Ubora wa Paul Matthysse a.k.a P-Funk Majani wa Bongo Records

MKuu kuna ngoma nimeitafuta hapa lakini nimeikosa, nini mnataka mazee ya Pig black. Kama unayo naomba uitupie hapa, shukrani!

Mkuu salama

Ngoma ipo hapa, anzia mwanzo utaipata.!
 
zacha pandisha Homa ya dunia- Solo thang- produced by P-Funky

Kwa mtazamo wangu huu ndio wimbo bora daima wa Hip Hop,kwa message iliyomo,floor ya kunata na beat,instruments arrangement . ni wimbo ambao ukiusikiliza maneno yake ni kama mpya umetoka studio.

Bahati mbaya sana Solo alimezwa na album ya Juma Nature- Ugali na ya Prof Jay
 

Mkuu uko vizuri.
Sawa ntajitahidi kesho mapema
 

Attachments

Kwa mtazamo wangu huu ndio wimbo bora daima wa Hip Hop,kwa message iliyomo,floor ya kunata na beat,instruments arrangement . ni wimbo ambao ukiusikiliza maneno yake ni kama mpya umetoka studio.

Mimi kila nikisikiliza Tunasonga naona kama umeandikwa jana.
 
Asee acheni masihara hao producers wengine ni kweli walikuwa na mchango wao ila si kweli kwamba wao ndo walimsimamisha P funky,yule jamaa alikuwa na uwezo Wa ajabu
Ila majani nadhani bado hajatangaza rasmi kuacha uproducer imekuaje siku hizi yupo kimya?

Ila pia nadhani miaka ile producers walikua wachache sana na yeye ndio alitengeneza ngoma nyingi, hakuwa na watu wengi wa kucompete nae ila kwa zama hizi producers wako wengi na wenye uwezo pia.
 
Mimi naamini jamaa ametumia nguvu na ajuzi Wa ke kwa muda mrefu so ni kama ameishiwa aidia hivi. Ila alivyokuwa kwenye peak sidhani kama kuna mtayarishaji atakuja kufika kiwango cha huyo jamaa. Kwanza alikuwa anapenda mziki akiegemea zaidi ktk vipaji vya kweli. Alikuwa anatengeneza mziki kwa mizuka
 
T

Hey sikiliza Homa ya dunia mwanzo mwisho,then to a mawazo!!
Mkuu umepiga penyewe.
Kwangu mimi huu ndio wimbo bora zaidi wa hip hop hapa bongo.
Ile msg mpaka kesho bado itasimama.
Tatizo ni kwamba wabongo wengi huwa hatupendi nyimbo za aina hii,huwa tunapenda nyimbo nyepesi zenye utani utani ndani yake.
Na ndio maana album ya homa ya dunia ya Solo ilimezwa na ile ya Nature kama ulivyosema hapo juu kwa sababu Nature alikuwa akiimba vitu vya masihara sijui ndio rap katuni!.
Ila album ya HOMA YA DUNIA ilishiba song zenye ujumbe na burudani kama vile homa ya dunia yenyewe,sukari ina pilipili,msako wa haki,mambo ya pwani,vina utata n.k.
Daaaaaah...
Machozi yanatoka ishara homa ya dunia
Binadamu wanyama ndege wote mbona mnalia
Parapanda italia,mito milima mabonde vyote vitaangamia
Madaktari waganga ujuzi washautumia
Wamemzunguuka mgonjwa homa ya dunia
Waumini wamemsalia
Na bado mikononi akawafia...
 
Hilo halina ubishi mkuu,
Ulamaa hiyo ngoma aliandika hasa
 
Weka ngoma alizosaidiwa na hao producers wengine
Na mimi niweke alizofanya mwenyewe halafu tufanye comparison tuone Majani ni nani!
Nna uhakika crown itarudi palepale ilipo kweny kichwa cha Halfan Majani
 
Hiyo chorus tu lazima ikufanye utafakari
 
Kuishiwa idea hapana,
Beat making imekuwa rahisi sana siku hizi kutokana na technology na ndio mana madogo kibao asa iv wanafanya production za kutisha.
Nadhani ni ile tu kwamba kila nabii na zama zake.
Leo hii kule mbele hatusikii mikono ya Dr Dre,dj premier, lex lugger, scott storch wala the runners ila sasa iv kuna madogo kama metro boomin' wanafanya mambo makubwa
 

Mkuu hiyo chorus then na mpapaso wa instruments za Majani kwenye chorus ni zaidi ya movie fulani ya hatari,cha kusikitisha zaidi kuna watu wakawa wanamchotea tuzo Binamu kila mwaka wa tuzo eti mwandishi bora na album yake ikabebeshwa tuzo ya Album bora ila album ambayo haijajaa utunzi mzuri na nyimbo nzuri kama album ya Daz Baba- Elimu Dunia na Daz Baba atafariki bila hata tuzo yoyote!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…