Ubaguzi wa kisiasa anaouonesha Magufuli hadi CCM wenyewe wanamshangaa

Ubaguzi wa kisiasa anaouonesha Magufuli hadi CCM wenyewe wanamshangaa

Tumekua tukisikia kwamba mkuu wa nchi ni mbaguzi hasa linapo kuja swala la mitazamo ya kisiasa kitu ambacho si kuzuri na hakifai kwa mkuu wa nchi.

Tofauti na viongozi wenyine hata marais waliopita, Mh hapa amefeli na inaonyesha anafanya makusidi.

Jana akiwa msoga diwani wa hilo eneo aliitwa atoe kero, Mh akadhani ni diwani toka chama cha chadema kwa sababu hakuvaa sare ya ccm, akaamuru anyang'anywe mic na maneno makali juu lakini baada ya kuuliza chama gani akaambiwa ni wa ccm, mara moja akaamuru arudishiwe mic na aendelee kuongea.

Leo tarehe 29 June 2020 akiwa kilosa akaanza kumponda mbunge wa eneo na kusema wananchi wa eneo hilo wanachagua kwa jazba akiamini mbunge wa eneo hilo ni qa chadema. Anaongeza kwa kusema yeye angekua mbunge wa eneo hilo angekua amemaliza changamoto zote ila kwa sababu wananchi wanachagua kwa jazba na wanachagua wabunge sio ndio maana bado changamoto zipo.

Baadae akauliza mbunge wa hapo anaitwa nani na wa chama gani? Wananchi wakamtaja na kumwambia anatoka chama chamapinduzi.. Bila hata aibu akaanza kumsifia na kuahidi kuzimaliza changamoto hizo akisadiwa na waziri husika.

Wananchi wa Tanzania sio watoto wanajua na wanaelewa vizuri, wao wanapendana bola kujali vyama, dini wala kabila lakini bado kuna viongozi karne hii wanasimamia ubaguzi.

Naamini mh Rais ana nia njema na Tanzania, lakini bado ana nafasi ya kuondoa hurka hii ya ubaguzi hata kama chadema walimpa wakati mgumu 2015.

Rais ndio kiungo pekee cha kuwaunganisha watanzania .

Sio sababu ya yeye kuendelea kubagua vyama vya upinzani hali kazi zake alizo zifanya zinaonekana.

Haya mambo madogodogo yanamuondolea kitu fulani kama kiongozi.

Tuungane kuuoinga ubaguzi.

Prof Jay
Hana nia njema na nchi yetu, acheni kumvisha vilemba vya ukoka
 
Watu nyomi ni jambo nadra nchi hii? Kama watu wanaweza kusimama na kuangalia bulldozer likichimba barabara, tena wakiwa wamejazana, ndio itakuwa kwenye ziara ya rais ambazo kuna vikundi vya burudani kabisa? Hujawahi kuona watu wamejazana wakiangalia show za promotion za bidhaa mbalimbali? Sasa kipi kinakushangaza watu kujazana kwenye hafla zenye burudani, tena huko mikoani?
Acha wivu mwana ufipa
 
kamisani utasikia mimi ni msema kweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu! yaan Mungu huyu ana kazi sana na rais wetu
 
Huyu jamaa msanii sana kama ile ga kilosa yaani anajichekesha bila aibu ukweli usemwe mh Rais anakosea kwa hili kwakweli.
Nikikaa na watu wazima halafu nakuta wanamsifia huyu mzee mwenzao huwa nashindwa kuwaelewa, natamani kuwapa somo ila naamua kimya.
 
Mleta mada huna hoja kabisa, unakalia majungu, mwageni data mmefanya nini tangu 2015?? Mmekosa vitu vya kusema mmebakiza majungu, mnasubiri Jemedari wetu kasema nini ndiyo mnapata vya kuongea,
Mkuu kwa hiyo unataka Chadema nao waoneshe mabarabara na madaraja waliyojenga?
 
Magufuli ni Mbaguzi hadi anakera ....anaweza kufanikiwa kushinda na kupitisha wabunge wake kwa nguvu ..tena "wake" sio wa ccm lakini atakayeingia mwaka 2025 itakuwa ngumu sana kwake ...awe wa chama chochote ..kurudisha umoja wa kitaifa ...huwezi kuwabagua watanzania namna hii , hatukuzoea kabisa ....hii ni laana ..
Na kama amesoma picha wananchi wanaanza kukereka na hii tabia ...
Hata kwa ''afya ya maendeleo'' ya nchi siyo vizuri hata kidogo. Watakaoshinda wengi watakuwa watu incompetent na hawatamsadia hata kidogo katika uongozi. Ila Magufuli anapenda sana kuabudiwa na kutokuwa challenged ndiyo maana anajari kuweka vilaza wenye uwezo wa kuimba sifa zake na kuitikia ndiyo kwa kila jambo. Kama ulivyosema rais atakayefuata baada ya Magufuli atapata shida sana kwani atarithi nchi ya hovyo kabisa.
 
Anayoyafanya chuki na nongwa ya wazi dhidi ya cdm yapo wazi. Sisi ni watu wazima na tunaona mwenendo wake. Kibaya zaidi hiyo chuki yake binafsi, anatumia vibaya madaraka yake kuagiza taasisi za kimamlaka kufanya kwa kadiri ya utashi wake. Na taasisi za kimamlaka kutokana na katiba mbovu, zinatii atakacho ili kutekeleza matakwa kwa ajili vya kulinda vibarua vyao. Mahakama na jeshi la Malawi viligoma kutekeleza utashi wa rais aliyekuwa madarakani, kwani wananitambua.
Magufuli ananikumbusha enzi za rais Moi wa Kenya, kipindi ameshika hatamu sana na anaabudiwa kama mungu mtu. Ila haya yote anayofanya ni mambo ya mtu anayeangalia hapo alipo bila kujua kinachoweza kuja mita moja mbele yake. Anaivuruga nchi kishenzi na madhara yake yatakuja kuwa makubwa tena kwa CCM yenyewe.
 
Kosa la Magufuli ni kufanya hata Yale ambayo watu wangali wakifikiri kuwa Kwa hilii!!! Hatoweza kulifanya

Ikitokea amelifanya, watu wa Aina hiyo, hulazimika humtafutizia makosa ya kulazimisha, ili tu naye angalau aonekane anafanya makosa!

Kwa kuwa naye ni Binadamu! Hawezi kuishi bila kukosea, hiyo ni huluka yetu binadamu, na hata mleta mada naye hukosea!!

Lakini Kwa ujumla wake, Makosa ya Magufuli ni kazi zake na si vinginevyo
Mkuu wewe una muongelea Magufuli baba Jesca au Magufuli rais na mkuu wa nchi? Kama unamuongelea Magufuli rais na mkuu wa nchi ya Tanzania na huoni tatizo kwenye hiyo mikutano miwili aliyofanya basi nakushauri ukapime corona,utakuwa unaumwa
 
Demokrasia ndani ya ccm inawatesa wasio kuwa nayo
Ha ha haaa. Chapisheni fomu mbili za urais. Fanyeni kama mnatania kwa kuita mwenye nia halafu mpaka kesho saa sita iwe mwisho wa kuchukua form muone itakuwaje. Shenzi taip.
 
Attachments

  • IMG-20200628-WA0059.jpg
    IMG-20200628-WA0059.jpg
    27.5 KB · Views: 1
Magufuli ananikumbusha enzi za rais Moi wa Kenya, kipindi ameshika hatamu sana na anaabudiwa kama mungu mtu. Ila haya yote anayofanya ni mambo ya mtu anayeangalia hapo alipo bila kujua kinachoweza kuja mita moja mbele yake. Anaivuruga nchi kishenzi na madhara yake yatakuja kuwa makubwa tena kwa CCM yenyewe.
This bush man is so incompetent and very short sighted.mtu wa hivyo kuliko hovyo yenyewe- Mimi bado naamini corona itakuwa fear kwa Tanzania same way ilivyofanya kwa Burundi
 
he is f****** this country big time. maisha ya watanzania yako modeled na mfumo wa simba na yanga. mashabiki wa hizi timu mbili siku zote hawakubaliani lakini hawadhalilishani wala kutwezana kuvuka mstari, ubishani na majigambo yote yanakoma uwanjani. magufuli must learn from this beautiful culture.
 
Tumekua tukisikia kwamba mkuu wa nchi ni mbaguzi hasa linapo kuja swala la mitazamo ya kisiasa kitu ambacho si kuzuri na hakifai kwa mkuu wa nchi.

Tofauti na viongozi wenyine hata marais waliopita, Mh hapa amefeli na inaonyesha anafanya makusidi.

Jana akiwa msoga diwani wa hilo eneo aliitwa atoe kero, Mh akadhani ni diwani toka chama cha chadema kwa sababu hakuvaa sare ya ccm, akaamuru anyang'anywe mic na maneno makali juu lakini baada ya kuuliza chama gani akaambiwa ni wa ccm, mara moja akaamuru arudishiwe mic na aendelee kuongea.

Leo tarehe 29 June 2020 akiwa kilosa akaanza kumponda mbunge wa eneo na kusema wananchi wa eneo hilo wanachagua kwa jazba akiamini mbunge wa eneo hilo ni qa chadema. Anaongeza kwa kusema yeye angekua mbunge wa eneo hilo angekua amemaliza changamoto zote ila kwa sababu wananchi wanachagua kwa jazba na wanachagua wabunge sio ndio maana bado changamoto zipo.

Baadae akauliza mbunge wa hapo anaitwa nani na wa chama gani? Wananchi wakamtaja na kumwambia anatoka chama chamapinduzi.. Bila hata aibu akaanza kumsifia na kuahidi kuzimaliza changamoto hizo akisadiwa na waziri husika.

Wananchi wa Tanzania sio watoto wanajua na wanaelewa vizuri, wao wanapendana bola kujali vyama, dini wala kabila lakini bado kuna viongozi karne hii wanasimamia ubaguzi.

Naamini mh Rais ana nia njema na Tanzania, lakini bado ana nafasi ya kuondoa hurka hii ya ubaguzi hata kama chadema walimpa wakati mgumu 2015.

Rais ndio kiungo pekee cha kuwaunganisha watanzania .

Sio sababu ya yeye kuendelea kubagua vyama vya upinzani hali kazi zake alizo zifanya zinaonekana.

Haya mambo madogodogo yanamuondolea kitu fulani kama kiongozi.

Tuungane kuuoinga ubaguzi.

Prof Jay

Wewe ni mzandiki, wapi amepokwa maiki?
 
Back
Top Bottom