#COVID19 Ubalozi wa Marekani, watoa tahadhari dhidi ya ongezeko kubwa la ugonjwa wa Covid-19

#COVID19 Ubalozi wa Marekani, watoa tahadhari dhidi ya ongezeko kubwa la ugonjwa wa Covid-19

Kwa kauli zako hapo juu tayari wewe ni mjuaji labda kama hujui maana ya ujuaji. Ubalozi umetoa tahadhari kwa watu wao, wewe kwa ujuaji wako unajifanya kukosoa andiko lisilokuhusu. Wewe endelea na kazi kama unavyojigamba na hutishwi na chochote.
Kabla hawajatoa kauli serikali ilishatoa kauli yake. Au hukuisikia🙄
Chukua tahadhari, chapa kazi, Kula vizuri, muombe Mungu 🙏
 
Jishaue tu, unadhani kila kitu kinahitaji propaganda za kisiasa, iko siku mtavuna mnachopanda.
Wewe hujioni unavyojishaulia kwenye ubalozi wa Marekani!? Sijui unahamia lini America😂😂😂

Yaani unajishau hadi unashindwa kufikiri.

Wewe unavyoona suluhu ya corona ni nini?
 
Sijui unaandika haya ukiwa wapi, inawezekana umejifungia ndani hujui chochote kinachotokea mtaa wa pili, kwa taarifa yako mkiendekeza hizi taarabu Corona itapokuja kupiga hapo sebleni kwako ndio utapata akili, now unaisikia kwa majirani ndio maana unaleta utani, na usiombe iwatembelee ndani kwasababu haiondoki na mmoja.
Nenda marekani hakuna korona wameisha ishinda wao huko.

Sent from my Infinix X655 using JamiiForums mobile app
 
Corona inaua sio utani, rafiki kafariki tumemzika mchana, kaanza kuumwa asubuhi shida kupumua mchana kafariki saa tisa tumetoka kumzika, nilivyoona ile misafara ya Coaster inayosindikiza marehemu wao mikoani sina hamu kabisa.

Kama mpaka sasa bado kuna mtu asieamini Tanzania kuna Corona Mungu amrehemu.
Huyo atakuwa amechoka kuishi kama shetani sasa anatafuta nafasi awahi kwa muumba
 
Hebu watupumzishe! Wameshindwa kuzuia vifo100 vya kupigwa risasi kila siku halafu hapa wanataka kutuongopea wanajali uhai wetuwetu.

Tuko zetu busy na kazi huku tukichukua tahadhari na kumwomba Mungu sana.
Ukiambiwa kuwa njaa imekupanda kichwani unarusha ngumi hewani
 
Back
Top Bottom