Uchaguzi 2020 Ubunge Kigoma Mjini, Zitto Kabwe vs Diamond Platnumz

Uchaguzi 2020 Ubunge Kigoma Mjini, Zitto Kabwe vs Diamond Platnumz

Unachagua kiuno unaacha akili? Halafu mnamlaumu Mungu kwa waafrika kuwa na mataifa ya kijinga!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata diamond ana akili anazo ndomaana kigoma wanamkubali Sana ukiachana nakupenda mziki wake anawasaidia Sana teyali ameshawajengea visima viwili, pia kachangia ujenzi wa mahabara pamoja ujenzi wa hospital.
 
Nimedokezwa na wadau hapa Kigoma ya kwamba wazee wanamtaka Diamond agombee.nafasi ya ubunge hapo kigoma mjini badala ya Zitto Kabwe.

Wanadai Zitto kawatelekeza, kahamishia harakati zake twitter na ndani ya jiji la Dar badala ya kuhudumia wanakigoma.

Magwiji hao wa siasa kigoma wanamtaka Diamond awe mgombea wao kupitia chama cha mapinduzi ,wana imani atawawakilisha Barbara,

Kama ni kweli huu ndio mwisho wa ndugu yetu Zitto aliehamishia majukumu yake Twitter.

Kila la kheri Diamond katika.utumishi wako wa ubunge, hakuna wa kukuzuia

Sent using Jamii Forums mobile app
uzi wa kijinga sana ktk mwaka huu mpya
 
Abood na Mo walikuwa wanataka ubunge kwa ajili ya faida ya biashara zao.Ukiwa mbunge unaweza kutumia cheo chako usilipe Kodi pia kusafeguard biashara zako sasa DIAMOND PLATNUMZ atafute ubunge kwa kipi? Kama umaarufu anao mkubwa Sana Kama pesa anayo pesa nyingi mpaka wakati mwingine anatumia kutoa misaada kwa watu tumeona kigoma kutengeneza visima viwili, kachsngia madawati 600 tandale,katoa bima za afya kwa wamama 40, katoa bajaji 45 kwa walemavu n.k hakuna sababu za msingi zitakazomfanya DIAMOND PLATNUMZ agombee ubunge naona kabisa mtoa mada ametulisha matango pori.

Bila ya shaka yawezekana kuwa una matatizo ya akili wewe
 
Kama kuna tume huru atapigwa mpaka ashangae...atashangaa sema wewe admn umeleta kishabiki sana unajitekenya wewe mwenyewe unacheka.
 
Lowassa alikua na pesa nyingi ,na alikua waziri mkuu lakini hakuridhika altaka kiti cha enzi (Urais ),kwanini asingetulia tu?

Bill Gate wa America na utajiri wote bado anasaka pesa,kwanini asingetulia tu kwa sababu anapesa ya kutumia mpaka anakufa.
Hakuna mwanadamu anayeridhika hapa duniani
Abood na Mo walikuwa wanataka ubunge kwa ajili ya faida ya biashara zao.Ukiwa mbunge unaweza kutumia cheo chako usilipe Kodi pia kusafeguard biashara zako sasa DIAMOND PLATNUMZ atafute ubunge kwa kipi? Kama umaarufu anao mkubwa Sana Kama pesa anayo pesa nyingi mpaka wakati mwingine anatumia kutoa misaada kwa watu tumeona kigoma kutengeneza visima viwili, kachsngia madawati 600 tandale,katoa bima za afya kwa wamama 40, katoa bajaji 45 kwa walemavu n.k hakuna sababu za msingi zitakazomfanya DIAMOND PLATNUMZ agombee ubunge naona kabisa mtoa mada ametulisha matango pori.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuulize wana Kgm. Kwa sasa zitto hana mvuto tena kwa wanakigoma. Hali iliyomtokea Kgm kaskazini hadi aka switch na serukamba ndio iliyopo mjini kwa sasa. Ujio wa Diamond Kigoma hata baba levo atamkimbia zitto.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nimezaliwa Kigoma mjini , hospital ya mkoa maweni ....

Watu pekee wanaojielewa kigoma ni kutoka ujiji Basi ... Maeneo mengine yote Ni watu hawajielewi Kama wewe. Ni kichaa pekee ndio anaweza kutokutambua juhudi za zitto kabwe kwenye mkoa wa kigoma...

Ni zitto ndio alipigania suala la uraia kwa wakazi wa kigoma , hapo awali watu wa kigoma walikuwa hawaishi kubambikiziwa kesi za uraia ... Zitto ndio kafanikisha barabara zote za kuunga mkoa wa kigoma , kuanzia barabara ya tabora na Daraja la kikwete ambae alikuwa swahiba wake... Ni zitto ndio alimshawishi ramadhani dau kupeleka mradi wa nssf kigoma ...

Ni chini ya zitto kabwe imepatikana barabara ya kigoma mpaka Burundi kupitia bitale.. hapo awali ilikuwa ni vumbi tupu.

Sitaki kuzungumzia maendeleo ambayo maendeleo ambayo ameyaleta Jimbo la kigoma mjini kipindi Cha miaka yake mitano ... Tangu kupata Uhuru Barabara ya airport ilikuwa haina lami .. Kwasasa ipo....

Bypass way ya kuanzia pale gungu kupitia nyuma ya masanga iko Safi tangu Uhuru. Hapa sijazungumzia barabara za ndani ya Jimbo ... Almost ujiji yote imejaa lami ... Haya mambo yote kuanzia 2010 kurudi nyuma kigoma mjini ilikuwa Kama pori.

Zitto ana mapungufu yake sikatai ila ni moja ya viongozi Bora kabisa tangu nchi hii kupata Uhuru , Nasikitika amekuwa Kiongozi kwenye nchi na raia baadhi wasioeleweka na hawana elimu ya uraia.

Leo ukienda majimbo yote hapo mkoa wa kigoma Hakuna Jimbo hata moja ambalo limepiga hatua Kama Jimbo la zitto kabwe Licha ya hayo majimbo kuwa chini ya ccm.. tembelea kakonko, uvinza, kibondo, na majimbo yote ya kasulu ni aibu tupu...

Ni siasa Tu za bongo zimekaa kutuchuma wananchi na wanajipatia nafasi kwa raia wasio na akili ... Diamond hana uwezo wa kuwa Kiongozi wa kigoma ... Miaka yake yote ya usupastaa wake hajawahi kufanya lolote la maana kigoma (Kama lipo andika hapa)... Ni juzi ndio katoa msaada wa msikiti...

Mimi ni raia wa kigoma mjini , huwa sipendi kujichangamanisha na raia wengine wa hizo wilaya zingine wasiojielewa , kwasababu kigoma mjini ndio chimbuko la mabadiriko miaka na miaka hususani ujiji (My home town).. Sehemu yenye watu wanaojielewa tangu na tangu na sio waha waliojaa ujinga kichwani na ushamba ....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nchi Tunakoelekea Sio yaani

Zitto Zuberi Kabwe unamlinganisha na Naseeb Abdul a.k.a Diamond

Halafu anakuja mtu why hatuendelei... Huyo Diamond anaweza akawa ni mzuri kimuziki ila hana ubora wowote kisiasa. Hajafikia hata robo ya nguvu zake kisiasa kwa Bobi Wine wa pale Uganda achilia mbali Prof Jay au Mr 2 ...

Hawa ndio wasanii wenye Hilba ya Uongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Abood na Mo walikuwa wanataka ubunge kwa ajili ya faida ya biashara zao.Ukiwa mbunge unaweza kutumia cheo chako usilipe Kodi pia kusafeguard biashara zako sasa DIAMOND PLATNUMZ atafute ubunge kwa kipi? Kama umaarufu anao mkubwa Sana Kama pesa anayo pesa nyingi mpaka wakati mwingine anatumia kutoa misaada kwa watu tumeona kigoma kutengeneza visima viwili, kachsngia madawati 600 tandale,katoa bima za afya kwa wamama 40, katoa bajaji 45 kwa walemavu n.k hakuna sababu za msingi zitakazomfanya DIAMOND PLATNUMZ agombee ubunge naona kabisa mtoa mada ametulisha matango pori.
Kwahiyo wewe kwa akili yako unadhani Hakuna mtu kigoma anaweza kutoa hivyo ulivyotaja... Au tukuwekee hapa mambo ambayo wamefanya watu hao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diamond siasa zitamporomosha!

Anaotaka kuwanufaisha kisiasa kwa kutumia umaarufu wake ni watu wasiokubalika na Watanzania wengi hivyo awe makini
Kwanza Diamond hana Uwezo wa Kujenga hoja kisiasa
 
Hii nchi Tunakoelekea Sio yaani

Zitto Zuberi Kabwe unamlinganisha na Naseeb Abdul a.k.a Diamond

Halafu anakuja mtu why hatuendelei... Huyo Diamond anaweza akawa ni mzuri kimuziki ila hana ubora wowote kisiasa. Hajafikia hata robo ya nguvu zake kisiasa kwa Bobi Wine wa pale Uganda achilia mbali Prof Jay au Mr 2 ...

Hawa ndio wasanii wenye Hilba ya Uongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umesema kabisa kwanza Prof na Sugu wana Exposure kubwa sana ya mambo ya kiutawala siyo Diamond
 
Tanzania wahinga ni wengi.
Sifa ya mtu kuwa mbunge ni umaarufu na kuvua nguo mbele ya watu?

Congo iliharibika iliporuhusu kuongizwa na wakata viuno na kuacha na kizazi cha wasomi na watu waliotaka kuifikisha Congo mbali.

Tanzania nayo inakwenda kwenye mkondo uleule,tutakuja kutawaliwa na Rwanda kma wanavyotawala Congo halafu hatutaweza kujitetea.

Unaanzaje kulinganisha akili na ujinga, zitto na Diamond na bado ukajiona unaakili timamu?

Kama hutaki Mbunge aina ya Zitto,Mnyika uwe na mbunge kama Diamond,Ambaer Rutty,Shilole,Harmonize wasanii?

Hilo litakuwa Bunge Kweli? Au itakuwa genge la wavuta Bange na walevi?

Acha utaahira,watu wa Kigoma wanampenda Diamond kwenye Burudani lkn sio kuwa kiongozi wao wa Kisiasa.
 
Hill linafahamika Ni mpango Wa ccm, ila akiingia kwenye siasa atajimaliza
 
Back
Top Bottom