Tetesi: Ubaguzi wa ajira kwenye Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Tetesi: Ubaguzi wa ajira kwenye Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,291
Kuna taarifa za ubaguzi wa ajira ndani ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa wapinzani na hasa watu kutoka kisiwa cha Pemba. Taarifa hizi zinaendelea kuzagaa na kutolewa katikati ya lawama za wakubwa kufumbia macho taarifa hizo au kukanusha bila uthibitisho wa ziada.

Taarifa zinadokeza kuwa mara baada ya kufanyika uchaguzi wa marudio wa Machi, 2016 , mikakati ilipangwa kuhakikisha wapinzani hawapati nafasi za kuajiriwa na vile vile kuhakikisha watu walidhaniwa kuwa wapinzani wanaondolewa katika vitengo nyeti. Taarifa zinadokeza kuwa zoezi hili limefanyika kwa asilimia zaidi ya 90%

NAMNA UBAGUZI UNAVYOFANYWA.

Taarifa zinaeleza kwamba zoezi la uajiri wa nafasi mpya, linaratibiwa vyema kwa kushirikisha vyombo vya usalama (usalama wa taifa) na UVCCM, Vijana wa UVCCM waliomo serikalkini na mawakala wao kwenye TISS wametengeneza mtandao kuhakikisha kila nafasi inashikiliwa na mwana CCM au wanaoitwa ":watu wetu". Mkakati huu umepangwa na kupata baraka za ofisi moja Kupitia Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar.

Taarifa zinasema kuwa kumekuwa na hamisha hamisha ya wafanyakazi hasa wa utumishi kwenye vitengo ambao waliokuwepo huondolewa na kuchomekwa watu wa mfumo ili kufanikisha suala hili. Kuna idara nyingi na hata taasisi zenye bodi na mashirika zinaingiliwa majukumu yake na Utumishi mkuu kwa watu kuhamishwa na mamlaka ya bodi hizo kunyanganywa kwa kisingizio cha "Utumishi Mkuu"

Zipo taarifa kuwa hata zile nafasi zinapotangazwa zilizohitajika zijazwe na watu kutoka Pemba kwa mfano, hupelekwa watu kutoka Unguja au Bara ambao wanaaminika kuwa wako upande wa Utawala na kuchukuwa nafasi hizo.

MAJIBU MEPESI.
Kupitia tuhuma hizo, Waziri wa nchi ofisi ya Makamo wa pili wa Rais( Mh Muhamed Aboud) amewahi kutolea ufafanuzi suala hili na kubainisha kwamba hakuna ubaguzi na mchakato unakuwa wa wazi ambapo hutangazwa na wenye sifa ndio wanaajiriwa jee huo ndio ukweli ?

Taarifa zinasema hilo sio tatizo, Sheria ya Utumishi wa ummma imeeleza vyema kuhusu mchakato ambapo nafasi hutangazwa na wenye sifa ndio wanatakiwa kuajiriwa, Hapa tatizo si mchakato, Tatizo ni DHAMIRA, inaelezwa kuwa mkakati ni kuwa hata kama mtu ana sifa ilimradi ni Mpinzani anatafutiwa mazingira ya kuachwa. Zipo taarifa kuwa imefika mahali watu wana sifa na wameshachaguliwa na kuhojiwa halafu wanaachwa baada ya kufanyiwa "veting" na kile kitengo kinachoitwa "GSO" Veting hio inasemwa inaelekezwa kwenye siasa na kupekuliwa asili ya familia ya mtu. Hapa ndipo vijana wa mfumo wa UVCCM wanapohusishwa.

Viongozi ama kwa kutojuwa au kwa makusudi hawataki kujiridhisha kadhia hii. Mfano wa karibuni ni uajiri wa walimu na nafasi zinazotangazwa kupitia mashirika na taasisi za Serikali.

ATHARI
Athari ya kwanza ni kuajiriwa watu ambao hawana uwezo na nyengine ni kuigawa jamii. Katika hili Kule Zanzibar , jamii ya watu wa Pemba imeathiriwa sana. Zipo taarifa kuwa ukiwa Mpemba hata kama ni CCM huaminiwi na wako wengi wamekosa kuajiriwa kwa kudhaniwa kuwa wapemba wote ni wapinzani. (huu sio ukweli)

Tetesi hizi ni nyeti. Imefika wakati maofisa wanaohusika na uajiri huwaeleza watu wazi wazi kuwa "...wewe unazo sifa lakini huwezi kuajiriwa, huwa wanasema tatizo liko kwa watu wenu ambao wametoa taarifa kuwa hufai..." Hii ndio hali ilivyo.

Mwandishi amepataa tetesi hizi kupitia kwa vyanzo muhimu na sasa taarifa hizi zimezagaa kule Zanzibar.

MWISHO.
SMZ inatakiwa kuondowa dhana hii kwa vitendo, Kwenye jamii hizi taarifa zpo na hazipaswi kupuuzwa. Wazanzibari wenyewe wanafahamiana na huwa unaambiwa Zanzibar hakuna siri. Ikiwa Mkakati huu upo basi kwa haraka uondolewe kwa maslahi ya Taifa.




Kishada.
 
Yaani vijana wanaambiana na kuhadithiana. Kulikuwa na wimbi la vijana kuchukuwa kadi za CCM ili wapate ajira, zoezi la kutoa kadi likafungwa baada ya wenyewe kushtuka. Sasa kuwa na kadi hakutoshi wanatumika kitengo cha "GSO " kufuatilia nyendo za kifamilia na wakinusa tu harufu ya upinzani kwenye familia basi wanaripoti kuwa hufai kumbe kwa sababu za kisiasa lakini wanaficha.
 
Ccm zanzibar wanabomoa nchi yao bila kujijua

Kuna kero nyingi za muungano CCM hawana ubavu wa kutetea Zanzibar kutokana na Protocali za kichama, sasa wanafanya makosa yale yale ya kurundikana watu ambao hawana uwezo wa kuisemea Zanzibar ndani ya Serikali. Wanafanya hivyo wakiamini watakuwa salama na siri zao klufichwa kumbe tahamaki nchi inapotea.
 
Kuna kero nyingi za muungano CCM hawana ubavu wa kutetea Zanzibar kutokana na Protocali za kichama, sasa wanafanya makosa yale yale ya kurundikana watu ambao hawana uwezo wa kuisemea Zanzibar ndani ya Serikali. Wanafanya hivyo wakiamini watakuwa salama na siri zao klufichwa kumbe tahamaki nchi inapotea.

Watakuja kushangaa tunaigeuza Zanzibar kuwa mkoa, shauri yao
 
Yaani zanzibar kama ww zi ccm ajira utaiskia redioni tu

Na km ww ni mpemba ndo zaid yaan ni balaa tu nawahurumia sna ndugu zangu ambao mawazo yao ni kuajiriwa na SMZ tu wakat wao ni pure wapemba na wapinzani
 
Ubaguzi uko kwenye damu, acha kusingizia siasa....nafanya shughuli zangu Zanz nayashuhudia yote haya ila tunawaona mapoyoyo tu maana hata wakinibagua hawanipunguzii chochote ....ila kwa kujifanya watu wa dini sasaaaa!!!!!
Kabisa mkuu.

Anahubiri asibaguliwe wakati wao ndio wabaguzi wakubwa.
 
Yaani zanzibar kama ww zi ccm ajira utaiskia redioni tu

Na km ww ni mpemba ndo zaid yaan ni balaa tu nawahurumia sna ndugu zangu ambao mawazo yao ni kuajiriwa na SMZ tu wakat wao ni pure wapemba na wapinzani

Hata hao CCM wanaotokea Pemba hawaajiriwi kisa hawaaminiwi
 
Mada: Ubaguzi wa Ajira ndani ya SMZ
Ubaguzi ubaguzi tu. Ndio nawaambia muanze kujisafisha ili kitu ubaguzi lisiwepo kabisa.

Umeandika tetesi unaamanisha nini?

Na usipotaka kubaguliwa na wewe usiwe mbaguzi.
 
Ubaguzi ubaguzi tu. Ndio nawaambia muanze kujisafisha ili kitu ubaguzi lisiwepo kabisa.

Umeandika tetesi unaamanisha nini?

Na usipotaka kubaguliwa na wewe usiwe mbaguzi.

wewe ndio sarikali ? Mbona unakereketwa sana. Hoja yako ni nini ?
 
Back
Top Bottom