Ubalozi wa India wawatahadharisha raia wake dhidi ya ajira za MeTL

Nilichogundua kuna mtu alushawahi kusema, "kuna idadi ya miaka ukiifikisha ukiwa unafanya kazi kwa muhindi hutaweza kuacha" huu usemi nahisi una umweli maana kuna wazee wapo tangu 1992 lakini mpaka leo wanapanda dala dala na mshahara hauzidi 700k
Ama nasema uwongo ndugu zangu. This is the matter of fact. Lazima niongee ukweli......
 
Mkuu hongera sana tafadhali andika makala kabisaaa kuhusu hili, Watanzania ni wavivu asikwambie MTU. Tunapenda mteremko, binafsi niliwahi kufanya kazi Kwa wahindi sababu ya kuona kazi ngumu nikawa nafanya pole pole. Muhindi mmoja anaitwa Ridhwan akaniambia si ulitaka kazi hii ndio kazi tangu siku hiyo Nikabadilika.
 
Masuala ya ajira kwa Nchi zetu hizi yana manyanyaso sana... Unaeomba kazi unaonekana kama punguani flani usiekua na thamani.. Bado ukipata kazi hiyo ukakutana na Boss mpuuzi unakaa kwenye shida kuu na mateso.

Sheria za Labour ni kama hazipo na wala hazifanyi kazi.. Vyama vya wafanyakazi Tanzania vikishajifia kitambo ni zero plus.. Ndio mana muajiri ana nguvu sana.

Hawa akina Metl wakienda Kenya hapo tu watapigwa kesi wazimie mchana kweupe coz Kenya mahakama zinajitambua..na Ndio mana hawawezi kuthubutu kufungua Biashara Ulaya wanajua Labour Laws zipo na zinang'ata kweli.

Wahindi wanaoletwa Tanzania ni kwasababu sisi wenyewe Watz hatuna miiko ya Kazi unakuta mtu ni mhasibu anaenda Bar anaanza kutaja mikopo ya kampuni anayofanyia kazi...Ujinga.

Ila wahindi wanatunza siri za kazi au kampuni zao na ukichanganya na akili zetu wabongo tunaoheshimu nyapara Mhindi kuliko mbongo basi ndio mana wanaletwa hao.
 
Mbongo anaweza akakufanyia kazi zako kwa maneno yake ya mdomoni.......usipomkagua na ukamlipa ndio imekula kwako hiyo.

Wabongo maneno mengiii.... utendaji zeroo tena hawa wasomi ndio zero kabisa
 


✔✔✔✔✔✔10000% true.
 
Kama MO mnyonyaji nendeni kwengineko ambako hamnyonywi. Mbona ni simple Logic tu.

Hata EPZ pale kuna kiwanda cha majinzi kazi zipo.
Watanzania wengi wanapenda ugawane nao, kama bidhaa inauzwa 500 basi yeye achukue 200
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…