Maghayo Kwa mzaliwa na kukulia Bongo; akaenda huko majuu na akawa na hulka ya kuingia katika mitandao yetu kama JF au kila siku kusoma magazeti ya udaku ya Tanzania; lazima atajisikia mpweke na atarudi tu. Kama ulivyosema lazima uwe na malengo. Kama unaenda kuchuma na kurudi au kama unataka ukaazi wa huko weka pamba masikioni tafuta toto la kizungu uoe maisha yasonge.
Ukiendekeza ubaguzi huwezi kufanya kitu maishani. Mbona hapa watu tunabaguana lakini tupo. Angali Wazanzibari wanavyobagua wenye vichogo ukienda kwao. Narudia kusema tusi si tusi mpaka mtusiwa aone ni tusi. Je, hapa JF si ukiwa si mpenzi wa Chadema unabaguliwa? Mbona hatukimbii tusiyoiabudu Chadema.
Achana na upuuzi wa kujishuku, mtu akisema waafrika wananuka, sema hewala mbona na wazungu wakiwa Afrika hunuka ile mbaya. Maisha yanasonga. Ukirudi utajuta kuzaliwa maana hapa bila kianzio ni mtihani mkubwa