Ubalozi wa Marekani nchini wasikitishwa na Uminyaji demokrasia na ukamataji wa Viongozi wa Upinzani nchini

Ubalozi wa Marekani nchini wasikitishwa na Uminyaji demokrasia na ukamataji wa Viongozi wa Upinzani nchini

Itategemea mmeamkaje siku hiyo.
JK Nyerere alisema, kila mtu anataka awe na hakika ya Kesho yake, haiwezekani mtu akashauriwa na mkewe huko halafu...., Tueshimu sheria, tuache demokrasia isitawi, pia tueshimiane na kuvumiliana, mwisho tusioneane na kudhalilishana, tukitekeleza hayo amani na umoja utaimarika zaidi na kudumu!
 
Inabidi tuwaige mambo yanapokwenda mrama kwao wakipiga risasi Raia na sisi tunatoaa ka tamko wakileta nyoko tunahesabiana matamko
Watu wao wakipewa haki ya kuandamana dhidi ya baya lolote, na sisi tutawapa haki ya watu kuandamana hapa kwetu dhidi ya maovu?

Vyama vyao vikipewa haki ya kufanya siasa bila bugdha, na sisi tutafanya hivyo hivyo kwa vyama vyetu vya siasa?

Wao wakiwa hawahangaiki na viongozi wa kisiasa, hawawatengenezei kesi fake, hawawafungi, hawawanyanyasi, wala hawawashambulii au kuwapoteza wanaomkosoa Rais wao, na sisi tutafanya hivyo hivyo?

Wao wakifanya uchunguzi juu ya wanaopotezwa, nasi tutafanya hivyo hivyo kuhusiana na kupotea kwa akina Ben Saanane, Gwanda, na wengineo?

Tusiwe wapumbavu, tuna mengi ya kijinga, we live in primitivity, tushukuru pale kunapotokea watu wanaotukumbusha kuhusu umuhimu wa maisha ya ustaraabu na utu.

Kuishi kwenye ufungwa wa mawazo, kunapumbuza akili. Angalia mataifa kama China, pamoja na uwingi wa watu kuzidi Taifa lolote, hakuna wanachogundua zaidi ya kuiga. Wataalam wa Sayansi ya ugunduzi wanatuambia huwezi kuwa mgunduzi kama akili yako imefungwa kwenye utumwa wa akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JK Nyerere alisema, kila mtu anataka awe na hakika ya Kesho yake, haiwezekani mtu akashauriwa na mkewe huko halafu...., Tueshimu sheria, tuache demokrasia isitawi, pia tueshimiane na kuvumiliana, mwisho tusioneane na kudhalilishana, tukitekeleza hayo amani na umoja utaimarika zaidi na kudumu!
Super wise words mkuu,ni kama vile Nyerere aliona yajayo yatakavyokua.
 
Hayo ni maoni yao kwa sababu wana uwakilishi wa kibalozi hapa, na wamekuwa ni wadau wakubwa wa maendeleo, wanapotoa tathmini yao tusiwabeze na kuwaita mabeberu wakati misaada yao tunapokea..
 
Ni lzm wasikitishwe sababu wanao uzoefu wa hayo.Maana wao ndio uingia gharama kubwa za kuhudumia wakimbizi na sio sisi Kama waafrika.Nchi za kiafrica ziwezacho ni kuzalisha wakimbizi duniani na sio kuhudumia wakimbizi.
Pia sisi ni global village ni sehemu ya dunia.
Jumuia za kimataifa zipewe meno za kuwaeliminate watawala wote duniani wenye viashiria vya uvunjifu wa amani sababu ya malezi mabovu utotoni,hii itaeupusha jumuiya za kimataifa kuingia gharama kubwa za kusawazisha Mambo pakichafuka.
Hadi Leo hujui anayezalisha wakimbizi duniani hasa Afrika?
 
They can go get some beers
Kama watu wana uhuru but they cannot breathe in their own country what does it mean?
giphy.gif
 
Ni lzm wasikitishwe sababu wanao uzoefu wa hayo.Maana wao ndio uingia gharama kubwa za kuhudumia wakimbizi na sio sisi Kama waafrika.Nchi za kiafrica ziwezacho ni kuzalisha wakimbizi duniani na sio kuhudumia wakimbizi.
Pia sisi ni global village ni sehemu ya dunia.
Jumuia za kimataifa zipewe meno za kuwaeliminate watawala wote duniani wenye viashiria vya uvunjifu wa amani sababu ya malezi mabovu utotoni,hii itaeupusha jumuiya za kimataifa kuingia gharama kubwa za kusawazisha Mambo pakichafuka.
Correct
 
Back
Top Bottom