Ubahili, silaha ya siri wanayoitumia matajiri wengi ambao walikuwa masikini

Haya madini yalikuwa wapi!!!
 
NI KWELI KUPATA PESA SIO SHIDA JEE UNAWEZA KULINDA PESA ? HAPO MTIHANI
 
sasa mwisho wa kuwa tajiri ni nini kama hu spendi hizo hela utatumia kwa ajili ya nini
Mwisho wa utajiri ni usalama, mtoto wako akipata tatizo la moyo kwa mfano, unampeka moja kati ya hospitali bora kabisa India kupata tiba ya moyo.

Utajiri ni kuweza kufanya unachotaka, je wewe ni mshabiki wa soka, vipi ukiwa na kipato cha kutosha cha kukupeleka Qatar mwaka 2022 world Cup kushuhudia hayo mashindano?

Utajiri ni kuhifadhi mali za kutosha na kufika hatua ukiwa bado na nguvu zako na kuamua kustaafu kazi (siongelei kustaafu ajira). Tunataka utajiri kwa sababu kama hizo.

Ubahili ni utamaduni muhimu katika maisha yako. Mfano ukiwa unaingiza milioni 200 kwa mwaka, unaweza sasa kuamua kutumia hata milioni 50 (ni mfano) kwa mwaka na ukawa unauenzi utamaduni wa ubahili na bado maisha yakawa matamu. Mfano ukiwa unaingiza 50 milioni kwa mwaka na ukazitumia zote milioni 50 utakuwa masikini milele
 
hao matajili wanaoenda na vyakula maofisi mwao wanaogopa kuwekewa sumu hamna chochote
Sababu za kiusalama zinaweza zisababishe, lakini vipi kwa hao matajiri wengine wanaokula cafeteria na wafanyakazi wao. Kamprad tajiri wa pili Ulaya mmiliki wa kampuni ya IKEA anakula na wafanyakazi wake cafeteria.

Warren Buffet tajiri wa tatu duniani anaishi nyumba ya vyumba vitano, nyumba hiyo hiyo aliyonunua mwaka 1958 kwa $ 31,500 ndio anaishi mpaka leo. Kumbuka mwaka 1958 alikuwa hajawa hata millionaire, sasa hivi ni billionaire mwenye $ 70 billions

Nina mifano mingi sana mkuu, lakini tuishie hapa. Hoja ya msingi hapa ni kama unataka kufanikiwa kimaisha kwenye eneo la uchumi, lazima u adopt huu utamaduni wa ubahili.
 
Nimesoma
Hii
Imenigusa between 2015 untill this year i have blown money so bad and now imekuwa ngumu to get that pick point again.. i wish nijifunze zaidi about money.. for me i like the good life i use to tell
Myself if i cant live maisha mazuri sasa hela yakazi gani.. the more money napata ndivyo navyoongeza gharama ya maisha yangu... yani this year ndo najuta hasa because i wish i had done better choices and non of the things i have make me happy anymore anyway.. nilikuwa nahisi kuwa navitu vya gharama ni respect ila wala kawaida tuu kwanza i thought itaniketea wateja wamahana in business kujiweka classy ila ndomkwanza people fear that its just gonna be expensive ‍♀️‍♀️‍♀️.. help jamani i wish nipate mtu anifundishe about money.. msiniambie books im too busy.
 
mifano uliyotumia ina mushkeri kidogo kulingana na ulichokiongea ktk uzi labda kama mimi nimekuelewa vibaya
 
Hii ni dhana tuu. Ubahili unaweza kuwa ni sehemu ndogo sana ya sababu zinazochangia mtu kuwa tajiri.

Huwezi kuwa tajiri kwa kuwa mbahili. Huku ni kuwaponza watu.

Matokeo yake ni kutesa watu tuu. Jamaa yangu mmoja aliumwa akalazwa siku mbili tuu, naenda kumbelea akaanza kunipa wasaa nisiwe mbahili. Jamaa alikuwa anaongea kama vile anajutia kurundika hela. Ulikuwa ni woga tuu, mpaka kesho nikimkbusha tunacheka.

Huwezi ushinda umasikini kwa kuwa mbahili, ni majuto ndio huguata baadae.

Utajiri ni illusion guys. Huwezi fundishwa kuwa tajiri ukubwani. Tutakufa kwa madeni, sio kila mwenye hela ni tajiri. Na Ubahili sio utajiri.

.......................
 
NI KWELI USIWE BAHIRI , USITUPE PESA WAKAATI SIO MUHIMU
 
Hebu nitofautishie ubahili na uchoyo
Mwenyewe nimedhani hapo kwenye ubahili angeweka ubinafsi ingewa na mantiki manake mbahili ni mtu ambaye hatumii kipato chake na hivo hata kuwekeza sijui manake sinibahili lakini mbinafsi ndo anaweza kuwekeza kwa sababu chake ni chake na chako ni chake pia yaani hata kama ana bilioni lakini buku yako anaitaka pia!
 
Nimeshakidownload ngoja nianze kukisoma weekend.
 
Mkuu nashukuru kwa kunigusa,huwa nami naambiwa hivyo hivyo namimi nakubali kwel ni mbahili lakini ubahiri wa maendeleo,nakumbuka nilianza na laki 3 ila kwa sasa namiliki vimilion kadhaa si haba,ubahiri huo ndiyo umenisaidia nifike hapa kwa hiyo ubahiri na mimi ni kama maji na Samaki,na siku zote ukitaka mafanikio kuwa bahiri hiyo ndiyo siri na pili usitunze pesa Benk au ndan itafutie kaz ya kufanya,bora ubaki hauna kitu lakini pesa ipo kwenye kaz au inazunguka,na wote waliopata pesa wakazitunza na kuanza kutoa kidogo kidogo waliishia kufirisika,kuna Mtu kutoa hata laki 5 ifanye kaz anaogopa itapotea na hao ndiyo mabingwa wa mipango kabla ya kupata pesa wakipata pesa wanaitelekeza mipango yao.Ubahili ni silaha maishani ila usipite kipimo,kwa mfano Mtu kwa mwezi anaingiza lak 4 lakini ananunua nguo au viatu elfu 50/laki au Mtu anamilik simu ya laki au laki 3 au mbili,mimi huwa najiuliza swali la kawaida tu Mtu anayemiliki simu ya smartphone ya laki moja na mwingine laki 3 huwa kuna utofaut gani? au zinatofautiana kip? cha maana,zingatia-: simpangii Mtu cha kununua au kumilik bali huo ni mtazamo wangu
 
Mkuu Ahsante sana.Mimi kila ninapokaa wananiita bahili ila yangu yananyoka kwa amani kabisa.
 
mifano uliyotumia ina mushkeri kidogo kulingana na ulichokiongea ktk uzi labda kama mimi nimekuelewa vibaya
Mkuu kwenye jambo gani. Kwa mifano ya ulaya/marekani nimelenga kuonesha kwamba hata matajiri wakubwa wanaishi maisha ya chini tofauti na ukubwa wa kipato wanachopata. Na penginevwangeishi maisha extravagant life wasingekuwa hapo walipo.

Na hiyo ninayoongelea ni culture ya kutumia below your means ndio jambo la msingi. Angalia kina bill Gates wanavyovaa.

Kama huamini angalia watumishi/wafanyakazi wanavyovaa, wanavyokula, magari wanayoendesha, matumizi yao bar n.k halafu fananisha na maisha ya wafanya biashara. Kisha angalia maisha ya watumishi uzeeni walio wengi utakuja kugundua, wanaishi magumu kutokana na utamaduni walijiwekea wakati bado wanafanya kazi.

Ubahili unaleta vitu viwili vikubwa. Kwanza unasaidia kulimbikiza mali, pili unaweza kukufanya uishi maisha ya aina yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…