Ubinafsi wa Mayele unavyoighalimu Yanga

Ubinafsi wa Mayele unavyoighalimu Yanga

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Mayele ni mchezaji mzuri hasa kwa jitihada zake za kujituma awapo uwanjani. Ila kwa mtazamo wangu licha ya mazuri yake kwa upande mwingine amekuwa akiighalimu sana timu kutokana na uchoyo uliopitiliza. Mechi ya leo na Simba amepiga mashuti mengi akiwa katikati ya uwanja badala ya kuwapa wenzake waliokuwa wamefungua.

Njoo kwenye mechi zile mbili na Al Hilal (home & away) ubinafsi wake ulichangia Yanga kufunga magoli machache hapa nyumbani na kupelekea kutolewa. Amekuwa akilazimisha kufanya vitu vingi peke ake akisahau kuwa mpira ni mchezo wa timu.

Anacheza kutafta "Personal glory" kuliko "Team success". Mara kadhaa nimekua nikimuona kocha akimkumbusha lakini habadiliki.

Mechi ya Dabi km ya leo ni mechi inayochezwa kimkakati sana. Ukicheza kibinafsi vile unawaraisishia wapinzani kukukaba na ndivyo Simba walivyofanikiwa. Kutokana na sifa anazosifiwa Mayele amekuwa akicheza kifadha sana.

Anapoteza mipira mingi na kwa uzembe kabisa! Siamini kama Nabi ameshindwa kumbadilisha na kama ni hivo basi uongozi uingilie kati kwa manufaa ya timu.

Namkumbusha Mayele, mashabiki wa Simba na Yanga huwa hawana mapenzi ya kudumu. Asione watu wapo kimya siku wakilipuka asishangae akianza kuzomewa, kama haamini amuulize Boko. Licha ya timu nzima kutocheza vizuri leo ila Mayele kazingua sana.

Hongereni Simba though, na poleni Utopolo.
 
Utoh!!! mshukuruni mayele japo kwa kidogo alichofanya.. bila yeye msingekuwa na on target hata moja.....
Kwamba zile Ally Salim alikuwa anapongezwa kwa michomo ya Mayele pekee? Zile za Aziz Ki na Morison hazihesabiki kama on target?
 
Mayele ni mchezaji mzuri hasa kwa jitihada zake za kujituma awapo uwanjani. Ila kwa mtazamo wangu licha ya mazuri yake kwa upande mwingine amekuwa akiighalimu sana timu kutokana na uchoyo uliopitiliza. Mechi ya leo na Simba amepiga mashuti mengi akiwa katikati ya uwanja badala ya kuwapa wenzake waliokuwa wamefungua.

Njoo kwenye mechi zile mbili na Al hilal( home & away) ubinafsi wake ulichangia Yanga kufunga magoli machache hapa nyumbani na kupelekea kutolewa. Amekuwa akilazimisha kufanya vitu vingi peke ake akisahau kuwa mpira ni mchezo wa timu. Anacheza kutafta "personal glory" kuliko "team success".Mara kadhaa nimekua nikimuona kocha akimkumbusha lakini habadiliki.

Mechi ya Dabi km ya leo ni mechi inayochezwa kimkakati sana. Ukicheza kibinafsi vile unawaraisishia wapinzani kukukaba na ndivyo Simba walivyofanikiwa. Kutokana na sifa anazosifiwa Mayele amekuwa akicheza kifadha sana. Anapoteza mipira mingi na kwa uzembe kabisa! Siamini km Nabi ameshindwa kumbadilisha na km ni hivo basi uongozi uingilie kati kwa manufaa ya timu.

Namkumbusha Mayele mashabiki wa Simba na Yanga huwa hawana mapenzi ya kudumu. Asione watu wapo kimya siku wakilipuka asishangae akianza kuzomewa, km haamini amuulize Boko.
Licha ya timu nzima kutocheza vzr leo ila Mayele kazingua sana.

Hongereni Simba though na poleni Utopolo.

Kule mbele anaecheza kitimu ni yule Kenedy Juma sorry nani vile Musonda
 
Back
Top Bottom