Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
Katika pitapita zangu katika maeneo mbalimbali ya viunga vya Jiji la Dar es Salaam, nimeshuhudia hivi karibuni mfumuko wa mabango na makaratasi mbalimbali ya kumnadi mgombea wa Urais wa CCM, John Magufuli pamoja na baadhi ya wagombea wa CCM wa Ubunge na hata Udiwani.
Makaratasi hayo inaonyesha yamebandikwa kwa fujo na jeuri fulani huku ikionyesha waliobandika walikuwa na kinga fulani.
Kwa mfano, nimeyaona katika kuta za ofisi za umma mfano bodi ya Utalii.
Cha kufurahisha ni pale nilipooona makaratasi yaliyobandikwa katika kuta za ubalozi wa Ufaransa, yakiwa yamefutwa ingawa kwa sababu yaliwekwa na gundi, yameharibu kuta zile.
Swali langu ni, hizi fujo kuchafua maeneo ya umma, ofisi za taasisi zisizofungamana na upande wowote, ofisi za umma na za watu binafsi pamoja na makazi yao bila idhaa yao, si kinyume cha sheria?