KWELI Ubalozi wa China wakanusha kufungua vituo vya Polisi Afrika ikiwemo Tanzania

KWELI Ubalozi wa China wakanusha kufungua vituo vya Polisi Afrika ikiwemo Tanzania

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Madai
Shirika la utangazaji la BBC liliripoti kuwa nchi ya China ina mpango wa kufungua vituo vya polisi nchini Nigeria, Lesotho na Tanzania ili kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na raia wake wanaoishi katika nchi hizo tatu za Afrika, tovuti inayomilikiwa na mtu binafsi ya Nigeria ya Vanguard imeripoti. Wakiwanukuu watetezi wa Usalama, Vanguard amesema mpangilio wa China unaweza kuonekana kama shambulio dhidi ya uhuru wa eneo husika.

Aidha inaelezwa kuwa, [China] imeamua… kushirikiana na United Front linked, mashirika ambayo yako nje ya nchi katika mabara matano, kuanzisha mfumo mbadala wa polisi na mahakama ndani ya nchi tatu, na kuhusisha moja kwa moja mashirika hayo katika mbinu zisizo halali zinazotumiwa kuwasaka 'wakimbizi',

1666671474091.png

Picha: Sehemu ya Tweet ikionesha habari iliyotolewa na BBC kuhusu China


1666671786044.png

Picha: Sehemu ya tweet iliyojibiwa na Ubalozi wa China kwenye ukurasa wa BBC
 
Tunachokijua
Ubalozi wa China umeibuka na kupinga vikali habari hii kwa kuwajibu BBC
Balozi wa Tanzania nchini China Mberwa Kairuki amekanusha taarifa zilizochapishwa na baadhi vya Vyombo vya Habari kwamba China inadaiwa kutaka kufungua Vituo vya Polisi nchini Tanzania “Taarifa hizi hazina ukweli wowote zipuuzwe”.

Ubalozi wa China nchini Tanzania umeikituhumu chombo cha habari cha Uingereza(BBC) kwa kutunga habari. Ubalozi huo umesema habari ya China kufungua vituo vya polisi Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania ni uthibitisho unaoonesha jinsi BBC inavyosambaza taarifa zisizo za kweli kuhusu China ili kuvunja uhusiano wa China a Afrika.

1666671786044-png.2397044

Picha: Sehemu ya tweet iliyojibiwa na Ubalozi wa China kwenye ukurasa wa BBC

Ubalozi umesisitiza China na Tanzania wanafurahia urafiki wa muda mrefu kwenye nyanja zote ambao hauwezi kutikiswa na tetesi au kuharibu taswira kwa taarifa za uongo.

Hata hivyo ubalozi huo haukueleza ukweli ni upi katika taarifa hiyo

Polisi watoa tamko
Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, naye alizungumzia suala hilo huku naye akionekana kujibu swali kwa swali:

"Waulizwe wao BBC kuwa hizo taarifa wamezipata wapi, zina ukweli gani? Na je matukio ya kihalifu yakitokea huwa nani anaulizwa?

"Kabla mimi sijaongea, wao BBC ndio wangeanza kutoa ufafanuzi wa taarifa yao walipoitoa? Wewe ulishaona wapi nchi nyingine inafungua kituo cha Polisi katika nchi nyingine?"
Back
Top Bottom