Na kwa vile leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Nyerere Day, tuiadhimishe kwa kuwapongeze viongozi wetu wote wanao muenzi Nyerere kwa kumuishi kwa maneno na matendo, Rais Magufuli ni mmoja wao. Miradi ya Umeme wa Stigler Gorge na kuhamia Dodoma ni kutimiza ndoto za Nyerere.
Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kiukweli ukweli, nina kaswali kadogo, kitendo cha Rais Magufuli cha kuendelea kumuishi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa maneno na matendo, kwa vile Nyerere alitawala Tanzania kwa kipindi cha miaka 23, na Magufuli anafana na Nyerere, jee unaonaje pia katika kutawala, ili Magufuli azidi zaidi kufanana na Nyerere, mnaonaje tukimpa Magufuli muda kama wa Nyerere au kwa kukaribiana tu japo vipindi viwili vya miaka 10/10?.
Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa dhati, naomba kutumia fursa hii, kuwahimiza wale wote wanaomkubali Nyerere, tarehe 28 October, Watanzania tusifanye makosa, ni asubuhi na mapema, kuwahi katika kituo cha kupigia kura, kumchagua Nyerere wa pili, na ukifika, kazi ni moja tuu,
unachukua...,
unaweka...
malizia...
Happy Nyerere Day.
Paskali