Ubalozi wa Marekani nchini Iraq wachomwa moto, inasikitisha

Ubalozi wa Marekani nchini Iraq wachomwa moto, inasikitisha

Kaka USA kuvamia Iraq, au kutetea Kuwait, kusaidia Libya, kuingilia maugomvu Syria, Kumchukia Iran na Venezuela, yana jibu moja tu, OIL, basi..

Kabla ya vita ya Iraq na Iran nilikuwa huko na nimeishi miaka mingi mpaka uvamizi ulipoanza wa Saddam huko Kuwait
Kweli tatizo lote ni wizi wa mafuta lakini tambua ya kuwa Saddam alikuwa rafiki mkubwa wa USA hata viatu Saddam na G.W.Bush walikuwa wanashonewa kiwanda kimoja na mtengenezaji mashuhuri Andrea Artioli wa Italy

Iraq ilikuwa Iraq Kweli wakati huo na kila kitu walitengeneza wao kuanzia barabara mpaka madawa
Nimekaa Baghdad na Basra pia pamoja na miji mingine ila jamaa alikuwa mbabe haswa aliweka sanamu zake kila sehemu tena kubwa.
Ukiiona tu utafikiri yuko mbele yako
Washenzi wenye tamaa wakamezea mate mafuta yao na kuwachonganisha na Iran na baadae kumvamia baada ya kutaka haki yake aliyoibiwa na ndugu zake majirani hapo Middle East
Yaliyokuja baadae ikawa historia na mimi nikakimbilia Havana

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mbinu za kimarekani kama hujui.. mmarekani anajianda kuondoka Iraq
 
Ubalozi wa Marekani nchini Iraq nchi ambayo Marekani imekuwepo kijeshi kwa muda mrefu tangu walipompindua Saddam Hussein umechomwa moto na waandamanaji wenye mrengo wa kuiunga mkono Iran. Hii inafuatia hapo juzi kushambuliwa kwa kambi za wanamgambo huo na kuuliwa wapiganaji wasiopungua 25.

Katika mashambulizi hayo ya juzi Marekani ilijigamba kushambulia Iraq na Syria kwa wapiganaji wenye kuiunga Iran. Hii ilitokana na shambulizi siku mbili kabla lililomuuwa mkandarasi wa kimarekani nchini humo.
HAUJACHOMWA, IT WAS ONLY STORMED!
 
Inasikitisha kwanini ?.Huyu jamaa aliyeingia Iraq kwa ubabe wa kutisha sasa hatakiwi na hata vibaraka aliowaweka na watu mitaani ndio kama hao wanatamani wasione hata ubalozi wake.Uwongo wa Marekani umekuwa hadharani kwa kila mtu.
 
Tutaendelea kaa mkileta fyokofyoko tutasababisha muuane milele

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo hali haipo tena kwa Marekani,Kumbuka matamko ya Trump kila kukicha anataka kuondoa majeshi yake kila eneo.Watu wasioelewa vyema jinsi taifa lao linavyodidimia kiuchumi na kiheshima ndio wanaomshinikiza Trump aendelee kuweka majeshi nchi walizozivamia.
Mwishowe hata rafiki yake mkubwa Korea kusini amemtaka alipe pesa tele ili jeshi la Marekani liendelee kubaki.Kule Saudia kila siku anawadai dola ili aendelee kuwalinda.
 
Unaweza ukajipa moyo hivyo lakini moto umechomwa kwenye eneo la ubalozi ingawaje haukuunguza kama kule Tripoli nchini Libya..
Huu uzi umenikumbusha issue ya Libya na movie yake 13 Hrs:Secret Soldiers of Benghazi
Hii sijui itakua na title gani

marehemu may they RIP
 
Marekani ni wabishi Sana yaani raia wameandamana hawataki uwepo kwenye nchi yao wanachoma ubalozi lakini bado tu anakaza ubongo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom