Ubalozi wa Marekani wamkumbuka Mwl. Nyerere. Wasema "maendeleo ni watu sio vitu"

Nyerere alikuwa mjamaa ila alikuwa haogopi kupambana na hao mabeberu kwa hoja.

Ndio maana wanamheshimu mpaka leo.
 
Sitaandika mengi Leo,
Watanzania tujifunze kutoka Libya na pia tusisahau kufuatilia historia ya utajiri wa U.S.

Ila yangu ni haya,
Tusimsikilize U. S kwa lolote kwani U. S hajawai kuwa mtu mwema.
Huwa ni mtu wa ku take advantage nyakati za vita na nyakati za uchaguzi. Rejea vita ya kwanza ya dunia, vita ya pili ya dunia na vita za wenyewe kwa wenyewe katika nchi mbalimbali.

lakini pia msisahau kurejea hotuba zao kile kipindi cha mwanzo wakati China anapambana na corona huku wao wakichekelea kwamba uchumi wao utaoenda kupanda kwa kasi. Na wakawaahidi China watatengeneza dawa.

Hizi ndio dili za hawa jamaa kuuza silaha wakati sisi tumekorofishana huku wao wanachukua mali zetu.
Rejea Libya tuache ushabiki wa kuwashabikia angalia kizazi chako cha mbele.

Lazima tutumie mbinu zetu wenyewe kutoka nchi zilizo jipatia maendeleo kwa njia halali. Maendeleo yaliyopatikana kwa watu kufanya kazi kwa bidii.

Zipo nchi nyingi.
Na swala la maendeleo ni vitu ni muhimu sana kwani tunahitaji miundombinu imara ili watu wawe na maendeleo.

Ni hayo tu
 
Ndugu hakuna haja ya kuhangaika na hawa chadema wanaohangaika kukata roho. Ina maana wao sera yao ni ipi? In short hakuna maendeleo ya watu bila vitu labda kama kuna vitu wanavyovilenga wao watuambie waziwazi ni vitu gani ambavyo ambavyo havileti maendeleo vinavyofanywa na serilai ya awamu ya tano. Wanaitumia kauli ya mwalimu Nyerere kisiasa tena kwa kuipotosha zaidi. Hivi niulize swali moja tu, Ni vitu gani ambavyo serikali ya awamu ya tano chini ya Jemedali Magufuli inavifanya ambavyo havikufanyika wakati wa serikali ya awamu ya kwanza chini ya mwalimu Nyerere?

Je Nyerere hakujenga mabawa ya umeme tena kwa fedha za mkopo, hakujenga reli (TAZARA) tena kwa mkopo wenye riba nafuu/usiokuwa nba riba, Hakujenga vivuko na madaraja, hakujenga shule za msingi, sekondari na vyuo, hakujenga viwanda, hakujenga zahanati, vituo vya afya na hospitali, hakununua ndege 11 kwa ajili ya shirika la AirTanzania, hakujenga barabara hata kama ni za changarawe (kulingana na uchiumi wetu wakati huo, hakutengeneza na kukarabati meli kwenye maziwa na bahari ya nchi yetu, Hakuwekeza kwenye kuboresha bandari zetu n.k n.k n.k? CHADEMA NI CHAMA KILICHOKOSA SERA NA ITIKADI INAYOELEWEKA WAMEBAKI KUONGEA PUMBA TU. TUNATAKA CHADEMA WATUAMBIE WAO WAKIINGIA MADARAKANI WATAFANYA NINI NA WALA SI KULAUMU BILA KUTUAMBIA NJIA MBADALA.

Kimsingi Raisi Magufuli ndiye anayemuenzi kimatendo mwalimu Nyerere kwa kufanya yale yote ambayo mwalimu aliamini kwamba ndio chachu ya maendeleo ya watanzania.
 
 

Kama ni watu mbona wao kila siku wana lalamikiwa na wananchi wao bajeti ya jeshi kuwa kubwa na mavifaa ya kivita.watu kome
 
Kwa hiyo ni sawa baba kununua gari nyumbani huku watoto wakishinda na njaa kisa tu hilo gari watoto hao watapanda??

Maendeleo ya vitu ni mazuri mno kama tu yatafanyika without expenses za maendeleo ya watu.

Yaani ndege zinunuliwe huku ajira za kutosha zitangazwe na vijana wapate kipato.

Yaani reli ya SGR ijengwe huku sekta ya kilimo iwezeshwe kwa ufanisi na wakulima watafutiwe masoko yatakayowafaa na kuwaiingizia kipato.

Shule zijengwe huku wanafunzi wote wapate mikopo kwa wanaohitaji pasipo kuwabagua waliosoma shule binafsi.

Bwawa la Nyerere lijengwe lakini watumishi waongezwe mishahara ili kuendana na hali halisi ya maisha ya sasa.

Nadhani utapata picha kidogo hapa
 
Vizuri. Kujenga kituo cha afya, kukipatia madaktari, na kukipatia dawa za wagonjwa ni maendeleo ya watu. Kununua ndege nyingi sana, kujenga flyover wakati hakuna dawa mahospitalini na kipato kimeshuka ni maendeleo ya vitu tu bila watu.
 
Mkuu sasa misaada yao kama USD 300 Million walizozitoa mbona hamzikatai?

Mwanamke anayekukataa hadharani huku akila pesa yako sirini,huyu tunamuitaje lakini?

Kama nyie ni wanaume kataeni misaada yao ili taifa huru mnalolitaka lipatikane!
 
Tena kule kumejaa wanawake wengi weupe weupe, tatizo lao ni wao kuongea lugha ya malkia tu.
 
Ukweli wa kauli ya Nyerere ni huu sio tafsiri mnazo taka nyinyi

 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…