Uchaguzi 2020 Ubunge jimbo la Mpwapwa 2020-25 twende na JUNE FUSSI tu

Nampata vizuri, nmefanya nae muziki miaka ya 2000. Yupo chama gan
Yupo jamaa fulani hivi miaka ya nyuma alikuwa PATUU na kina Dr. Ishengoma ametembea sana maeneo mbalimbali ya wilaya ya mpwapwa na ni mtu msikivu Sana. Anajihusisha na shida za watu na kurahisisha utatuzi wa changamoto nyingi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujue unamharibia
 

Mkuu kugombea jimbo moja na kwenda jimbo lingine sioni kama ni tatizo.

Nakumbuka Mrema amewahi kua mbunge wa Temeke na Vunjo
Waitara ndio huyo anatoka Ukonga anaenda Mara

Nadhani hoja ya msingi ni je huyo Fusi nayo elimu, uzoefu na umakini wakuweza kusaidia watu wa Mpwapwa. Majimbo ya Dodoma vijijini yana challenge tofauti na yanahitaji watu wenye uzoefu mkubwa, umakini, weledi na uzoefu wa kudeal na serikali

Kama huyu mama mnasema ana Masterz na amekua ofisa mwandamizi serikalini kwa miaka mingi nadhani atawasaidia zaidi wana mpwawa kuliko huyu kikongwe Lubeleje au huyu bwana mdogo Mtoro Nyange. Huyu Mtoro Nyange yuko hapo Kigamboni ni bwana mdogo sana. hana uzoefu, umakini na weledi

Kueni makini msifanye mihemko kwenye mambo ya serious. Kumuondoa kikongwe na kumleta mtoto nisawa na kutia maji kwenye gunia

Mpeni huyo mama atawavusha kwakua sifa zake ni kama zile za Ndugai na Simbachewene. Mtazamo wangu
 
Tutamchagua Ngoi Edward Limu ambaye ni mtu mwenye Kariba ya kuongoza umma wa watanzania wote hivyo tunaanza na kumpa Jimbo la Mpwapwa. Huyo Pusi sijui Ufuzi sijui Fusi akajipange huko vichakani

Mtakosea sana kuchagua vijana wadogo wakuja kujifunzia siasa jimboni kwenu. Hilo jimbo sio kichwa cha mwenda wazimu cha vijana wadogo na watoto kuja kujifunzia kazi

again kuweni makini acheni mihemko na ushabiki kwenye mambo serious

Chagueni mtu mwenye uzoefu sawa na Simbachawene au Ndugai. Huyo mama atawafaa zaidi kuliko hao watoto au huyo kikongwe Lubeleje
 


Niliwahi kufanya kazi mpwapwa miaka 4 sasa niko Dodoma mjini

Kuna changamoto nyingine naona umezisahau. Mpwapwa kuna kituo cha afya kimoja tu kinachohuduimia kata 15 wakati upande wa pili kwa bwana Simbachawene kuna vituo vya afya 3 (hii ni walaya moja)

Bado kwa kiasi kikubwa hawana maji safi na salama

Kuna maeneno makubwa bado hayana umeme

Kuna changamoto za elimu - Yapo matatizo makubwa ya watoto wa kike kupewa mimba na kushindwa kuendelea na elimu (mpwapwa inaongoza kwa dodoma

Makusanyo ya kodi ya kodi mpwapwa bado yako chini sana linganisha na majimbo mengine

Wilaya ya Kongwa ni mtoto wa Mpwapwa lakini wao wana barabara, Vituo vingi vya Afya, Maji safi na salama, na wana rank nzuri kielimu

Wilaya ya mpwapwa ni kongwe sana lakini maendeleo yake ni duni na kwasababu kila wakati wa uchaguzi wilaya hiyo hukosa umakini wa kuchagua au hukosa wagombea bora

Kama kweli huyo mama anazo sifa hizo ulizo zitaja nadhani huu ni wakati sahihi kwa mpwapwa kufanya mabadiliko makubwa na kubadili mwelekeo

Chagueni mwanamke kwa mara ya kwanza katika historia ya mpwapwa
Chagueni mwanamke kama kondoa
Chagueni huyo mama msomi mwenye uzoefu serikalini aende akapambane na wenzake serikalni kuwaletea mabadiliko

Badilisheni upepo mpwapwa fanyeni mabadiliko
Mjipange vizuri

Kila la Khery
 
Poleni pambaneni na halizenu ila wewe Ngeanakilala mnaa sana si ajabu ndiyo huyo mama kikongwe
 

Msichague vijana kwenye majimbo makongwe kama mpwapwa yenye changamoto nyingi sana

si mnaona wenzenu wa Kongwa (Ndugai) na Kibakwe (Simbachawene) wanavyo faidi kwasababu wamechagua watu wenye uzoefu serikalini. Sasa hao vijana wote mnaowataja ni amateurs. Tafuteni msomi makini, mwenye uzoefu serikalini na elimu kubwa. Anaweza kupata hata unaibu waziri akawakomboa.

Msiwape amatures jimbo wajifunzie kazi mtaendelea kupiga mark time na kulia lia
 
Kaa kimya kwa muda maana kampeni bado labda kama unataka kumharibia
 
Maeneo mengi ya watu wa maisha ya chini ni wapiga kura wa chama tawala hata uwaeleze vipi hawakuelewi, ila uchaguzi ukipita wanaanza kelele maji, njaa, michango mingi Mara kodi tunatozwa sana, utasikia Polisi wanatuonea
 
Sijafurahishwa na post yako:
1. Official campaigns hazijaruhusiwa.
2.watumishi wa umma hawaruhusiwi.
3.kama hujatumwa kumuangamiza shangazi yangu futa post hii
 
Niliwahi kufanya kazi mpwapwa miaka 4 Wilaya ya Kongwa ni mtoto wa Mpwapwa lakini wao wana barabara, Vituo vingi vya Afya, Maji safi na salama, na wana rank nzuri kielimu
Badilisheni upepo mpwapwa fanyeni mabadiliko
Mjipange vizuri
Kila la Khery
Duh, kumbe sasa Kongwa mambo safi?. Angalau uspka unalipa, ila pia kwa maendeleo ya jimbo la Kongwa, JF nayo, imesaidia saidia, mabandiko kama Haya yamesaidia katika amsha amsha

Kwa Wale Mliowahi Kufika Kongwa, ni Jimbo Choka Mbaya Kiasi Kwamba Mbunge Wake Hafai Kwa Lolote!. - JamiiForums

P
 
JUNE FUSSI nadhani ni busara ukagombee kwenu Songea ambako shida walizonazo wananchi wako huko utakuwa unazijua vizuri zaidi kuliko huko ugenini. Ni ushauri tu.
 
JUNE FUSSI nadhani ni busara ukagombee kwenu Songea ambako shida walizonazo wananchi wako huko utakuwa unazijua vizuri zaidi kuliko huko ugenini. Ni ushauri tu.
Aliyekudanganya kuwa kwao ni songea ni nani?., kwake ni mpwapwa. Period
 
Hao vijana ni lini wameonyesha nia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…