Soma kwa akili wewe kijana! Kwani nimezuia SGR isijengwe au?Hujui matokeo ya SGR katika uchumi wa Tanzania, huwezi kutambua matokeo ya Bwawa la Umeme Julius nyerere? Kama huwezi kutambua hayo inakubidi urudi shule ukajifunze upya.
Kibaya sijamsikia Mkuu wa nchi akitamka neno haki tangu aanze kampeni zake.Kama kuna kitu ambacho Lissu amepatia ni kutumia falsafa ya Nyerere kama sehemu ya kampeni yake. Hapo amecheza kama Messi.
CCM hakifanani kabisa tena na chama alichokianzisha Nyerere. Wameachana na misingi yote ambayo walikuwa wanaisimamia. Nikitumia maneno ya Kolimba, kimepoteza dira.
Wewe na Raisi wako ndio mnatakiwa mrudi shule tena, ili kujua kuwa ilipaswa kujenga daraja pale Jangwani kuliko SalenderHujui matokeo ya SGR katika uchumi wa Tanzania, huwezi kutambua matokeo ya Bwawa la Umeme Julius nyerere? Kama huwezi kutambua hayo inakubidi urudi shule ukajifunze upya.
Baba wa Taifa anasema maendeleo yasiwe yametokana na kunyonya watu - upo hapo?Kwa hiyo ni sawa baba kununua gari nyumbani huku watoto wakishinda na njaa kisa tu hilo gari watoto hao watapanda??
Maendeleo ya vitu ni mazuri mno kama tu yatafanyika without expenses za maendeleo ya watu.
Yaani ndege zinunuliwe huku ajira za kutosha zitangazwe na vijana wapate kipato.
Yaani reli ya SGR ijengwe huku sekta ya kilimo iwezeshwe kwa ufanisi na wakulima watafutiwe masoko yatakayowafaa na kuwaiingizia kipato.
Shule zijengwe huku wanafunzi wote wapate mikopo kwa wanaohitaji pasipo kuwabagua waliosoma shule binafsi.
Bwawa la Nyerere lijengwe lakini watumishi waongezwe mishahara ili kuendana na hali halisi ya maisha ya sasa.
Nadhani utapata picha kidogo hapa
Soma tena nilichoandika,kisha soma tena ulichoandika,alafu niambie kama kuna utofauti!Baba wa Taifa anasema maendeleo yasiwe yametokana na kunyonya watu - upo hapo?
Sasa basi kwetu tumeambiwa mishahara haiongezwi mpaka miradi mikubwa ya kimkakati itakapomalizika. Huko si kuwanyonya watu?
NiiceUongo .Idadi ya watu marekani sensa ya 2017 walikuwa 326,971,407 wakati mamilionea walikuwa milioni 11 kwa mwaka huo ukitoa hapo utapata watu milioni 321,971,407 hawako kundi la mamilionea