Ubahili, silaha ya siri wanayoitumia matajiri wengi ambao walikuwa masikini

Ubahili, silaha ya siri wanayoitumia matajiri wengi ambao walikuwa masikini

Sasa hv nikipata hela sitatumia nitabaki nayo maisha yangu yote.
 
Tatizo letu WaTz, tunakuwa mabahiri sehemu moja,lakini upande mwingine tunaachia!!!
Mf. Bahiri nyumbani, bar anaajiachia
Au bahiri home, kwa michepuko zinakwishaa.

Ila tukitumia akili ya mtoa mada, tutafanikiwa.
 
Nakuunga mkono mkuu. Huo ni kama utajiri wa kishirikina.Eti usile vizuri,usivae vizuri,usilale pazuri, Usijistareheshe huo sasa si utajiri ni umaskini. Huo utakua umaskini.Tajiri wa kweli anatafuta na akisha ona katengemaa au amejiridhisha ana anza kula matunda ya jasho kidogo kidogo si kiurafi.
 
Ubahili ni kutumia fedha ama mali ndogo kuliko fedha au mali unayoingiza. Ubahili ni kujinyima kwa maana kuna vitu unaweza kuvitamani na uwezo wa kuvinunua unao lakini usinunue.

Ubahili ni kujinyima na kumnyima mtu mwingine ili hiyo fedha uje uitumie kwenye jambo lingine kubwa na bora. Narudia tena UBAHILI NI KUJINYIMA NA KUNYIMA. UCHOYO NI KUNYIMA MTU/WATU WENGINE wakati wewe unatumia bila kujinyima. Watu wengi wanadhani hayo mawili ni jambo moja moja.
post imeongelea point nzuri ila neno ubahili limetumika vibaya ubahili auko hivyo ulivyozungumzia ungetumia kuwa mchumi (frugal). ubahili sio mzuri yani bahili hata vitu vya msingi anunui, anakufa kwa ugonjwa wakati angenunua dawa angepona. yani neno bahili linaharibu maana ya post.
 
Mkuu unataka nikuorodheshee matajiri mabahili na namna wanavyoishi? Wapo wengi sana. Tena matajiri kama hawa Tanzania tunasema ni utajiri wa ndagu.

Kifupi matajiri wengi sana wana discipline kubwa ya matumizi ya rasilimali zao, na kuwa na discipline ndio ubahili, ndio frugality ndio thriftiness. Kama unataka nikuorodheshee matajiri na ubahili wao nitakuorodheshea hata hamsini.

Lakini pia hoja sio Zuckerberg ni bahili ama laa (japo ni bahili bila kujali vitu vinavyomsababisha aishi kibahili). Hoja ni matajiri wengi wanaishi kibahili (kuishi maisha chini ya vipato vyao).

Ndio maana tunaweza muita Bakhresa bahili kama akiwa anatembelea paso, lakini tutamuita karani wa ofisi serikalini mfujaji (sio bahili) akiwa anatembelea hiyo hiyo paso.

Kwahiyo kwa jamaa mwenye utajiri Dola milioni elfu sitini na sita ($66bilion) si ishu kwake kumiliki private jet yenye thamani ya $ 45 million, just a drop of water in the sea.

Pia kikubwa, huyu jamaa maisha mengine anayoishi ni ya kibahili sana (kawaida sana) ukilinganisha na mkwanja anaomiliki. Na mara nyingi haitumii hiyo ndege, anatumia ndege za abiria tu.

Back to the point, huwezi kutoka chini kwa kipato na kuja kuwa na mali nyingi kama si bahili. Pia, huwezi kubaki na mali zako/utajiri kama si bahili (discipline katika matumizi). Tuna mifano mingi hata hapa nchini ya watu waliofulia kwa kushindwa kuwa mabahili.
nini kigezo chako cha kusema fulani ni bahili? mtu anaevaa nguo za kawaida lakini ana ndege binafsi ya bei mbaya huyo ndio bahili? kama ndivyo unamuitaje mtu mwenye utajiri wa $85b lakini anaishi kwenye 'kanyumba' kalekale alikokanunua miaka zaidi ya 60 iliyopita kenye thamani ya $55,000,asiyetumia simu ya mkononi wala kuwa na private jet nk?
boss basi tunatofautiana juu ya uelewa wa maana za maneno 'ubahili' na 'nidhamu ktk matumizi'..
 
Nadhani mkuu unangang'ania mfano mmoja au miwili na kutoka kwenye moyo wa mada.

Maana ya ubahili nimeshaisema mara kadhaa, so haina haja ya kurudia. Zuckerberg na Amancio nimeshawaelezea mara nyingi kwanini ninawaona ni mabahili. Kwani jumia inawaona wao ni mabahili. Hii ni universal, it is not just how I define ubahili, frugality, thrift. It is how the world see them and define then.

Back to the point, unaweza kuchukua mifano mingi sana ambayo inaweza kukusaidia kuelewa hoja yangu ya Mali na Ubahili badala ya kuangalia mifano miwili ambayo kwa maoni yangu inakuchanganya kutokana na tafsiri yako binafsi ya neno ubahili.
 
tuyaache tu boss maana hatutofikia muafaka!
 
NI KWELI, MSINGI MKUBWA NA MUHIMU WA UKWASI NI UBAHILI. WATU WENGI HATUJUI MAANA HALISI YA UBAHILI HATA HUKOSEA TUKAUFANANISHA NA UCHOYO. TUNAKOSEA. UBAHILI NI KUJINYIMA KWA AJILI YA KESHO.
 
Heshima kwenu wakuu wangu

Kama kawaida leo nakuja tena katika jukwaa muhimu kwangu hapa JF.

Hakika kuna mambo mengi sana yanayochangia mpaka mtu kuwa na mali nyingi ama utajiri. Ukiachilia mbali matajiri waliorithi mali, waliopata utajiri kwa bahati kama michezo ya bahati nasibu na wale waliojikusanyia mali kutokana na vipaji vyao kama Sanaa na soka, matajiri wote waliobaki ambao walikuwa masikini na wakawa matajiri wana sifa kubwa ya UBAHILI.

Lakini bila kujali umepata vipi utajiri wako, kama hutakuwa mbahili, hakika utafilisika, hakika hutadumu na mali zako, hakika ipo siku watu watakucheka na kusema umefulia. Kiufupi, matajiri wote unawaona duniani ambao wamedumu kwa muda mrefu ni mabahili. Ni vyema pia ujue kwamba ubahili wa mtu kama Warren Buffet hauwezi ukafanana na ubahili kama wa yule Mkinga wa Kariakoo, wote ni ubahili ila tofauti ni mmoja anafanya ubahili kulingana na matrilioni alionayo na mwingine anafanya ubahili kulingana na mamilioni alionayo.

Naomba pia ieleweke kwamba, ninaposema tajiri natambua kwamba unatofautiana ngazi. Kuna wanaomiliki duka moja kubwa la jumla wakati anaanza maisha alianza kuuza duka la kaka yake, kisha kiosk baadae akamiliki duka kubwa namuita tajiri. Kuna yule ambaye ana estate labda Chicago naye namuita tajiri. Ana hisa timu ya Barcelona, naye ni tajiri.

Nikiri kwamba hii mada imekuja kichwani baada ya mara kwa mara watu, waume kwa wake kupenda kuniita bahili. Ki ukweli huwa nafarijika sana, sababu kwangu bahili ni kinyume cha mfujaji, kwangu bahili ni mtu anayetumia rasilimali zake kwa uangalifu, kwa akili ama mtu anayetumia mali yake baada ya kushirikisha ubongo kuamua na si moyo. Kwangu ubahili ni hatua moja muhimu kwenda kwenye utajiri. Pia ni hatua muhimu sana, kubaki na utajiri.

Ubahili ni kuishi maisha chini ya kipato chako, na si kuishi maisha sawa na kipato chako, au zaidi ya kipato chako. Ubahili ni ku save. Sijawahi kuona mtu aliyeanzia chini kwa kipato na baadae akawa tajiri halafu akose sifa ya ubahili.

Mark Zuckerberg mmiliki wa Facebook, huvaa t-shirt na jinsi, vazi la bei raisi kazini na katika sehemu kubwa ya maisha yake. Amancio Ortega (ana mali zenye thamani ya $ 66 Billions) huwa anakwenda mgahawani kula na wafanyakazi wake chakula cha kawaida sana. Charlie Ergen (anamiliki $14 bilioni) huwa anabeba chakula kutoka nyumbani kila siku kwenda nacho ofisini kwake (kwenye kampuni yake). Warren Buffet kila siku hutengewa na mke wake kati ya $2 na $3 kwa ajili ya chai.

Hii ni kweli hata kwa Tanzania au Africa, tunawafahamu watu wengi waliofuja mali na sasa hivi wamebaki masikini na kituko kwenye jamii zetu hususani wale waliorithi ama kupata mali kwa ghafla. Nawakubali Wachaga wengi, wapare wengi sababu hii silaha huwafikisha mbali sana kimaisha.

Ubahili sio sifa mbaya. Lakini usiwe mbahili kula, ukawa mfujaji kwa mademu, usiwe mbahili kuitunza familia yako, ukawa mfujaji kwenye mitungi. Ishi maisha ya kawaida, kipato unachopata wekeza.

HATA UWE UNAINGIZA HELA NYINGI KIASI GANI, UKIWA MTU WA KUFUJA MALI UTAKUFA MASIKINI. NA HATA UWE UNAINGIZA PESA NDOGO KIASI GANI, UKIWA BAHILI NA KUWEKEZA UTAKUWA TAJIRI ENDAPO MUNGU ATAKUPA UZIMA.
Umetisha mkuu
 
Kuna Mzee Mmoja kijijini kwetu ana vitega uchumi vinavyomuingizia pesa zaidi ya Milioni 50 kwa mwezi lkn ukiingia ndani ya nyumba yake Chakula anachokula cha kawaida sana bora hata Sisi tunakula vizuri.Lakini yeye anakula vyakula vyenye virutubisho kama vile ugali wa Dona,mihogo,mbogamboga za majani kwa wingi na anafanya mazoezi kila siku.nyumba yake ni ya kawaida sana yaani inacost kujenga haizidi Milioni 50 na furniture zake ni za kizamani sana.Lakini kila mwaka anaenda Ulaya na familia Mara Moja kwa mwaka Kula bata na pia kila mwaka huenda India kufanya checkup ya magonjwa mbalimbali.Gari ya huyo mzee ni pickup single board ya Milioni 15
 
Yap watu wa namna hii wapo, na watu kama hawa kuwa masikini labda Mungu mwenyewe aamue
 
Back
Top Bottom