Uchaguzi 2020 Ubunge Tarime Mjini: Ngicho ahamishia nguvu zake kwa Gerald Martin

Kiukweli Kama tunataka viongozi wenye uchungu na Tarime wasiangalie aliyetoa pesa.
 
Haya Majungu ya kishamba tena kijinga jinga zaidi ya yale ya Kigamboni kawe na sehemu zingine CCM walipotoa Rushwa wote, watia nia wagombea wote wa CCM wametoa Rushwa kila kona ya Tanzania ingawa Rushwa zilitofautiana kulingana na mgombea mwenyewe, cha ajabu wale waliofeli wakishindwa kwenye kura za maoni wamekuwa na wivu mkubwa kwa washindi kama ilivyokuwa Arusha mpaka kurekodi video wakitoa tuhuma za Rushwa zisizo na ushahidi wa Takukuru live, CCM wote wametoa Rushwa lakini CCM wengi hawakukamatwa live na Rushwa, wale wenye wivu na roho mbaya wameamua kuwarubuni Takukuru na vyombo vingine wawaandikie report mbaya washindi wa kura za maoni wapate kuwaengua wakose wote, Mfumo wa kijinga mfumo uliopitwa na wakati, CCM nendeni na style mpya ya kuwapata wagombea ubunge acheni Mbinu za kuja kuchuja majina Dodoma mnalea mnakarisha uongo fitna Majungu makubwa.
 
ni kweli Tarime imekuwa shamba la bibi kwa muda mrefu, bora walete hata wa mwisho ambaye hakutoa rushwa ila ana uwezo wa kushinda.
CCM wote wametoa Rushwa asikutanganye mtu tena wale wa mwisho pesa zao huwauma pindi zikiliwa na wajumbe kisha kuambulia patupu wanakuwa vinara wa Majungu kuwakomoa washindi ni wivu umetawala kura za maoni CCM
 
Ni kweli hizo tuhuma zipo, Chadema walipambana kutoa pesa ili mgombea anayepita CCM awe ambaye wataweza kumgaragaza kwa urahisi.
CCM nao wametoa pesa nyalandu awe mgombea wa Urais kwa chadema ili magufuli arejee ikulu bila hata ya kufanya kampeni
 
Tabia za fisi kula fisi...inasikitisha!
Mleta mada wenzako huacha namba za simu!

Anyways tuwaache wafu wazikane.

Everyday is Saturday........................... 😎
Mleta mada hawezi kuweka namba za simu anajua kuwa amepika Majungu ambayo yakibainika yatamgharimu
 
Tuhuma za Rushwa ikithibitika pasipo shaka huyo waitara atafyekwa Dodoma, cha muhimu ni ushahidi sahihi na kweli usiwe ushahidi wa kutengeneza kimajungu jungu.
 
Nashauri Tarime Mjini tuweke Mgombea makini wa kupambana na Mbunge anayemaliza muda wake vinginevyo tunaweza kupoteza Tena Jimbo hili.
 
Kikubwa tujitahidi CCM ishinde maana Upinzani bado una nguvu Sana hapa Tarime na hivi vijana maisha magumu wasije wakapiga kura kutukomoa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…