YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 52,001
Ubalozi wa Marekani waongo wakubwa. Watanzania tuna njia yetu rahisi ya kujua tatizo la corona ni kubwa kiasi gani hawawezi kutudanganya hawa watu wa ubaloziliki ya pichaAFP
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa tahadhari mpya ya afya na kusisitiza kuwa hatari ya maambukizi ya virusi vya corona bado ipo juu jijini Dar es Salaam.
Kujua kirahisi kama tatizo la corona Ni kubwa sana Dar es salaam au Tanzania jiulize kwenye ukoo wako upande wa baba yako na mama yako na mke au mume wangapi wameugua ugonjwa wa corona, wangapi wamekufa kwa corona, wangapi bado wanatibiwa corona na je maambukizi ya corona yanaongezeka kwenye hizo koo zako au yanapungua?
Hutakiwi kusema tu ohh serikali inaficha takwimu. Hakiki wewe mwenyewe kwenye ukoo wako; takwimu ambazo ni rahisi tu kuzipata sababu wewe ni sehemu ya wanaukoo.
Usilishwe takwimu hewa ya kufikirika za wazushi kama hawa wa ubalozi wa marekani wawe au wa vijiweni,wanasiasa au mitandaoni hakiki mwenyewe. Uzuri kwa sisi Waafrika tuna koo kubwa sana na ni rahisi kujua tatizo likitokea kubwa kwenye ukoo, taarifa ni rahisi kupata.
Marekani unaweza toa statement general kama ya huyo balozi wa marekani sababu kule
wanaishi maisha ya kujifungia kila mtu kivyake hakuna ,mtu hata jirani hamjuani kule rahisi kudanganya hata kusema ohh kwenye huu mtaa kuna watu kibao wanaumwa au wamekufa kwa corona sababu hakuna amjuaye jirani!!! Sio Tanzania au Dar es salaam
Huyu balozi muongo tena sana .Dar es salaam watanzania tunajuana mgonjwa akiugua mtaani mtaa mzima utajua au ndugu wote watajua au ukoo utajua
Hao walio na maambukizi makubwa dar es salaaam ni wafanyakazi wa ofisi ya ubalozi ambao ni wamarekani au wapi?
maisha yetu tunajuana hatuishi kama wamarekani huu uongo wake waletwe CIA au FBI waje wa verify kama huyu balozi hatatimuliwa kwa kutoa taarifa za uongo kwa wamarekani