Tangu lini uchaguzi serikali za mitaa ukawa na wasimamizi wa kimataifa?
hao waingereza si ndio hao hao ambao waziri mkuu wao Borris johnson alilisimamisha bunge kinyemela ili kulinyima uwezo wa kupiga kura dhidi yake juu ya BREXIT ya EU?
Hawa wamarekani si ndio wako kwenye mchakato wa kupiga kura ya IMPEACHMENT dhidi ya Rais Donald trump?
kisa kuifanya kampeni chafu dhidi ya mmojawapo wa wanafamilia ya mgombea urais wa Democrats senator Joe biden?
huyo trump mwenyewe kuukalia urais ni baada ya kufanya udukuzi dhidi ya mgombea mwenza mama Hilary clinton?
akisaidiwa na urusi ya putin?
Hawa waingereza na wamarekani si ndio hao walioshirikiana kuiharibu amani ya mashariki ya kati hadi afrika huko libya na syria hadi Yemen?
na leo tunashuhudia desperate journeys,waafrika wenzetu wakiangamia baharini,kukimbia machafuko huko kaskazini mwa afrika.
*NA MBAYA ZAIDI NCHI ZOTE MBILI ZIMEFUNGA MIPAKA YAO DHIDI YA WAKIMBIZI*
Na sasa wanachota mafuta bure huku wakiendeleza choko choko huko Iran?
Damu za watu wasio na hatia zimewajaa mikononi,na cha kuudhi ni kwamba wao hawajasaini mkataba wa ICC.
Huku mabwege fulani humu wakiwaona kama wakombozi wao.
Hawa ndio walimuua mpigania haki na uhuru kamili wa muafrika,Patrice lumumba( R.I.P).
tena kwa kumtumbukiza kwenye pipa la acid ili ayeyuke kabisa.
Ni hapo marekani ndio kuna ubaguzi mkubwa wa haki za binadamu na mauaji ya kibaguzi mitaani tena yakifanywa na police wa serikali ya marekani.
TUWE TUNAWEKA AKILI ZETU SAWA,NA TUACHE KUWEKA MATUMBO YETU NA TAMAA BINAFSI MBELE.
TUJITAMBUWE KAMA WAAFRIKA NA HAKUNA SIKU MZUNGU ALIMPENDA MUAFRIKA.
Viva Tanzania, viva JPM [emoji1241][emoji818]