Jimbo la uchaguzi la Mpwapwa tunatia aibu, Tangu lianzishwe tulibahatisha kupata mbunge mmoja tu Ali Mtaki, baada ya hapo tunapiga washout tu mala zote, mbaya kuliko zote ni kumweka siku nyingi mbunge wa sasa Lubeleje.
Mbunge huyu Lubeleje hajui kabasa job description za mbunge yeye hufikiri ubunge ni kuuliza maswali tu na kurudi jimboni kuanza kununulia watu ujugu.
Sasa tunatalajia kupata mbunge ambaye anaweza kuwapiku wabunge wote waliopita huyu Mama June Fussi sasa tunaona anafaa kuwa mbunge wetu kwa kipindi hiki cha sasa ambacho mapambano bungeni ni makali sana.
June Fussi ana uwezo wa kuwa msumbufu kwa makatibu wakuu wa wizara ambao ndio wenye mafungu hasa kipindi hiki baada ya mnvua njingi madaraja mengi yamekatika kwa hiyo mtifuano wa kutaka yajengwe bunge lijalo utakuwa ni mkubwa sana, June Fussi ana uwezo wa kuhimili mpambano huo hatuna shaka naye kabisa.
Juni Fussi ni mfanyakazi mwandamizi serikali ana uzoefu wote wa kujua serikali inafanyaje kazi pia ni mkazi wa Mpwapwa eneo la Mwanakianga kwa hiyo matatizo ya Mpwapwa anayajua vilivyo ni mpamabanaji mzoefu kwani katika ajira serikalini kaanzia kama Afisa UGANI ngazi ya kata hadi kuwa mwandamizi katika wizara ya Mifugo na Uvuzi masuala ya utafiti mwenye elimu ya Masters Degree, hakika wana jimbo la Mpwapwa tukimchagua June Fussi tutakuwa tumelemba dume.
Safari hii tusifanye makosa ya kuchagua wanaume tena tuchague mwanamke ambae atakomaa na matatizo yetu.
Niliwahi kufanya kazi mpwapwa miaka 4 sasa niko Dodoma mjini
Kuna changamoto nyingine naona umezisahau. Mpwapwa kuna kituo cha afya kimoja tu kinachohuduimia kata 15 wakati upande wa pili kwa bwana Simbachawene kuna vituo vya afya 3 (hii ni walaya moja)
Bado kwa kiasi kikubwa hawana maji safi na salama
Kuna maeneno makubwa bado hayana umeme
Kuna changamoto za elimu - Yapo matatizo makubwa ya watoto wa kike kupewa mimba na kushindwa kuendelea na elimu (mpwapwa inaongoza kwa dodoma
Makusanyo ya kodi ya kodi mpwapwa bado yako chini sana linganisha na majimbo mengine
Wilaya ya Kongwa ni mtoto wa Mpwapwa lakini wao wana barabara, Vituo vingi vya Afya, Maji safi na salama, na wana rank nzuri kielimu
Wilaya ya mpwapwa ni kongwe sana lakini maendeleo yake ni duni na kwasababu kila wakati wa uchaguzi wilaya hiyo hukosa umakini wa kuchagua au hukosa wagombea bora
Kama kweli huyo mama anazo sifa hizo ulizo zitaja nadhani huu ni wakati sahihi kwa mpwapwa kufanya mabadiliko makubwa na kubadili mwelekeo
Chagueni mwanamke kwa mara ya kwanza katika historia ya mpwapwa
Chagueni mwanamke kama kondoa
Chagueni huyo mama msomi mwenye uzoefu serikalini aende akapambane na wenzake serikalni kuwaletea mabadiliko
Badilisheni upepo mpwapwa fanyeni mabadiliko
Mjipange vizuri
Kila la Khery