Naunga Mkono kurekebisha Kero za Muungano lakini siungi Mkono Kuvunjika Kwa Muungano.
Siungi Mkono Serikali Tatu, Hii itawapa uhalali kabisa Zanzibar kuwa Nchi inayojitegemea na Muungano hautakua na Maana yoyote.
Katiba inapaswa kuwa Moja, Raisi Mmoja, Baraza la Mawaziri Moja na Wimbo mmoja wa Taifa. Ardhi yote iliyopo Tanzania iwe chini ya Wa Tanzania wotee Bila Kujali Eneo la Kijiografia, hoja ya Kusema Zanzibar ni ndogo Ardhi ibaki Kwa wazanzibar ni hoja mfu isiyo na Mashiko yoyote.
Hata wachina Leo Hii wanahangaika kuileta HongKong na Taiwan kuwa sehemu Moja na sio Ile One Country two Systems, Huu ni Uhuni. Huwezi ukasema Una nchi halafu watu wake wamegawanyika na wanaviongozi tofauti. Itakuaje Siku Raisi wa Zanzibar akiamua kusaliti na Kupewa Nguvu na Mataifa Dhalimu maana hata Askari japo wako chini ya Jeshi Moja lakini tayari wako katika Nchi inayojitegemea kbisa kikatiba na Raisi.