Ubalozi wa Canada: Tunafatilia kwa karibu kesi ya Freeman Mbowe, wasema demokrasia inahitaji uhuru wa kutoa maoni na mikusanyiko

Ubalozi wa Canada: Tunafatilia kwa karibu kesi ya Freeman Mbowe, wasema demokrasia inahitaji uhuru wa kutoa maoni na mikusanyiko

Mbowe kama alithibitika anastahili kukamatwa kwa ugaidi ni bora wangemkamatia msibani kule machame na si kwenye tukio la kudai katiba kule Mwanza, serikali mmetuangusha kimataifa na sasa serikali itaumia kiuchumi wa kimataifa na wananchi ndio watakaosaga meno kama enzi si nyingi.
CCM salama yao wakubaliane na Wapinzani lini tunaanza kuandika Katiba ya Wananchi(Haraka) kabla hawajajipeleka Mahakama ya Wananchi.
 
Nchi inaenda kubaya huku tozo za Mpesa mara mafuta yapo juu ukijisahau unasikia mbowe gaidi Nchi ngumu sana hii washazoea kusingizia kesi kila kukicha...
 
Nawashauri CCM hii kesi waachane nayo...inawaaibisha...watafute njia nyingine bora zaidi ya kumdhibiti Mh. Mbowe na mikutano yake ya kidai katiba mpya.
Na vipi kuhusu kesi ya Ole Sabaya. Nayo Serikali iachane nayo?
 
Mambo yamekorogeka Mama anatamani asafiri nje ya nchi mwezi mzima ila hapati mialiko nchi zinazojielewa
 
Ghafula paa nchi mikononi kwa Mabeyo kwa mwaka mmoja.
Ghafula paa uchaguzi na Mbowe mgombea urais.
Ghafula paa wasimamizi wa uchaguzi ni JWTZ.
Ghafula paa MBOWE mshindi
Itakuwaje? CCM tutaanza kutoa siri?
Nani atakubali kuwa Mkiti taifa CCM
Hahahaha kwa kweli chadema mna ndoto za kusikitisha
 
Leteni pesa zenu twala...... mengine mtabaki kua wapenzi watazamaji tu.......hadi hili koloni la bibi kizee linataka kubweka
 
Ghafula paa nchi mikononi kwa Mabeyo kwa mwaka mmoja.
Ghafula paa uchaguzi na Mbowe mgombea urais.
Ghafula paa wasimamizi wa uchaguzi ni JWTZ.
Ghafula paa MBOWE mshindi
Itakuwaje? CCM tutaanza kutoa siri?
Nani atakubali kuwa Mkiti taifa CCM
Naomba namba ya pusha wako
 
Kweli dunia imedalika. Enzi ya Nyerere, huyo balozi angeitwa ikulu ajieleze kwa nini anaingilia mambo ya ndani ya nchi yetu. Dunia ya enzi ya Nyerere ilikuwa ni multi-polar yaani nchi za magharibi zikikuzinguwa unaenda kuomba msaada kwa nchi za mashariki zikiongozwa na USSR maisha yanaendelea. Baada ya cold war kuisha na USSR kusambaratika, dunia imebaki uni-polar ni nchi za magharibi zikiongozwa na America ndiyo zinaongoza. Mabalozi wao au viongozi wakikoroma, serikali inanywea.
 
Mbowe kama alithibitika anastahili kukamatwa kwa ugaidi ni bora wangemkamatia msibani kule machame na si kwenye tukio la kudai katiba kule Mwanza, serikali mmetuangusha kimataifa na sasa serikali itaumia kiuchumi wa kimataifa na wananchi ndio watakaosaga meno kama enzi si nyingi.
Serikali imezingua kuanzia kwenye matozo na hii Kanata kamata mama kakufungulia CV yake aisee
 
CCM mpya ya kutotumia miguvu na mibavu, isiyo taka kodi za dhuluma. Ila mafisadi wakifisidi sio dhuluma ni halali bin haki.

CCM inayoenda na dunia inavyoenda kujasiria corona. Kiko wapi? Mmenyanyua mikono kwenye corona, lakini mtabanwa kuhusu uhuru holela holela na hivi wanawasubiria mmalizane nao kwenye hii mikataba ya biashara ya chanjo. Ndio mtajua Mzungu hana urafiki wa kudumu na kuaminika. Ataanza kuwa wekea kibano cha uhuru wa kujieleza, kukusanyika na makongamano yasiyo na utaratibu.

CCM shaurianeni muanzishe mchakato wa Katiba mpya. Hiko kichaka mnachojifichia cha haikuwa agenda ya ilani yenu na kujenga uchumi kwanza hakvta wasaidia kamwe.

Ni bora mkaanzisha mchakato wa katiba mpya mtakao usimamia na kuuendesha kuliko mkaacha mpaka kufikia kulazimishwa na mchakato ukafanyika mkiwa mmelazimishiwa na hamna jinsi ya kuudhibiti mchakato huo.
 
Hapana Samia rais kabla ya kuwa mwenyekiti wa CCM na Samia rais na mwenyekiti wa CCM ni watu wawili tofauti.
Mie bado najiuliza ....hivi serikali ya Tz na polisi wanavyowatendea ukatili wapinzani, je sijui ingetokea nini kama ingekuwa kama tukio la kule Kenya wakati Oginga wa upinzani baada ya uchaguzi, alipokwenda na kuapishwa Uhuru Park,na polisi wa Kenya kuonyesha walivyopevuka kidemokrasia, walimuacha tu na hakuna ghasia, fujo zilizotokea,wala hali ya uvunjifu wa amani iliyotokea kutokana hatua za busara zilizochukuliwa na polisi ....mwisho wake maisha yakaendelea safi na Kenyatta hadi leo ni Rais wa Kenya...........aiseeee Tz safari bado ni ndefu.
 
Wapenda amani kote nchini na wazalendo wa nchi popote pale walipo kamwe tusikubali hawa wahuni wachache wanao jifanya wanadai haki kwa kuvunja sheria watuharibie Amani ya nchi yetu.
tuchukue hatua za kuwafichua na kuwa ripoti popote pale walipo.
sio wafuasi wote wa chadema wanafurahia uhuni huu bali wapo wahuni wachache wenye chembe chembe za Ugaidi/uhalifu/ujanbazi/wizi ndio wanafanya vitendo hivi vya kihuni ili wapate sababu.
 
Back
Top Bottom