Miundombinu ya usafiri na usafirishaji inajumuisha njia zote za usafiri na usafirishaji kama vile barabara, reli, anga na usafiri wa njia ya maji(bahari, maziwa na mito na mabwawa).
Miundombinu hii ni kichocheo kikubwa cha maendeleo na ukuaji wa uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja. Lakini kwa kiasi kikubwa hasa vijijini Miundombinu hii sio rafiki kwa matumizi ya jamii husika.
Ni dhahiri kuwa asilimia kubwa ya Watanzania wanaishi maeneo ya Vijijini ambapo hujihusisha na shughuli mbali mbali za uzalishaji mali kama vile kilimo, ufugaji, uvuvi, uwindaji, uchimbaji mdogo wa madini na biashara.
Hivyo maeneo haya ya Vijijini kwa kiasi kikubwa ndiyo vyanzo vya malighafi na mazao mbalimbali ambayo huhitajika mjini kwa ajili ya matumizi ya viwandani na matumizi ya majumbani, tunaweza kusema kuwa wanazalisha wa vijijini lakini wanatumia wa mijini.
Kwa mantiki hii tunaona kuwa maeneo ya Vijijini yana umuhimu mkubwa wa kuchangia maendeleo ya taifa na mtu mmoja mmoja kwa mijini na vijijini. Japokuwa maeneo hayo yana umuhimu mkubwa kwa ukuaji wa uchumi lakini bado mengi hayana Miundombinu rafiki kwa usafiri na usafirishaji, maeneo mengi yana barabara za msimu ambazo hupitika majira ya kiangazi tu ifikapo masika barabara huwa hazipitiki hivyo kuleta adha kwa wasafiri na watumiaji wengine wa barabara hizo ikiwemo wafanyabiashara.
Pia maeneo mengine hayana barabara kabisa hali inayowapa ugumu wazalishaji kusafirisha bidhaa zao hii hupelekea wazalishaji na wafanyabiashara kupata hasara kwani kuna baadhi ya malighafi na bidhaa ambazo haziwezi kuhimili kukaa muda mrefu.
Kuna maeneo mengine ambayo yamezungukwa na maji kama vile mito bahari na maziwa haya pia yana changamoto ya usafiri kwani hawana vivuko wala boti za kisasa bali hutumia njia za asili za usafiri ambazo si salama kwao na mali zao.
Lakini jambo la kutia moyo na matumaini ni kwamba serikali imeahidi kuendelea kuboresha Miundombinu ya usafiri vijijini kwa kuahidi kuipatia TARURA pesa zaidi ili kuendelea kuboresha barabara za vijiji na mitaa.
Miundombinu hii ya usafiri vijijini ikiboreshwa vizuri itaongeza ufanisi katika uzalishaji wa malighafi na mazao mbalimbali na usafirishaji utakuwa rahisi zaidi hivyo watu wa vijijini wataongeza vipato vyao na hatimaye ukuaji wa uchumi wa taifa zima.
Ni muhimu zaidi Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo kuhamasisha uboreshaji wa barabara za vijijini ila kupaisha maendeleo.
Uboreshaji wa Miundombinu ya usafiri na usafirishaji Vijijini ni kichocheo cha Maendeleo.

Upvote
0