Ubalozi wa Marekani nchini wasikitishwa na Uminyaji demokrasia na ukamataji wa Viongozi wa Upinzani nchini

Ubalozi wa Marekani nchini wasikitishwa na Uminyaji demokrasia na ukamataji wa Viongozi wa Upinzani nchini

Katika tamko lao Ubalozi wa Marekani umesema umesikitishwa na hatua za hivi karibuni za Serikali ya Tanzania za kuminya demokrasia

Uminyaji wa demokrasia wametaja kuhusu kukamatwa kwa viongozi wa vyama vya upinzani wakiwa katika mikutano ya ndani. Wahanga wa ukamatwaji ni viongozi 8 wa ACT-Wazalendo japo hawajawataja kwenye tamko lao

Pia ubalozi umesikitishwa na tukio la kuwafutia leseni gazeti la chama siasa cha upinzani. Wamesema hatua hizi ni mwendelezo wa mlolongo wa matukio ya kusikitisha ya vitisho kwa wanachama wa vyama vya upinzani, asasi za kiraia na vymbo vya habari

Ubalozi wa marekani unafahari kusaidia na kuunga mkono uhuru wa kujieleza na ushiriki jumuishi wa kisiasa kwa namna zote kwa kuwa mambo haya yamejumuishwa na Katiba ya Tanzania na tamko la kimataifa la Haki za Binadamu


1593069402420.png
 
Kuna watu wana kibri kama wataishi milele,kumbuka kwa haya yote unayowafanyiya wenzako ipo siku utaachia madaraka, au utakufa.sijui kama kungekuwa kunakuishi milele ukatili wa binadamu ungepindukia kiasi gani
 
Kaimu balozi na Balozi hawapo ili tamko la kichochezi limetolewa na nani?
Kama Balozi na Kaimu hawapo haina maana Ubalozi umefungwa mpaka warudi. Ofisi ya Serikali haitembei na mfanyakazi yeyote wa ofisi hiyo hata asiporudi kabisa shughuli zote zitaendelea kama kawaida. Wajinga wengi, pamoja na wewe, wanafikiri Tanzania ni mfano mzuri wa kuigwa katika kuendesha mambo ambapo mtu mmoja anaamua kila kitu na asipokuwapo basi hakuna chochote kinachofanyika mpaka arudi. Balozi za wenzetu hazitekelezi kazi zao kwa kutegemea mkuu ameamkaje kila siku, wait hata asipoamka mambo yao yataenda Kama kawaidà. Wafanyakazi wote was Ubalozi wowote ni wakazi wa nchi ilipo ofisi yao na mengi yanayotokea kwenye nchi walipo yanawagusa kwa namna moja au nyingine. Kukiwa hakuna mafuta au sukari nao wanaadhirika.
 
Wakaanzie kwao kwanza maana Wananchi wao wanapigwa risasi mtaani km wanyama
Ni lzm wasikitishwe sababu wanao uzoefu wa hayo.Maana wao ndio uingia gharama kubwa za kuhudumia wakimbizi na sio sisi Kama waafrika.Nchi za kiafrica ziwezacho ni kuzalisha wakimbizi duniani na sio kuhudumia wakimbizi.
Pia sisi ni global village ni sehemu ya dunia.
Jumuia za kimataifa zipewe meno za kuwaeliminate watawala wote duniani wenye viashiria vya uvunjifu wa amani sababu ya malezi mabovu utotoni,hii itaeupusha jumuiya za kimataifa kuingia gharama kubwa za kusawazisha Mambo pakichafuka.
 
Hiyo inaitwa the balance of terror. Ukiwa na maguvu Sana wewe mwenyewe Ni mbaya. Kuna wakati anatakiwa awepo kilanja ambaye ataleta kabalance.
 
Wapambane na iran kwanza hao makuwaidi wa ubeberu

Tanzania tuna marafiki wazuri km China na Russia hao USA hatuna muda nao

Russia na China za kijamaa ndio zilikuwa marafiki zikiwpatia financial and technical support!! Sasa hivi watu hao hawana msaada wowote isipokuwa wa kuwatawala kimawazo. Ukitafuta hao “wahisani wa maendeleo” Russia anaweza kuwa hayupo au yuko chini kabisa. Angalia UK, US na EU katika list hiyo ndio utajua umepandikizwa chuki dhidi ya watu wanaofanya angalau jambo la maana - kuchangia bajeti ya nchi yako!!

China na Russia ulizozitolea mfano ndio viongozi wa ukandamizi wa demokrasia. Hivi kweli hata akili kiduchu ya kutambua haya huna pia?? Unajua kuvuka barabara tu??
 
Bado tu hawajaacha tabia ya matamko ya kijinga jinga kila siku, wanahangaika sana na hii nchi waseme tu ukweli nini wanachokitaka na si kutufanya wajinga eti wanauchungu na Tanzania.
Wanawataka ninyi majike ya mbuzi
 
Huyu jiwe ati anajipima misuli na Marekani, ataondoka bila kuaga!! 2021 naiona kwa mbali Serikali ya Umoja wa kitaifa inanukia.
 
nayahesabu matamko yashafika 5 tayari... haya yanatosha kabisa kutuanzishia safari za Ze Hegi.
 
Ya corona yameshimda wamegeukia ya demokrasia wanapata taabu sana.
 
Ila kweli.
Polisi wanakosea sanaa.
Kuna mambo wanayafanya hayana umuhimu.
kama kuna kiongozi anawatuma wafanye hayo ajue sio sahihi..
Watu mmewakaba kila sehemu lakini bado mnawaogopa HAMJIAMINI?
 
Back
Top Bottom