Ubalozi wa Marekani wahoji utata wa kifo cha kijana wa Ki-Tanzania nchini Urusi

Ubalozi wa Marekani wahoji utata wa kifo cha kijana wa Ki-Tanzania nchini Urusi

Wanataka kutuma Rambirambi ?

Huenda wasingesaidia kwa kuchochea na kutuma silaha huko huyu jamaa asingefariki.....
 
Kuna tofauti ya kuwa mwanajeshi wa kudumu kwa hiyari katika jeshi la nchi na kulazimishwa kuwa mwanajeshi mamluki wakati wa vita.

..mimi naona yote ni kutafuta maisha.

..zaidi huyo bwana hakuwa askari hapa Tz hivyo hatuwezi kumtuhumu kwa utoro au uasi.

..Ni hatujui role yake ilikuwa ni combat au non-combat.
 
Kaka ubalozi umehoji hao weusi huko Russia wanalazimishwa au matakwa yao? Kuna habari kuwa wafungwa weusi wanashawishiwa kuingia vitani ili vita ikiisha wawe huru

..hata hapa Tz wafungwa wanapigwa na kufanyishwa kazi ngumu.

..pia hatujui kama bwana Nemes alijiunga na jeshi kwa hiyari au kwa kulazimishwa.

..pia hatujui role yake ktk vita ilikuwa ni combat au non-combat.
 
Hiyo haiwahusu muhuni alikua kwenye harakat za kutafuta maisha, mi mwenyewe nimeamua kuwa mercenary
Nikajiunge PMC wagner group kutafuta maisha vitani
 
Ubalozi wa Marekani kupitia taarifa waliyoweka kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, Wamehoji juu ya utata wa kifo cha kijana wa raia wa Tqnzania aliyefariki akipigana vita Urusi.

Ubalozi huo umehoji pia kama Urusi inawalazimisha wafungwa wenye asili ya Afrika kupigana vita yake na Ukraine.

View attachment 2488873
Waliotunguliwa na ndege ya Ukraine mwanzoni mwa operation alikuwamo mtz mbona hawkuhoji. Waache unafiki mashoga hao
 
Ubalozi wa Marekani kupitia taarifa waliyoweka kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, Wamehoji juu ya utata wa kifo cha kijana wa raia wa Tqnzania aliyefariki akipigana vita Urusi.

Ubalozi huo umehoji pia kama Urusi inawalazimisha wafungwa wenye asili ya Afrika kupigana vita yake na Ukraine.

View attachment 2488873
Sasa kama wanajeshi wa urusi wamemalizwa na Ukraine Urusi ijitetee vipi?
Itafika mahali urusi italazimisha raia wake wanaougua maradhi yasiyo na tiba kwenda vitani kupigana kuwaondolea kufa bure tu.
 
..naunga mkono hoja.

..kuna kijana wa Kitanzania ni askari ktk jeshi la Marekani lakini hakuna mtu amelalamika.
Huyu ni JokaKuu the legend ninayemjua mimi ndiye ume comment hii?
Kwa heshima niliyo nayo kwako sitaku challenge wala sitafafanua. Acha niifumbie macho.
 
Serikali ya Russia inatakiwa kutolea hili suala maelezo yanayojitosheleza, ni jukumu lao na wajibu kwao.
 
..hata hapa Tz wafungwa wanapigwa na kufanyishwa kazi ngumu.

..pia hatujui kama bwana Nemes alijiunga na jeshi kwa hiyari au kwa kulazimishwa.

..pia hatujui role yake ktk vita ilikuwa ni combat au non-combat.
Sasa haya ndio yanahitaji maelezo toka serikali ya Urusi, kwangu Mmarekani yupo sahihi.

Kumuunga mkono Mrusi kwenye hili suala, ni sawa na kutaka maswali kama hayo hapo juu uliyouliza yasitolewe maelezo, which is not correct.
 
..naunga mkono hoja.

..kuna kijana wa Kitanzania ni askari ktk jeshi la Marekani lakini hakuna mtu amelalamika.
Kuna tofauti, kama unamuongelea nnae mfahamu yule jamaa ni Marine na alienda huko kusomea hadi kupata hio kazi.

Huyu marehemu alikua mercenary tu, Sidhan hata kama alikua na mafunzo ya kijeshi. Mara ngapi tunaona kwenye vita watu ambao hata sio skilled kuvita wanapewa mafunzo basic af wanawekwa frontline kama human shield? Watu wanapumbazwa na marehemu kuagwa kijeshi lkn sio jeshi la nchi lilimuaga ni haohao wagner ambao kiukweli wangekua africa hawana tofauti na kina m23
 
Kama alipigana kama mercenaries alipwe mpunga,poa tu ni moja ya utafutaji

Ova
 
Back
Top Bottom