Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Basi urais tumpe mama yako yule kipofu muuza sambusaHuyu mama hafai kuwa rais assee anaongea bila uchungu kabisa
Mimi hii tumbo limenichezaHuu uzi umetia uchungu mithili ya ule wa kujifungua
😁😁😁😁🙌🙌🙌Hatari .
Nchi imefunguliwa mpaka imeanza kujifunga yenyewe.
Uber watarudi trust me..!Bolt wanaendelea na Kazi.
Anyway Maisha lazima yaendelee...
Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Bolt wanaendelea na Kazi.
Anyway Maisha lazima yaendelee...
Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Mtoa mada umeona vyema. Lakini tufanye nini ili mambo kama haya yakomeshwe. Wapi tunakosea kiasi cha kuchezewa na wawekezaji uchwara?Tumepigwa tena na kitu kizito kichwani watanganyika![emoji31]
Uber ni bepari ... Bepari sifa yake ni uchoyo uliopitiliza(craving) anapenda mno kupokea lakini kutoa japo kidogo ni mchungu mno na anaumia mno..!
Sababu alizotoa Uber kufungasha virago baada ya MIAKA 6 ya kufanya biashara nchini naweza kusema ni nyepesi na za kijinga mno... Kapiga ndefu ndani ya miaka mitano ya bila kodi kama sheria inavyosema kwa wawekezaji wakubwa.. Huu ni mwaka wa sita anatakiwa sasa aoneshe hesabu zake kwa ujumla kama alipata faida ili aanze kulipa kodi stahiki sasa.. ANAKIMBIA[emoji35][emoji34]
Tumeliwa kwa miaka mitano mtu kaja na mkoba anaondoka na utajiri mkubwa.. Uber hayuko peke yake katumia udhaifu wa sheria ya kuvutia uwekezaji na wawekezaji kama wengine walivyofanya kwenye
Makampuni ya madini
Kwenye mahoteli makubwa nchini
Kwenye viwanda mbalimbali vya wageni
Kwenye uwekezaji wa kina aina..!
Tumeshuhudia kwa uchungu mno tangu enzi za Mkapa watu waki DECLARE LOSS baada ya miaka mitano ya uwekezaji lakini hapo hapo walichokisema hakina faida wakawauzia 'wenzao' (kumbe ni wenyewe) kisha nao wakapata msamaha wa miaka mitano.. Ndio maana kila baada ya miaka mitano makampuni yanabadili majina biashara inaanza upya..! Tunaliwa mpaka sehemu za aibu wallah[emoji35][emoji43]
Na haya yote yanafanyika kwa msaada wa wazawa wenyewe..watu wetu waliokosa uzalendo na uaminifu ... Lakini kama mamlaka zinaiba kura ili zibaki madarakani wao ni nani wasile kwa urefu wa kamba zao?? Tanganyika yangu iko mnadani
Uber sio pekee anayefanya biashara ya usafiri nchini.. Matatizo kwenye mamlaka ni kweli yapo mengi tu lakini hayajafikia kiwango cha sababu walizotoa uber
Wana gari almost mpya
Gari zao ni za cc ndogo sana
Gari zao karibia zote zimefungwa mfumo wa gesi
Wanawabana mno madereva
Kodi wanazolipa si halisi wanachakachua mno.. Leo wanasema wameshindwa phyuuu... Mtuhurumie jamanim..!
Na ukijua bado wanatatutamani wamesema kanuni zikirekebishwa watarejea ..[emoji23] ni wahuni sana hawa jamaa.. Wanajua wazi baada ya bunge la bajeti kupita kuna sheria na kanuni mbalimbali zitafanyiwa marekebisho.. Hapo ndipo wanaposubiri wapate kisingizio cha kurejea na kupata miaka mingjne mitano kama sheria ya kuvutia uwekezaji inavyotaka
Wangeweza kubadili jina kidogo tu wasingeondoka.. Lakini inaelekea huko jikoni magazijuto yaligoma maana jina lao ni brand world wide!.. Sasa hesabu zote zinafungwa waliopiga wamepiga kila mtu kwa urefu wa kamba yake!
Ninayemuonea huruma ni mtanganyika kwa hali zote kuanzia huduma muhimu za jamii mpaka future yake kama mwananchi.. Mimi wewe yule na sisi sote tunaoendelea kupigwa na vitu vizito kwa ghiliba za watawala na mapebari kupitia chama chawala...[emoji848][emoji2827]