Ubosi unanifanya nisiolewe, umri unazidi kusonga

Ubosi unanifanya nisiolewe, umri unazidi kusonga

1. Unapotoka nje ya mazingira ya kazi usiendelee na ubosi wako

2. Jichanganye kwenye makundi mema baada ya kutoka kazini kama wewe ni mkristo nenda kwenye vyama vya kitume au kwaya.

3.Jitahidi kuwa myenyekevu kwa watu waliokuzidi umri na tabia yako isomeke hadharani kuwa ni njema

4.Usiishi maisha ya juu sana kama kuendesha gari masaa yote kwani neema za wanaume unazikosa saa nyingine unapotembea kwa miguu ndio waoaji wanakuona na kuanza kukufukuzia

5. Usipende kuvaa vitu vya garama saana kwani kuna wanaume wema wataona wakikuoa utawaingiza hasara hata kama ana kipato

6. Epuka sana kuwa wa bandia kama kubadilisha ngozi na kuvaa madude mengi artificial kwani kuna wanaume wengi hutathmini mwanamke aliyebadilisha ngozi kuwa hata tabia yake anaweza kuibadilisha kama kinyonga jinsi apendavyo na ajiamini na uzuri aliopewa na Mungu

7.Usipende kukosoa wanaume hadharani kwani kwa yule unayemkosoa kuna wengine wanakufuatilia kwa siri bila kukuambia na ukiona kitu kidogo tuu gubu la kufa mtu basi na wao wanajitoa kiulaini

8. Epuka sana kufikiria kuolewa na msomi mwenzako ama tajiri bali yeyote utakayempenda na anayekupnda kwa dhati na mwenye tabia njema anaweza kukufaa na mkaishi maisha mazuri na ya amani kuliko msomi mwenzako ambaye kwanza kumpata inakuwa kazi kwani baadhi huoa ambao hawajasoma kwa sababu hushuhudia live vituko vinavyofanyika vyuoni

9. kubali utumwa na kamwe usishawishike na wanaharakati wanataka kuwa sawa na wanaume

10. Kumbuka kuwa katika muungano wowote kila mtu lazima apoteze sehemu ya uhuruwake na kupokea mapungufu ya mwenzake na kuyavumilia. Hivyo usitarajie mtu ambaye yupo pafect kama malaika ndio akuoe utakosa wale ambao uliowakataa kwa kusema sii kiwango chako masi kama bado wapo warudie kwa unjenyekevu laa sivyo "imbombo ngafu""

Ushauri mzuri kabisa huu
 
Afunguke hapa tu, nitamuelewa. Inbox wanaingia na wajinga.
Nipo Mimi nafunguka

Elimu yangu darasa la 7

Kazi mjasiliamali natembeza mitumba

Umri 35

Lugha Swahili, French, English, Rwanda,

Urefu 5.8"

Rangi mweusi

Makazi Pwani

Chakula ndizi samaki

Michezo mpira, karate,judo

Dini mkristo


Nisichopenda mwanamke mvaa wigi na nguo za kuonyesha maungo yake, ulevi na uzinzi napenda mwanamke ajiheshimu
 
Naomba unitumie namba yako ya simu au email tafadhali ili nikupatie ushauri Wa dhati na ambao MTU mwingine hawezi kuusoma.
 
Elimu Masters, Kazi international org. Mshahara wa kawaida maisha nayajua vzr sana labda ushindwe wewe. Karibu inbox
 
Kwani mabisi wenzako hawakuoni... ukizingatia mbona utakuwa bosi mdogo sana.. yaani hauna muda mrefu kwenye hicho cheo.. na pengine unakaimu tu. Angakia makosa yako yako wapi.. jirekebishe alafu uone.
 
Elimu Masters, Kazi international org. Mshahara wa kawaida maisha nayajua vzr sana labda ushindwe wewe. Karibu inbox
Sifa unazo za kutosha ashindwe mwenyewe ila ungesema mshahara kwa mwezi unapata kiasi gan?
 
Sexless,

KUOLEWA NA CHEO HAVINA UHUSIANO NA KUTOOLEWA, ILA TABIA INAYOENDANA NA MAJIVUNO YA CHEO NA UWEZO NI SUMU KUBWA KWA MAHUSIANO, UKIWA MNYNYEKEVU HATA KAMA WEWE NI TRUMP UTAPENDWA, YOU LIVE WITH YOUR PROBLEM IN YOUR HEART AND PERSONALITY AND SIO CHEO!
 
Avatar is not my true life jamani. Nilipenda kuweka baada ya sera za JPM. Kabla ya hapo nilikuwa na avatar ya ugly man mwenye mapengo.
 
Back
Top Bottom