Sisi wakazi wa kingolwira majengo mapya (mtaa wa bomba la mafuta).
Kuna miundo mbinu ya maji iliwekwa zamani na miradi ya Mh Mariam ditopile ambayo ilifika kwetu na maji tulikuwa tunapata vizuri tu hadi april mwaka jana 2021.(sisi tunaamini before JPM passing).
Yalitoka vizuri iwe mvua liwe jua.ila kwa sasa hatupati maji .
Toka august mita zetu hazisomi maji tunauziwa na bowser kwa sh 20000 kwa lt 1000 kwa vile huku ni mbali.(inatugharimu).
Mwanzo tuliambiwa ni ukame, mvua imenyesha tunaambiwa ni matope,
Ajabu ni taasisi za karibu tunaotumia mradi hii ya karibu karibu yaani maeneo ya chem chem ya mlima yaani magereza, jeshi na mkambarani hadi mikese wao hawakuwa na kadhia hii, Jeshi la pangawe wanauza masaa 24 mabomba 4 na utokaji ni presha nzuri sana.ajabu sisi tulio chini ya mlima wa jeshi hatupati ni IMANI pamefungwa mahali kututaabisha.
Sisi tunaambiwa ufumbuzi ni kuusubiria mradi wa mwindu, mazimbu, lukobe, yepsa , tungi na kingolwira ufike.
Tunachokiona moja SSH anahujumiwa.watu kauli zao ni kabla yalitoka ila baada ya kutenguliwa mkurugenzi wa moruwasa hatupati maji.
Pili, Diwani ni magumashi ni mbabe na watu tunamuogopa.
Tatu mkuu wa wilaya amekagua sana vyanzo vya maji lakini waliandaa mabomba na kumwambia wanabadili mradi wa zamani kwenye ule mradi aliowahi simamia Ditopile.
Sasa mvua zinanyesha hatujapata hata tone na ni wiki ya pili mvua zinanyesha.