Uber yasitisha huduma zake Tanzania, yazitaja nauli elekezi Latra kama sababu. Itarejea kanuni zikibadilishwa

Inaweza kuwa kuna rafiki, ndugu au shemeji yako au mtu wako katika familia amekutana na kadhia hii na kumfanya akose ridhiki yake ya kila siku.

Je ? Umefurahia anguko lake katika hustling zake?
Uber nayo utaita hustling?
 
Sasa hii barua haina hata Logo au stamp au signature si mtu yoyote anaweza kuandika tu. Hebu tuwe serious kidogo barua sio namna hii tena yenye mambo mazito kama haya.
 
Sasa hii barua haina hata Logo au stamp au signature si mtu yoyote anaweza kuandika tu. Hebu tuwe serious kidogo barua sio namna hii tena yenye mambo mazito kama haya.
Simple tu, wewe fanya kutokuamini hio barua then endelea na mambo yako mengine.
 
bro mimi ni dereva wa bolt hyo bei unayosema hapo ya bolt tujiulize wote 10000 hyo bolt wanakata 23.5%kama comision yao dereva anabaki na shilingi ngapi?? bolt wanaumiza sana madereva kwa kigezo cha kumjali mteja kitu ambacho sio sahihi, Latra wametoa bei elekezi na wamewaambia comision yao isizidi 15% nauli za mchana na usiku zitofautioane. na hapo hii bei elekezi LATRA walitoa kabla hata ya mafuta kupanda kama yalivyo sasa. wao wanataka waendelee na bei za zamani na commisiom za zamani dereva na mwenye chombo atapata faida gani??
 
Haya sasa nanunua Passo,Ist na vitz kwa mafungu,zikianzia gari tano zitahesabika kama fungu moja m5 unapewa utaki unaacha.
 
Je wanaopanda ambao wengi ni waajiriwa wamepandishwa mishahara?
 
Kwan wanalazimishwa? Wewe mbona unalipwa mshahara kidogo hatusemi
Unaongea bila kuzingatia usawa. Uber wanakata karibu asilimia 30 ambayo kimsingi ni kubwa sana. Anatumia hizo kauli za kikatili kwamba kwani mnalazimishwa?

Mshahara wangu ni mkubwa sana.
 
Huyu mama alifeli mapema sana. Ile hotuba yake ya kwanza aliposema...."mimi ndiye raisi na mimi ni mwanamke". Nilimuweka pembeni saa ileile.
Hakuwa na haja ya kusema yeye ni mwanamke,ni dalili ya kujitutumua.
 
posta mwenge nauli Tsh 23,000/= hiv unaandika uhalisia au ushawah kua dereva wa uber ukapata nauli posta mwenge Tsh 23,000?
 
Kwani kabla ya Ubar mlikua mnatumia nn? Tuanzie hapo kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…