Ubahili, silaha ya siri wanayoitumia matajiri wengi ambao walikuwa masikini

Sasa hv nikipata hela sitatumia nitabaki nayo maisha yangu yote.
 
Tatizo letu WaTz, tunakuwa mabahiri sehemu moja,lakini upande mwingine tunaachia!!!
Mf. Bahiri nyumbani, bar anaajiachia
Au bahiri home, kwa michepuko zinakwishaa.

Ila tukitumia akili ya mtoa mada, tutafanikiwa.
 
Nakuunga mkono mkuu. Huo ni kama utajiri wa kishirikina.Eti usile vizuri,usivae vizuri,usilale pazuri, Usijistareheshe huo sasa si utajiri ni umaskini. Huo utakua umaskini.Tajiri wa kweli anatafuta na akisha ona katengemaa au amejiridhisha ana anza kula matunda ya jasho kidogo kidogo si kiurafi.
 
post imeongelea point nzuri ila neno ubahili limetumika vibaya ubahili auko hivyo ulivyozungumzia ungetumia kuwa mchumi (frugal). ubahili sio mzuri yani bahili hata vitu vya msingi anunui, anakufa kwa ugonjwa wakati angenunua dawa angepona. yani neno bahili linaharibu maana ya post.
 
nini kigezo chako cha kusema fulani ni bahili? mtu anaevaa nguo za kawaida lakini ana ndege binafsi ya bei mbaya huyo ndio bahili? kama ndivyo unamuitaje mtu mwenye utajiri wa $85b lakini anaishi kwenye 'kanyumba' kalekale alikokanunua miaka zaidi ya 60 iliyopita kenye thamani ya $55,000,asiyetumia simu ya mkononi wala kuwa na private jet nk?
boss basi tunatofautiana juu ya uelewa wa maana za maneno 'ubahili' na 'nidhamu ktk matumizi'..
 
Nadhani mkuu unangang'ania mfano mmoja au miwili na kutoka kwenye moyo wa mada.

Maana ya ubahili nimeshaisema mara kadhaa, so haina haja ya kurudia. Zuckerberg na Amancio nimeshawaelezea mara nyingi kwanini ninawaona ni mabahili. Kwani jumia inawaona wao ni mabahili. Hii ni universal, it is not just how I define ubahili, frugality, thrift. It is how the world see them and define then.

Back to the point, unaweza kuchukua mifano mingi sana ambayo inaweza kukusaidia kuelewa hoja yangu ya Mali na Ubahili badala ya kuangalia mifano miwili ambayo kwa maoni yangu inakuchanganya kutokana na tafsiri yako binafsi ya neno ubahili.
 
tuyaache tu boss maana hatutofikia muafaka!
 
NI KWELI, MSINGI MKUBWA NA MUHIMU WA UKWASI NI UBAHILI. WATU WENGI HATUJUI MAANA HALISI YA UBAHILI HATA HUKOSEA TUKAUFANANISHA NA UCHOYO. TUNAKOSEA. UBAHILI NI KUJINYIMA KWA AJILI YA KESHO.
 
UBINAFSI NI UCHOYO AND VICE VERSA. UBAHILI NI KUJIKANA NA KUJINYIMA KWA AJILI YA KESHO.
 
Kuhusu zuckerburg kazidisha.
Tisheti ya hasara hasara na jeans ya kawaida sana
 
Umetisha mkuu
 
Kuna Mzee Mmoja kijijini kwetu ana vitega uchumi vinavyomuingizia pesa zaidi ya Milioni 50 kwa mwezi lkn ukiingia ndani ya nyumba yake Chakula anachokula cha kawaida sana bora hata Sisi tunakula vizuri.Lakini yeye anakula vyakula vyenye virutubisho kama vile ugali wa Dona,mihogo,mbogamboga za majani kwa wingi na anafanya mazoezi kila siku.nyumba yake ni ya kawaida sana yaani inacost kujenga haizidi Milioni 50 na furniture zake ni za kizamani sana.Lakini kila mwaka anaenda Ulaya na familia Mara Moja kwa mwaka Kula bata na pia kila mwaka huenda India kufanya checkup ya magonjwa mbalimbali.Gari ya huyo mzee ni pickup single board ya Milioni 15
 
Yap watu wa namna hii wapo, na watu kama hawa kuwa masikini labda Mungu mwenyewe aamue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…