Ubalozi wa Marekani: Tumesikitishwa na ukiukwaji uliojitokeza kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania

Ubalozi wa Marekani: Tumesikitishwa na ukiukwaji uliojitokeza kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania

Hata sisi tunasikitishwa na wamarekani wanavyoinyonya Africa, ngoma droo wawe wapole tuu
 
Kwa Akili za Mwenyekiti Wao, hachelewi Kuropoka Kuwa Hauwahusu. Atambue Muda wowote tunaweza wekewa Vikwazo ndipo ataelewa wanahusika au lah!
Mara nyingi watu vichwa maji huwa hawaambiliki hadi wazabwe vibao. Viongozi wa Tanzania wamekuwa ni vichwa maji balaa, kiburi kimewajaa hadi kwenye masaburi; hata sielewi wanategemea nini!!!?
 
Mara nyingi watu vichwa maji huwa hawaambiliki hadi wazabwe vibao. Viongozi wa Tanzania wamekuwa ni vichwa maji balaa, kiburi kimewajaa hadi kwenye masaburi; hata sielewi wanategemea nini!!!?
Lakini itamgharimu yeye na Taifa kiujumla. Japo upande mwingine ndiyo utakuwa mwanzo wa Kuheshimu maamzi ya sheria na kwenda Tanzania mpya ya Watanzania na si ya CCM.
 
Mkuu, nakuelewa sana unapo ongelea demokrasia. Nami pia sifurahishwi na baadhi ya mambo yanayo endelea kisiasa nchini kwetu.

Lakini hebu nikumbushe ni nchigani ambayo hao wazungu waliingiliakati na kuwaondoa ama kuwauwa viongozi wanaowatuhumu kuwa wanadhulumu haki za raiya wao alafu nchihiyo ikapata amani ya kudumu na maendeleo.

Some times things a very complicated in this world.
Tuwe makini.

Kuhitaji maendeleo sio kigezo cha kufanyiwa hujuma. Si vibaya tukaenda kwenye angle wanayotupeleka watawala.
 
Trump mwenyewe tuna mashaka na ushindi wake. Waanze naye huyo kwanza.🚶🚶🏃🏃
 
Yasije tukuta ya zimbwabwe unaenda na Milioni kununua mkate
 
Ivi ubalozi wa Tanzania huko Marekani huwa pia wanatabia
Ya Kucomment juu ya utawala
Wa Trump?
 
Tangu lini uchaguzi serikali za mitaa ukawa na wasimamizi wa kimataifa?

hao waingereza si ndio hao hao ambao waziri mkuu wao Borris johnson alilisimamisha bunge kinyemela ili kulinyima uwezo wa kupiga kura dhidi yake juu ya BREXIT ya EU?

Hawa wamarekani si ndio wako kwenye mchakato wa kupiga kura ya IMPEACHMENT dhidi ya Rais Donald trump?

kisa kuifanya kampeni chafu dhidi ya mmojawapo wa wanafamilia ya mgombea urais wa Democrats senator Joe biden?

huyo trump mwenyewe kuukalia urais ni baada ya kufanya udukuzi dhidi ya mgombea mwenza mama Hilary clinton?
akisaidiwa na urusi ya putin?

Hawa waingereza na wamarekani si ndio hao walioshirikiana kuiharibu amani ya mashariki ya kati hadi afrika huko libya na syria hadi Yemen?

na leo tunashuhudia desperate journeys,waafrika wenzetu wakiangamia baharini,kukimbia machafuko huko kaskazini mwa afrika.

*NA MBAYA ZAIDI NCHI ZOTE MBILI ZIMEFUNGA MIPAKA YAO DHIDI YA WAKIMBIZI*

Na sasa wanachota mafuta bure huku wakiendeleza choko choko huko Iran?

Damu za watu wasio na hatia zimewajaa mikononi,na cha kuudhi ni kwamba wao hawajasaini mkataba wa ICC.

Huku mabwege fulani humu wakiwaona kama wakombozi wao.

Hawa ndio walimuua mpigania haki na uhuru kamili wa muafrika,Patrice lumumba( R.I.P).
tena kwa kumtumbukiza kwenye pipa la acid ili ayeyuke kabisa.

Ni hapo marekani ndio kuna ubaguzi mkubwa wa haki za binadamu na mauaji ya kibaguzi mitaani tena yakifanywa na police wa serikali ya marekani.

TUWE TUNAWEKA AKILI ZETU SAWA,NA TUACHE KUWEKA MATUMBO YETU NA TAMAA BINAFSI MBELE.

TUJITAMBUWE KAMA WAAFRIKA NA HAKUNA SIKU MZUNGU ALIMPENDA MUAFRIKA.

Viva Tanzania, viva JPM [emoji1241][emoji818]
 
Back
Top Bottom