda wote wa maisha yako. Kila nikikumbuka maisha niliyopitia kutafuta ajira baada ya degree ya UDSM? Nilikuwa njisemea hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!

I always consider my life experience in Europe and North America positively.

Leo nikikutana na kijana mdogo ananiomba ushauri wa kwenda nje kutafuta maisha..nitamwambia nenda! kikubwa kuwa na malengo na uende huko ukiwa bado na nguvu..siyo kwenda kuwa mzigo wa serikali na walipa kodi.
 
Hivi upo Sweden au Denmark?
 
Mda Mwingine Rangi hutubagua yenyewe
 
Maghayo Kwa mzaliwa na kukulia Bongo; akaenda huko majuu na akawa na hulka ya kuingia katika mitandao yetu kama JF au kila siku kusoma magazeti ya udaku ya Tanzania; lazima atajisikia mpweke na atarudi tu. Kama ulivyosema lazima uwe na malengo. Kama unaenda kuchuma na kurudi au kama unataka ukaazi wa huko weka pamba masikioni tafuta toto la kizungu uoe maisha yasonge.

Ukiendekeza ubaguzi huwezi kufanya kitu maishani. Mbona hapa watu tunabaguana lakini tupo. Angali Wazanzibari wanavyobagua wenye vichogo ukienda kwao. Narudia kusema tusi si tusi mpaka mtusiwa aone ni tusi. Je, hapa JF si ukiwa si mpenzi wa Chadema unabaguliwa? Mbona hatukimbii tusiyoiabudu Chadema.

Achana na upuuzi wa kujishuku, mtu akisema waafrika wananuka, sema hewala mbona na wazungu wakiwa Afrika hunuka ile mbaya. Maisha yanasonga. Ukirudi utajuta kuzaliwa maana hapa bila kianzio ni mtihani mkubwa
 
Nani anampenda mwivi? Utoke ulikotoka kwenda kuwa mwivi?
Siyo kupenda wizi. Kuna makosa mengine ni ya kusamehe. Yani unaiba supermarket unadepotiwa hapana. Wizi supermarket kutukana iyo ni offence siyo crime.

Rape, murder, bodily arm, driving carelessly and causing accident hapo sawa deportation labda itahusika.
Unamdeporr mtu kwa commit offence kwa kuiba supermarket kweli iyo inaleta mantiki.?
 
Bongo bado viwanja vya kujenga vipo vingi sanaaa, ukiwa na toyota crown basi utatesa sana mtaani kwa kifupi bongo maisha rahisi sana kama unamkwanja naamini wengi mlio huko nje mkija huishi huku hamtajutia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…