Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
JKT kuna mtu wa Musoma mmoja alizoea kusema kura nimekura pa kurara je? Musoma wana r tatizo ni kwenye l.

Kweli mkuu

Mimi hua sijui wapi niweke L ama R hua najiuliza sijui ni tatizo gani linasumbua na kwanini iwe hivyo?
 
Mbowe,Lunyungu,DK.slaa,Mvungi,zitto,mrema....na mkuu wa wilaya anajua hali halisi ziaidi ya siasa morali waliuyo nayo watu wa uku..uku kuna msema wanaume hawapigwi wote jamani...

Nadhani neno unalotafuta hapa ni huku

Mtu asiye na kovu si mwanaume...lazima uwe na alama flani ya kukatwa ajari...kuonyesha umepitia hard time....mtu kwenda jela ni sifa...sasa wakati wa uchaguzi kuwaacha bila kuwa na hata picha ya askari...unataka kutengeneza nini...?

Huu ni uongo uliokithiri na upuuzi wa hali ya juu. Tafadhali sana Busweli acha utoto huu na ujiheshimu na uwaheshimu watu wa Tarime. Mimi na watu zaidi ya maelfu wa Tarime hatuna makovu na hatujivunii kwenda jela, hao wewe unaowasema hapa ni kina nani?

Mie naunga mkono askari kuwepo hapa kwa kulinda usalama hasa wakati huu wa uchaguzi....mabasi yote yatokayo nje ya tarime stand kuu ni tarime,si kila mtu anataka kupiga kula bwana...sasa kama zogo litazuka stand polisi hawapo..na unataka kwenda mwanza,sirari,kenya...si utakuwa victim...?

Kwanza uku hakuna anaye ongelea polisi hata kidogo ni sie kwenye mtandao....watu wanaongelea CCM kushidwa tu...hatakwa kuweka gogo...lipigiwe kula..kwa mwenye kupambanua..unawe jua ni nini hawa watu wako tiyari kufanya.

Ingekuwa usukumani wangesema doho tabu...tokwicha... wanaachana na uchaguzi.

Good day

Hii hatari tupu.... Tanzania kuna watu wa aina mbalimbali... huu unaoweka hapa ni mfano wa ajabu sana kwa jamii mpya inayojengeka Tanzania.

Aibu tupu.
 
Acha jazba Magabe kibiti...una rafiki zako lakini wewe binafsi hujawahi fika uku au kwa maneno mengine.....hujakaa muda mrefu uku..ongea vizuri na watu wa uku...ona wenzio hawajajibu swala hili kama lunyungu na wengine...wanajua this is true..

Ukija Maeneo haya unaweza futa kauli zako...njoo uku ongea na watu sema nao taratibu utaweza pata ukweli...in fact mie ni wa uku uku...na ni moja ya wanao pigana lakini kwa njia moja au nyingine sikubaliani nao..get that to ur mind.

Hoja iliyo mbele yetu ni kwanini Tossi,Suleimani kova waje wakati huu...wa uchaguzi..kwa kisingizio cha kisiasa ambayo kila mtu aliye changia ame support kuwa ni makosa...lakini mie upande wangu ni kuwa hawa watu bila polisi hawaendi jamani...au historia ilikupita kushoto magabe soma vyema utajua walikuwa wanatumika kama nini wakati huo.

Kwa kweli polisi ni lazima ikishindikana walete jeshi kabisa..anaye bisha aje wakati wa uchaguzi...mie nshaomba off....wiki nzima wakati wa uchaguzi...nini bana uchaguzi na siraha....wewe magabe njoo field uone mambo wewe unaongela dar....

Watu wana pata hard time ..... uku huwezi amini kwanza ume skip mambo mengi sana niliyo ongelea hapo...kama waziri mkuu ana kuja na wanamzomea...harafu msaada wa kujenga hospitali yao wenyewe...waziri anaondoka nao...nani mwenye faida?kulikuwa na mifuko 300 ya cement...lakini haikutolewa kwa ajiri ya jazba na kiburi cha wananchi wa hapa....

Sasa mgojwa aliye chomwa kisu tumboni nyamongo inabidi apelekwe Tarime ni mwendo wa saa moja au dakika 45 kwa mchomoko(mark two..ina beba watu 12)...ukiwa na land cruser ni danikia 35 tu..kwa njia ya juu..nyamwaga.

kama wangekubali kuongezewa miundo mbinu na waziri mkuu..leo hii tusinge kuwa na adha ya kupeleka wagojwa tarime...wakafia(passaway) kimakorere....

Upo kaka magabe
 
Wakati mwingine mambo ya kipuuzi kama haya inabidi yakemewe kabisa hapa JF na kwingine kokote. Hii generalization na dharau dhidi ya watu wa Tarime imezidi sana hapa JF na kwenye vyombo vya habari.

Wewe Buswelu acha upuuzi na ujinga wa kusema kuwa watu wa Tarime asili yao ni ugomvi. Mimi nimezaliwa na kukulia Tarime na sijawahi kuona hayo ya ugomvi wa asili na uvivu kama unaotaka kuuweka hapa.

Ukome kabisa kutumia lugha chafu dhidi ya watu wa Tarime. Kusema kuwa wao wangekuwa wasukuma kusingekuwa na mapigano ni upuuzi mkubwa sana na unaofaa kukemewa kwa nguvu zote.

Yanayoendelea Tarime yanajulikana kwa wanatarime na namna migogoro ya kipuuuzi inavyoletwa na kukukuzwa na vyombo vya usalama na vya habari ili kuwatoa watu kwenye the main issue ya Tarime - deposit kubwa kabisa ya dhahabu ambayo bado haijaanza kuchimbwa.

Hao polisi wanachofanya kinajulikana na watu wa Tarime wanawaangalia tu kwa mshangao. Mimi ningewashauri wa usalama kuwa makini na wastaarabu sana dhidi ya watu wa Tarime au watanzania wowote kokote kule Tanzania. Haya mambo ya kipuuzi na generalization za kizembe kama hizi hazitapelekea kusolve matatizo ya watu wa Tarime au watanzania ambao wanaendelea kuwa masikini kila kukicha.

Nimetumia lugha kali kwa makusudi ili kukemea upuuzi na maneno yako yenye vijembe dhidi ya watu wa Tarime kwako Busweli. Natumaini utaacha upuuuzi huu na kuanza kuheshimu watu wa Tarime ambao wengi wao ni wastaarabu na watu wasiopenda fujo.

Asante

Hapana bwana magabe kibiti wewe ni moja kati ya watu ninao wasemea hapa....ukweli ni tatizo kuu....nani ambaye hakusoma habari ya yule baba mkwe ambaye alimkata masikio mkwewe(mwanamke) kisa kauziwa na mkwe mwenzie(baba wa mwanamke)...kama nasema uongo(NIPASHE), in fact nilikuwa sehemu ya tukio.....i have been herE more than 3years...kubali ukweli kuwa lazima mbadilike ili kuwe na maendeleo kila mapigano ya kikabili nyie tu jamani....mkiambiwa ukweli ohh wapuuzi wala hujatumia lugha kali ni ya kawaida tu......wewe ni moja ya walio kimbia nyumbani....kama kina warioba na wa wenzie....njoo muone na msaidiE nyumbani....mie niko uku ndio maaana nasema hivi....njoo tushirikiane tumalize hili tatizo...ni PM kama huamini....

Am out
 
Hoja iliyo mbele yetu ni kwanini Tossi,Suleimani kova waje wakati huu...wa uchaguzi..kwa kisingizio cha kisiasa ambayo kila mtu aliye changia ame support kuwa ni makosa...lakini mie upande wangu ni kuwa hawa watu bila polisi hawaendi jamani...au historia ilikupita kushoto magabe soma vyema utajua walikuwa wanatumika kama nini wakati huo.

Buswelu acha kudanganya watu,halafu uache dharau yako hiyo ya kijinga.
manake nyie watu msiokuwa wazawa wa huku mnajifanya mnawafahamu sana wakurya.Hapa unataka kuongelea historia gani!?huwezi kuijua historia yetu kuliko sisi wenyewe, huo ni uongo uliokomaa, kwasababu tunawajua watu wa ccm ni kawaida yenu kudanganya na kuhadaa watu.Nyeupe mmezoea kudanganya watu kuwa ni nyekundu!
kama watu wa tarime bila polisi hawaendi hiyo miaka yote mbona huyo kova,tossi na hao askari 300 hawajawahi kuwepo na chaguzi zimekuwa zikifanyika?Kwa mara ya kwanza watu wamefariki tarime kutokana na vurugu za uchaguzi mwaka 2005, na hiyo ni baada ya ccm kuona kwamba wanashindwa,walikuwa wakiitisha mikutano ya kampeni inakosa wasikilizaji wakaamua kuanzisha mkakati wa kuwashambulia chadema kitu kilichopelekea vifo vya wananchi.
Wewe hata hiyo historia unayotaka 'kutufundisha' wakati hujui kuwa katika majimbo yote yenye mlengo tofauti na ccm lazima polisi wapelekwe kwa wingi kwa visingizio visivyokuwa na kichwa wala miguu.Pemba kwa mfano nako wanaishi wakurya?Manake kila uchaguzi polisi, wanajeshi n.k wanjazwa huko.
Au kiteto napo kuna wakurya?au historia unayoijua haikukumbushi jinsi wafuasi wa ccm walivyowashambulia viongozi wa chadema!?
Historia hiyo hiyo inatuonyesha jinsi polisi ilivyowashambulia na kuwazuia kuendesha mikutano ya kampeni, wafuasi wa aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo la musoma mjini kwa tiketi ya cuf, bw.mustafa wandwi mwaka 2000&2005,wewe unaijua historia gani?
ninayo mifano mingi sana ya kukufundisha hiyo historia unayotaka kutudanganya kwamba unaijua
.
 
Wewe ulitaka waje wakati gani?? na kwanini huhoji hayo makabila kwanini yamepigana wakati huu?
 
Hili swala la ubunge naona linakuwa so personal kwa sasa badala ya kushambulia hoja naona watu wanaanza kushambuliana ingekuwa bora hata kama mtu kakosea arekebishwe kidogo kuliko kulumbana post nzima, nani anajua - nani hajui kinachoendelea inakuwa personal zaidi na inaondoa muelekeo wa hoja nzima ya kinachoendelea na hali halisi ya mjadala huu inapotea.
 
Wewe ulitaka waje wakati gani?? na kwanini huhoji hayo makabila kwanini yamepigana wakati huu?

Mbona unakurupuka ndugu yangu.
soma vizuri maelezo yangu.na isitoshe unaonekana huijui tarime unasimuliwa tu!ndio sababu unachojua ni kwamba wanapigana sasahivi!!
yaani wewe siku zote hizo vyombo vya habari vinatangaza mapigano ya tarime hujawahi kuyasikia?hadi mwanamuziki mmoja wa bongo fleva ameweka mstari wa anchari na anchoka kwenye wimbo wake lakini wewe unayejiona mjuaji hilo limekupita kushoto?
kujibu swali lako, mimi nilitaka waje from the first day mapigano yalipoanza.
wakati wote marehemu wangwe akiitaka serikali kuimarisha ulinzi tarime na kukomesha mapigano ya kikabila ndo nilitaka waje.
na hata hivyo kwanini wamekuja kujazana mjini tarime ambako hakuna ugomvi badala ya kwenda vijijini kwenye ugomvi?
why??? kwaninini????
 
Kwa hiyo wewe FALSAFA yako unataka kutuambia KUSHINDWA CCM ktk jimbo hilo ni VYEMA kuliko kuokoa uhai wabinadamu,kwa namna nyingine uanataka kusema POLISI waogope kupambana na mapigano eti kwa vile CHADEMA,CUF watalalama??

wewe hujui kabisa unaweza ugua gonjwa zaidi ya miaka 5 ama mingi na akupona LAKINI ukafa siku nyingine tena kwa kujikwaa du na kuanguka?? Hivi utauliza kwanini hukufa wakati ule ulipoumwa mda mrefu na kwanini ufe kwa kujikwaa ?? Kaangalie upya falsafa yako.
 
Mimi naona bora yatokee mapigano na sio kunyukuana nyukuana ,yatokee kikweli kweli aidha polisi V/S wananchi au Upinzani V/S CCM , yaani zipigwe kikweli kweli ,ili dunia itupie macho utawala wa Muungwana na udikteta unaoanza kuota kama magugu.
Ila sidhani kama Wananchi wa huko wanaweza kustand na polisi kama wa kule Pemba ambako rekodi za ndani zinaonyesha vituo kadhaa vya polisi Pemba vilidhibitiwa kwa muda na polisi wengi tu kuchinjwa kama kuku ,polisi wenyewe wanalijua hilo japo wanaona ni siri lakini ukweli ,polisi walipewa kisago cha mbwa koko ,na ndio maana hadi hii leo bado hasira zao kwa waPemba hazijaisha lakini palipofikiwa ni kuheshimiana na ndipo walipo kati ya polisi na wananchi wa Pemba ambao naweza kusema ni wanaume wa shoka waliojitolea muhanga kupinga polisi kutumika kama chombo cha CCM na kutekeleza mikakati ya CCM.
Walichoamua waPemba ni kuichanganya Polisi na CCM kama kitu kimoja hivyo majibu waliyoyapata polisi ni kuhesabiwa kama tawi la CCM na upinzani walioupata polisi ni sawa na upinzani unaoikumba CCM huko Pemba...........Je wabara mnaweza kuihesabu polisi kama chombo cha CCM na kupambana nancho kifo kwa kifo ?
 
msianze kutenganeza mazingira ili mkishindwa mpate kupiga kelele .mnaanza kutuandaa mtakaposhindwa mje na hoja za polisi.

Kama mnaona vipi wawakirishi ktk vituo vya kupigia kura wawekeni makomandoo wa chadema na wao baada ya matokeo watakua na copy za matokeo hivyo wakitoa matekeo siyo ,ninyi mtuletee facts hizo na si fact za ffu na polisi.
hovyo! ufumbuzi sio huo
 
Mimi naona bora yatokee mapigano na sio kunyukuana nyukuana ,yatokee kikweli kweli aidha polisi V/S wananchi au Upinzani V/S CCM , yaani zipigwe kikweli kweli ,ili dunia itupie macho utawala wa Muungwana na udikteta unaoanza kuota kama magugu...............

Walichoamua waPemba ni kuichanganya Polisi na CCM kama kitu kimoja hivyo majibu waliyoyapata polisi ni kuhesabiwa kama tawi la CCM na upinzani walioupata polisi ni sawa na upinzani unaoikumba CCM huko Pemba...........Je wabara mnaweza kuihesabu polisi kama chombo cha CCM na kupambana nancho kifo kwa kifo ?

Heshima mbele Mwiba!!...... Habari ndio hiyo. Tanzania imefikia pahali kama wabongo hatuta amua kutumia nguvu basi tusitegemee kupata haki yetu kwa kupitia kisanduku cha kura. Sio tu jeshi la Polisi lakini vilevile Tume ya uchaguzi ni part and parcel ya CCM. Wasimamizi wa vituo vya kura ni hao hao makada ya chama cha mafisadi.

Unatakiwa mkongoto wa hali ya juu hadi roho za watu ziondolewe. Unapombana mbwa koko kwenye kona na kumshambulia pasipo huruma akiona kipigo kinazidi atakung'ata tu ili atoke hapo. Akikuumiza huwezi kumlaumu kwani njia ya kusalimisha maisha yake ilibaki moja tu.

Hata kama wakurya wanaikataa kata kata CCM, bila mishale kutembea kama iliyokuwa mwaka 2005 kangoye atatangazwa mshindi tu hata kama sio chaguo lao. Msiwe naive, Kura haziibiwi siku ya uchaguzi. kuweka makomandoo kituoni kunasaidia lakini sio solution. Kura zinaibiwa mapema. Kiteto kadi za kupigia kura zilipanda bei siku moja kabla ya kupiga kura msekwa, mungai, makamba walikuwa wanazinunua kwa shilingi elfu 45. Tarime kuna watu wananjaa vilevile kadi zitauzwa mtindo mmoja.

Viongozi wa CCM wakishirikiana na serikali wanaiba kura kwa kuwatishia wananchi wenye uelewa mdogo. Hao wapo kila mahali na huwezi kukataa. Bila kuwajaza hofu hawa watawala wezi wataendelea na intimidation tactics zao. Dawa yao ni kuwachinja tu. CNN na Aljazeera wajazane pale ndipo uchaguzi utakuwa wa huru. Kwa kutegemea TBC1 na magazeti ya rostam hata boksi la kula likiibiwa mchana kweupe hatutajulishwa tutaambiwa mambo yote yalikuwa salama.
 
Sio kweli kupigana sio suluhu.
Marehemu Chacha alitanganzwa mshindi hakua wa CCM,kama mnaona kuna uelekeo huo ina maana mmshehisi kubwaga ndio maana mnatengeneza ngao mapema.
 
Ufumbuzi ni kupigia kelele polisi waondoke ili watu waendelee kuchapana mshile.Duuuuuu hiyo imetulia.

Mwana wasu,

wachamawe!!, tangu sasa badili jina lako tafadhali,

Mkama jina lako haliendani wa hapa nyumbani Mara,yaani unafanana na watu wa pwani mkuu.hebu kweli ni furaha gani uliyonayo hapa jamvini na sisi ndugu zako tunaumizwa na hawa CCM?

Tunajua ninyi ndugu zetu mlioko Dar, Arusha , Mbeya MNATUCHEKA SANA WANA MARA KWA KILE TUNACHOKIAMINI NDANI YA MIOYO YETU, sisi tunaamini kuwa CCM wameshindwa kuendesha nchii hii na hivyo tunaona kuwa sasa ni wakati wa kuwatosa.

Tunajua kuwa sisi kama wana Tarime hatuwezi kuleta mabadiliko kwa kiasi kikubwa ila tutakuwa CHACHU ya demokrasia hapa nchini, endeleeni kutuunga mkono na hakika tutafikia hilo lengo letu, acheni kutubeza na kutudharau.

Sisi wanatarime hatuoni shida hata kama Jeshi la police lote tz likaamia hapa sisi tu washindi watarijiwa na Mungu atusaidie.
 
Wala usiwe na shaka wakwetu,
Hiyo ya kumwaga FFU ni kawaida ya CCM wanapohisi uwezekano wa kupata ushindi ni mdogo sana.Wanajua kuwa tarime ni vigumu wao kupata ushindi kihalali, kwahiyo lazima watumie mabavu ili kujitangazia ushindi.
Lakini hakuna haja ya kukata tamaa, muhimu ni kuendelea kuhamasishana na hatimaye siku ya uchaguzi watu wajitokeze kwa wingi kumchagua mwakilishi atakayekuwa na jeuri ya kutetea maslahi ya wanatarime.Kuchagua ccm ni kuchagua kuzika maslahi ya wanatarime.Mbunge kutoka ccm hawezi kuwakilisha maslahi ya wananchi,atawakilisha maslahi ya ccm.Kwani katiba yao (ccm) haiwaruhusu kutetea maslahi ya nchi bali mafisadi!
Ukitetea maslahi ya nchi wanaku-NAPE!eti kwa utovu wa nidhamu!

Tata Mwita, Mbuya.

Sijajua kuwa nini hatima ya mkoa wetu, ila ninadhani kama tukiwa na mchakato wa kweli tutakafanya jitihada ili huu mkoa mzima ugeuke na kuwa fikra mbadala na hapo ndipo tunaweza kupata maendeleo ya kweli.

Mwita, Mtanzania wa kawaida hapa Mara ameanza kujitambua kabisa na si vinginevyo, kuna kipindi niliwahi kusema kuwa tumshinikize Mbowe ajiuzuru ili tumpate mtu mbadala atakaeweza kukiongoza chama hicho chenye sura ya kitaifa kwa sasa .

Mwita, vyama vya siasa kwa sasa hapa Tanzania havina nguvu kabisa, na ndiyo maana sisi wana Tarime tumeamua kuwa ni lazima tuuonyeshe umma wa kitanzania kuwa Demokrasia ya kweli ni lazima iwe na ghalama
 
Mwana wasu,

wachamawe!!, tangu sasa badili jina lako tafadhali,

Mkama jina lako haliendani wa hapa nyumbani Mara,yaani unafanana na watu wa pwani mkuu.hebu kweli ni furaha gani uliyonayo hapa jamvini na sisi ndugu zako tunaumizwa na hawa CCM?

Tunajua ninyi ndugu zetu mlioko Dar, Arusha , Mbeya MNATUCHEKA SANA WANA MARA KWA KILE TUNACHOKIAMINI NDANI YA MIOYO YETU, sisi tunaamini kuwa CCM wameshindwa kuendesha nchii hii na hivyo tunaona kuwa sasa ni wakati wa kuwatosa.

Tunajua kuwa sisi kama wana Tarime hatuwezi kuleta mabadiliko kwa kiasi kikubwa ila tutakuwa CHACHU ya demokrasia hapa nchini, endeleeni kutuunga mkono na hakika tutafikia hilo lengo letu, acheni kutubeza na kutudharau.

Sisi wanatarime hatuoni shida hata kama Jeshi la police lote tz likaamia hapa sisi tu washindi watarijiwa na Mungu atusaidie.

Mwanawasu
Ndg yangu tusema ukweli tu wala tusipindishe mambo ,wizi wa ng'ombe zetu wala hua CCM hawa utengenenzi.

Haya mapigano yetu yamekuwepo mara nyingi sana ila wakati wa nyuma habari ilikua haisambai kwa urahisi kutokana na technologia ya habari kua finyu na mapigano yaliyokua yanasikika ni yale yaliyopiganwa mda mrefu.

Lakini sasa imefika wakati lazima tukubali haya mapigano yatokomezwe kwanza ndio tutapiga kura zetu kwa utulivu.

Isitafasiriwe kua Mapigano haya ni kwa sababu sisi watu wa mara ni wakorofi hapana hiyo si kweli ILA ukiangalia MIPAKANI kote kule juu kwa KENYA mipakani mwa ethiopia na somalia kuna mapigano ya aina hii na hata ukiangalia kule juu mwa UGANDA napo ni hivyohivyo ,hii inatokana na kabila fulani kua na koo ktk nchi mbili na kusaidia wizi koo fulani kutoka nchi tofauti.

Hivyo Badala ya sisi kujihami kwa mishale na mikuki ni wakati sasa Polisi watulinde na mali zetu.

Kuhusu CCM sijui CUF ama sijui nini siungi chama chochote kwa maana mimi natambua WANASIASA WETU ktk vyama vyote MALENGO yao NI MAMOJA yanafanana ktk kila NYANJA.

Mimi ninachopinga hapa ni kundi fulani likiona upepo unaenda mrama basi linaanza kujitengenezea mazingira ya kuhalalisha kushindwa kwake.

Mfano kulalamika POLISI eti ndio ushaidi wa kuibiwa kura siikubali MAANA kila kituo cha kupiga kura hua kina mwakirishi kutoka kila chama na matokeo hua wanapiga sahihi na kupewa kopi ya matokeo kila kituo.

Mimi ninachosema CHAMA kilalame baada ya kukusanya matokeo ya wawakirishi wake kila kituo cha kupiga kura kuwa tofauti na yaliyotangazwa na sio POLISI.
 
Sio kweli kupigana sio suluhu.
Marehemu Chacha alitanganzwa mshindi hakua wa ccm..........

Marehemu Chacha alishinda baada ya mishale kutembea sana na road blocks kwa sana za kuzuia nyendo za usiku za kilaghai za mafisadi. Ninafahamu. sijahadithiwa Nilikuwepo. Wana wa Songea walijifunza hilo. Nchimbi na uwaziri wake alipewa house arrest na wapinzani hakuweza kugawa burungutu la fedha alizokuja nazo na diwani wa chadema akashinda kata ya Songea mjini mwaka huu.
.........Sio lazima kupigana lakini ni lazima nguvu tena ya ziada itumike ili kuwe na fair play. Bila hivyo itakuwa danganya toto kama Kiteto. huwezi kumnyanganya fisadi kula bila kumpiga nyundo ya uso.
 
Kwa hiyo BURUNGUTU NCHIMBI alilitia ndani kwi kwi kwi kwi.

Hapana mkuu ni zana potofu tu imejengeka vichwani mwa wapinzani wachache ama ni njia yakujitafutia huruma baada ya kubwagwa ama ni tabia tu ya binadamu ya kwamba failure zake zimesababishwa na mtu fulani.

Kwa TZ bara asilimia 99% uchaguzi hua huru na wanashinda walio weza jipenyeza kwa wananchi kwa namna moja ama nyingine.

KABUYE BIHARAMULO alichukua ubunge kwa ticket ya TLP wala hakuna aliyelinda kura kuiibiwa.

Naamini hata KIGOMA kwa wakati waakina KABULU na ZITO sizani kama walilinda na kupigana vikumbo na polisi .

Mkuu wapinzani wanashindwa kuelewa kabisa kushindwa kwao
1.Wapinzani ni WAZEE wa LAST MINUTE yani wanatia nguvu nyingi zisizo mhimu wakati wa kampeni.Ni sawa na mwanafunzi mda wote hasomi ila analala usiku kucha akisoma na asubuhi yake anaiingia ktk mtihani.

2.wapinzani wanaungwa mkono na vijana wengi ambao hata hawajajiandikisha kupiga kura na wanaopiga kura na vijibibi na vijibabu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom