Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Kitu nachoona kwa mkoa wa mara au sehemu pekee ya mara maeneo ya Nyamongo,tarime,kemakorere,ngenkuru,nyamwaga,nyekunguru etc.

Ni watu wa hapa kukubali kuchanganyikana ili kutengeneza kizazi kipya...kuchanganya ile damu na zingine za maeneo mengine...kwa mfano....waje wasukuma,wahaya,wachaga,wazaramo na wengine waoane na watu wa maeneo haya,kwenye shule kuwa na wakina Rwechungura,Said,massawe,Mwakyembe,buyamba.Shija,Fatuma...itapunguza sana baada ya muda mrefu hii hali iliyo jengeka maeneo haya.Na sio unakuta majina yale yale Kibacho,Marwa,Ghati,Bhoke,chacha,mwita....

Kwenye hii ni njia moja kati ya nyingine nyingi zinazo weza fanikiwa....si busara wa sifa kila wakati wao ni kupigana na askari....ona sasa tunaongelea siasa lakini huwezi kuongelea hilo bila kuweka swala la mapigano...kwa maeneo haya....wakati mwingine tunaweza kuwa tunailaumu serikali lakini wana sababu zao za kuleta askari hata kama utaenda kwa amani bila watu kupigana,ila hawatabiriki hawa hata wakati wa kampeni.

Lolote linaweza tokea..baada,kabla,au wakati wa uchanguzi...na jana walikuwa wanatoa kiapo askari kufanya kazi yao kwa ufanisi....hii sio nzuri na si sifa ya kujivunia kuwa kupigana ni sifa...ilikuwa zamani..hii..kwa sasa haina nafasi kabisa...

Na kwa mtizamo wangu..navyoona CCM watashinda ukiongea na watu wa hapa chama cha upinzani ni CCM na ndio wanataka kishinde kama nimeelewa...yaani kwa kuwa chama tawara tarime ni chadema ambao wanataka kubakisha utawala ndani yao kwa hiyo CCM ndio upinzani kwa sasa.Huyu waliye mteu kwa sasa chama cha upinzani (CCM).

Anakubalika kwa asilimia 60 labda ibadilike siku chache kabla ya uchaguzi...

Good day
 
Kwa hiyo BURUNGUTU NCHIMBI alilitia ndani kwi kwi kwi kwi.

Hapana mkuu ni zana potofu tu imejengeka vichwani mwa wapinzani wachache ama ni njia yakujitafutia huruma baada ya kubwagwa ama ni tabia tu ya binadamu ya kwamba failure zake zimesababishwa na mtu fulani.

Kwa TZ bara asilimia 99% uchaguzi hua huru na wanashinda walio weza jipenyeza kwa wananchi kwa namna moja ama nyingine.

KABUYE BIHARAMULO alichukua ubunge kwa ticket ya TLP wala hakuna aliyelinda kura kuiibiwa.

Naamini hata KIGOMA kwa wakati waakina KABULU na ZITO sizani kama walilinda na kupigana vikumbo na polisi .

Mkuu wapinzani wanashindwa kuelewa kabisa kushindwa kwao
1.Wapinzani ni WAZEE wa LAST MINUTE yani wanatia nguvu nyingi zisizo mhimu wakati wa kampeni.Ni sawa na mwanafunzi mda wote hasomi ila analala usiku kucha akisoma na asubuhi yake anaiingia ktk mtihani.

2.wapinzani wanaungwa mkono na vijana wengi ambao hata hawajajiandikisha kupiga kura na wanaopiga kura na vijibibi na vijibabu.

Point zako mbili za wapinzani kuwa watu wa last minute na kuungwa mkono na vijana ambao hawakuandikishwa ni valid kabisa wala sizipingi. Lakini kusema uchaguzi ni fair hapo nakataa. Absolutely not!
Katika kila chaguzi kuu za vyama vya vingi nimekuwa wakala wa chama cha siasa kwenye vituo vya kupigia kura. Katika kila chaguzi either nimeishia polisi au mkuu wa kituo cha uchaguzi kuitwa kuja kusuluhisha malumbano yanayotokea kwenye vituo vya kupigia kura baada ya kuona kwamba haki haitendeki. How can it be fair wakati wapinzani hawashirikishwi kwenye michakato ya kupanga chaguzi zenyewe ila ccm tu??? Kwanza tume ya uchaguzi inachaguliwa na mwenyekti wa ccm sasa haki itatoka wapi. Unategemea kuwe na haki simba na yanga wakicheza halafu refa awe kada na mwanachama mwaminifu wa simba????

failure ya wapinzani haijaletwa na wapinzani wenyewe. Ila ni failure ya sisi watanzania walio wengi kutojua maana ya upinzani na kutoipa support. Upinzani sio vyama vya siasa peke yao upinzani ni wadau wote wanaotaka tuwe na checks and balances effective katika nchi yetu. Tunasubiri upinzani ukue upendeze ndipo tuunge mkono.

Kabuye was under estimated ndio maana akashinda vilevile mshindani wake alikuwa ameshachokwa na wapiga kura. watu wa kigoma wao wanatumia silaha kali zaidi kuliko mishale. Wana take advantage ya woga na hofu za waty wa kule za kishirikina ilikuwaweka kwenye mstari.
 
Ingelikuwa Chambiri na Gachuma ningepata uhondo!Yaani mmoja atoke CCM na mwingine Chadema.
 
Sawa kabisa mkuu ,ila kuna falsafa tunayopingana kidogo mimi Falsafa yangu ni kua MAbadiriko ya CHAMA ktk kushika hatamu hayataleta mabadiriko yoyote.Wanasiasa wetu ni wale wale mahudhui yao ni mamoja wawe wametoka upinzani ama chama tawala.

Harafu unapoongelea UPINZANI kuungwa mkono sijui una maana gani je wapinzani kwa vile ni wapinzani lazima tuwaunge mkono? Na je mfano CUF wakishitaka hatamu CCM watakua wapinzani na je? utahubiri tena watu waunge mkono CCM kwa vile ni wapinzani??

Nikupe mfano Wakati kibaki alipokua MPINZANI wakenya walikua na matumaini makubwa unajua walitofautiana nini na RAILA ni kwa sababu KIBAKI alikataa kuteua waziri mkuu ambaye ndiye RAILA awe na mamlaka makubwa.

KIKUBWA ndg yangu ni SERA zipi wapinzani wameaanda kuziuza ? hicho ndicho kikubwa . Achana na UFISADI na mikataba maana kila kichaa atasema kukomesha ufisadi na mikataba.
Je? ni mikakati ipi na sera zipi ambazo wapinzani wameziuza na wewe kuamini wakiingia madarakani watatukomboa??

NB.Naomba utofautishe sera na njozi.Njozi ni kama zile ya kua tutawapa elimu bure,matibabu bure,mabomba yanayotoa maji na maziwa,barabara nzuri na umeme mpaka vijijini.
 
Mwanawasu
Ndg yangu tusema ukweli tu wala tusipindishe mambo ,wizi wa ng'ombe zetu wala hua CCM hawa utengenenzi.

Haya mapigano yetu yamekuwepo mara nyingi sana ila wakati wa nyuma habari ilikua haisambai kwa urahisi kutokana na technologia ya habari kua finyu na mapigano yaliyokua yanasikika ni yale yaliyopiganwa mda mrefu.

Lakini sasa imefika wakati lazima tukubali haya mapigano yatokomezwe kwanza ndio tutapiga kura zetu kwa utulivu.

Isitafasiriwe kua Mapigano haya ni kwa sababu sisi watu wa mara ni wakorofi hapana hiyo si kweli ILA ukiangalia MIPAKANI kote kule juu kwa KENYA mipakani mwa ethiopia na somalia kuna mapigano ya aina hii na hata ukiangalia kule juu mwa UGANDA napo ni hivyohivyo ,hii inatokana na kabila fulani kua na koo ktk nchi mbili na kusaidia wizi koo fulani kutoka nchi tofauti.

Hivyo Badala ya sisi kujihami kwa mishale na mikuki ni wakati sasa Polisi watulinde na mali zetu.

Kuhusu CCM sijui CUF ama sijui nini siungi chama chochote kwa maana mimi natambua WANASIASA WETU ktk vyama vyote MALENGO yao NI MAMOJA yanafanana ktk kila NYANJA.

Mimi ninachopinga hapa ni kundi fulani likiona upepo unaenda mrama basi linaanza kujitengenezea mazingira ya kuhalalisha kushindwa kwake.

Mfano kulalamika POLISI eti ndio ushaidi wa kuibiwa kura siikubali MAANA kila kituo cha kupiga kura hua kina mwakirishi kutoka kila chama na matokeo hua wanapiga sahihi na kupewa kopi ya matokeo kila kituo.

Mimi ninachosema CHAMA kilalame baada ya kukusanya matokeo ya wawakirishi wake kila kituo cha kupiga kura kuwa tofauti na yaliyotangazwa na sio POLISI.

Mwana wasu,

Hakika leo umenena, hapa ninaanza kukusoma japo mimi nina asili ya jazba, kweli kama kila chama kitakuwa na wawakilishi kila kituo na pia simu za mikononi nazo zipo kwa wingi si lahisi kuibiwa kura,

Mwana wasu, mimi ningependa kukuuliza ni nini kifanyike ili huu mkoa wetu WOTE (Mara) uwapate wabunge wote wa upinzani ?

Mwana wasu ni kwanini hapa Tanzania bara hatuna mikakati ya kweli kwa kupitia vyama vya upinzani ili kukipiku chama cha CCM?

Je hatuna watu kama akina Raila wa pale kenya hapa Tanzania na je vyama hivi vimejiandaaje 2010 ?
 
Kitu nachoona kwa mkoa wa mara au sehemu pekee ya mara maeneo ya Nyamongo,tarime,kemakorere,ngenkuru,nyamwaga,nyekunguru etc.

Ni watu wa hapa kukubali kuchanganyikana ili kutengeneza kizazi kipya...kuchanganya ile damu na zingine za maeneo mengine...kwa mfano....waje wasukuma,wahaya,wachaga,wazaramo na wengine waoane na watu wa maeneo haya,kwenye shule kuwa na wakina Rwechungura,Said,massawe,Mwakyembe,buyamba.Shija,Fatuma...itapunguza sana baada ya muda mrefu hii hali iliyo jengeka maeneo haya.Na sio unakuta majina yale yale Kibacho,Marwa,Ghati,Bhoke,chacha,mwita....

Kwenye hii ni njia moja kati ya nyingine nyingi zinazo weza fanikiwa....si busara wa sifa kila wakati wao ni kupigana na askari....ona sasa tunaongelea siasa lakini huwezi kuongelea hilo bila kuweka swala la mapigano...kwa maeneo haya....wakati mwingine tunaweza kuwa tunailaumu serikali lakini wana sababu zao za kuleta askari hata kama utaenda kwa amani bila watu kupigana,ila hawatabiriki hawa hata wakati wa kampeni.

Lolote linaweza tokea..baada,kabla,au wakati wa uchanguzi...na jana walikuwa wanatoa kiapo askari kufanya kazi yao kwa ufanisi....hii sio nzuri na si sifa ya kujivunia kuwa kupigana ni sifa...ilikuwa zamani..hii..kwa sasa haina nafasi kabisa...

Na kwa mtizamo wangu..navyoona CCM watashinda ukiongea na watu wa hapa chama cha upinzani ni CCM na ndio wanataka kishinde kama nimeelewa...yaani kwa kuwa chama tawara tarime ni chadema ambao wanataka kubakisha utawala ndani yao kwa hiyo CCM ndio upinzani kwa sasa.Huyu waliye mteu kwa sasa chama cha upinzani (CCM).

Anakubalika kwa asilimia 60 labda ibadilike siku chache kabla ya uchaguzi...

Good day

Mkuu,heshima mbele.

Mara ya mwisho kufika mwanza ilikuwa lini? uapakumbuka pale buzuruga? da....., unachekesha sana,

Hebu ile shule ya buswelu ipo?

Mtizamo wako si mbaya sana japo kuwa una hisia tu, na lingine ni kuwa laiti ungejua hiki chama cha CHADEMA kilivyojiimarisha hapa nyumbani, ungekaa kimya na usingelikuwa a la kusema.

keep it up
 
Point zako mbili za wapinzani kuwa watu wa last minute na kuungwa mkono na vijana ambao hawakuandikishwa ni valid kabisa wala sizipingi. Lakini kusema uchaguzi ni fair hapo nakataa. Absolutely not!
Katika kila chaguzi kuu za vyama vya vingi nimekuwa wakala wa chama cha siasa kwenye vituo vya kupigia kura. Katika kila chaguzi either nimeishia polisi au mkuu wa kituo cha uchaguzi kuitwa kuja kusuluhisha malumbano yanayotokea kwenye vituo vya kupigia kura baada ya kuona kwamba haki haitendeki. How can it be fair wakati wapinzani hawashirikishwi kwenye michakato ya kupanga chaguzi zenyewe ila ccm tu??? Kwanza tume ya uchaguzi inachaguliwa na mwenyekti wa ccm sasa haki itatoka wapi. Unategemea kuwe na haki simba na yanga wakicheza halafu refa awe kada na mwanachama mwaminifu wa simba????

failure ya wapinzani haijaletwa na wapinzani wenyewe. Ila ni failure ya sisi watanzania walio wengi kutojua maana ya upinzani na kutoipa support. Upinzani sio vyama vya siasa peke yao upinzani ni wadau wote wanaotaka tuwe na checks and balances effective katika nchi yetu. Tunasubiri upinzani ukue upendeze ndipo tuunge mkono.

Kabuye was under estimated ndio maana akashinda vilevile mshindani wake alikuwa ameshachokwa na wapiga kura. watu wa kigoma wao wanatumia silaha kali zaidi kuliko mishale. Wana take advantage ya woga na hofu za waty wa kule za kishirikina ilikuwaweka kwenye mstari.

Nyumbu;

Tutaendelea kulalama hivi mpaka lini? tutaendelea kuonyesha huu uoga mpaka lini?

Mbona Zimbabwe imewezekana, mbona kenya iewezekana? mbona hata Tarime ITAWEZEKANA? mageuzi huamuliwa na wananchi na si vinginevyo.

Watanzania tuache uoga, tuache kulalama, tuonyeshe vitendo sasa, tukatae hila za CCM, tena kwa kuwapinga waziwazi, wakipenda watuuuwe tu ili kizazi chetu kipone, ni nani katuloga?
 
Nimesoma maoni yenu na nasoma maoni yenu hadi sasa .Majuzi usiku nimevamia kituo cha polisi ki namna kuona kunani .Niamini Tarime ni Iraq ndogo kama wanavyosema .Tarime na Serikali ya CCM hawana maelewano .Leo mtu akija akasema Kingoye anakubalika kwa 60% nashangaa sana .CCM itabwagwa tena kwa mara nyingine kwa kuwa Gachuma na Makamba wametumia nguvu kubwa kuliko kuwasikiliza wana CCM na wana Tarime .Gachuma hatikiwi kabisa ila wanaweza kushinda kwa kuwa mkakati wa Tossi na Mwema ni mzito .Tarime imejaa polisi na magari ya polisi kuliko kawaida .Jana mapema asubuhi nimesema na mwananchi mmoja akasema Lunyungu hapa watakufa watu sana safari hiii na kama huamini ngojea maana Polisi wanalitaka jimbo kwa nguvu zote .Uharamia huu wote JK yuko nyuma yake .
 
Wananchi wote warudi ccm na kuibadilisha lasivyo mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yako njiani....
 
Askari polisi waliomwagwa Tarime walia njaa

Na Mwandishi wetu

ASKARI polisi 400 waliopelekwa kulinda amani na kusimamia uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Tarime mkoani Mara, wanalia njaa baada ya kukosa fedha za kujikimu.

Askari hao wanasema hali yao ni ngumu kutokana na posho wanayolipwa kutokidhi mahitaji muhimu ya binadamu.

Mmoja wa askari hao aliyezungmza na Mwananchi Jumapili kutokea Tarime jana alisema wanalipwa kiasi cha Sh 1,000 kwa siku badala ya sh 35,000 kwa siku wanayopaswa kulipwa.

"Kimsingi hali yetu ni ngumu, hakuna chakula cha kutosha wala sehemu nzuri ya kulala. Posho tunayolipwa ni ndogo isiyoweza kukidhi hata mlo mmoja," alisema askari huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Kwa mujibu wa askari huyo, askari hao kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tabora, Arusha, Singida, Dar es Salaam, Manyara, Mara na Singida, ingawa wameshawasilisha malalamiko yao kwenye uongozi wa juu wa jeshi la polisi nchini, mpaka sasa hakuna jitihada zozote zilizofanywa kumaliza tatizo.

Alisema ukosefu huo wa fedha umesababisha baadhi yao kupata chakula kibovu na hivyo kuharisha.

"Kwa kuwa tu nyie mko mbali lakini hali ni ngumu, baadhi yetu wameanza kuhara kutokana na kulazimika kula chakula kisichokuwa na ubora," alibainisha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Liberatu Barlow jana alishindwa kuzungumzia suala hilo kwa maelezo kuwa yuko nje ya mkoa na kulitaka Mwananchi Jumapili kuwasiliana na Mkuu wa Opesheni wa Jeshi hilo, Kamanda Venance Tossy kwa maelezo zaidi.

Hata hivyo, Tossy jana hakuweza kupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kuita muda wote bila kupokelewa.

Naye Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Abdalah Mssika alisema jana kuwa ofisi yake haina taarifa ya suala hilo ingawa inawezekana taarifa ziko kwa viongozi wa juu wa jeshi la hilo.

"Inawezekana taarifa hizo zipo lakini mimi sijapata taarifa, tafadhali wasiliana na Kamanda Tossy kwa maelezo zaidi," alisema Mssika.

Askari hao walianza kuingia Tarime Jumapili iliyopita na watakaa huko kulinda amani na kusimamia uchaguzi mdogo wa jimbo hilo unaofuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wake, Marehemu Chacha Wangwe.

Source: Mwananchi
 
^^ Wacha sera za uchochezi wewe...!

Sio sera za uchochezi ,bali angalia Afrika nzima ni jinsi gani vyama tawala vinajiweka na vyombo vya dola , bila ya wananchi na vyama vya upinzani kuweka mkakati wa roho kwa roho basi mageuzi hayatapatikana , na huo ndio ukweli.

Ona Kenya ni kitu gani kimetokea leo hii heshima ipo pahala pake,na hapo Zimbamwe japo hawakufikia kutoana roho lakini walikuwa hawako mbali.
sasa imebaki Tanzania ambayo inanyanyaswa na vyombo vya dola ambavyo kwa uwazi kabisa vinatumika kuiwekea ubavu CCM.
Mifano ya vyombo hivi kutumika haihitaji miwani na darubini kuichunguza ipo wazi mfano mzuri ni wa Zanzibar ambako huko inasadikiwa polisi ndio wababe wanaoendesha matokeo na kutumika kuwahamisha mamluki kupiga kura kwenye vituo tofauti kwa kasi.

Haiwezekani jambo hili kuachwa kuendelea ni lazima likomeshwe na jinsi ya kulikomesha ni kuwatolea uvivu polisi ,ole wao polisi Zanzibar ni ndogo hakuna pa kujificha lakini kwa upande wa Tanganyika mbona risasi zikianza kurindimba na mishale kurushwa kutoka kila pembe polisi bila ya shaka yeyote watajua nini maana ya kuingia mitini.
 
Unapotolea mfano KENYA pia ukumbuke kabisa hicho chama TAWALA miaka sita tu iliyopita kilikua chama cha UPINZANI.

Mimi kwa kweli falsafa ya upinzania kushika hatamu ndio MWARABAINI bila kuangalia SERA zao WANAZINADI kivipi? na zimekaa vipi? bado itakua safari ndefu.
 
Mimi kwa kweli falsafa ya upinzania kushika hatamu ndio MWARABAINI bila kuangalia SERA zao WANAZINADI kivipi? na zimekaa vipi? bado itakua safari ndefu.[/QUOTE]

Bado Logic ya upinzini kushika hatamu ya uongozi tanzania hainiingii kichwani sawa sawa...sikatai baadhi yao ni wazuri...ila nani kati yao kuingia kushika serikari harafu awaongoze wenzie...mpaka sasa labda wakubali kubadili viongozi wao wote wajuu ili tuweze kuona mabadiliko mitizamoio...hawa tulio nao wote tulikuwa nao 10yrs back...sasa hawabadiliki...wameshindana mkapa sasa kikwete...

Kuna mtu anaweza kutuaminisha kati yao nani anaweza?Perhaps Mrema?Mvungu?Mbowe?Mbatia?Mtikila?
 
Tarime: CCM chali!

2008-09-13 18:09:11
Na Margaret Malisa, PST-Pwani

Wakati kampeni za uchaguzi mdogo wa kumsaka Mbunge wa Jimbo la Tarime zikitarajiwa kuanza kwa kishindo kesho, Chama cha Mapinduzi, CCM kimedaiwa kupata pigo la aina yake baada ya upinzani kuzoa viti vingi vya uongozi katika Serikali ya Kijiji cha Borenga, Kata ya Kisaka wilayani Tarime.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF , Bw. Wilfred Lwakatare, kuhusiana na matokeo ya uchaguzi mdogo uliofanyika katika kijiji hicho, inadai kwamba CCM imeambulia nafasi moja tu ya ujumbe kati ya sita zilizogombewa.

Taarifa hiyo ya Bw. Lwakatare imedai kuwa CCM pia imelizwa katika nafasi ya uenyekiti wa kijiji hicho ambayo imeangukia mikononi mwa CUF.

Aidha, kwa kutwaa na nafasi hiyo ya uenyekiti, kwa ujumla upinzani umeweza kutwaa nafasi sita zilizowaniwa huku CCM ikiambulia moja pekee ya mjumbe mmoja wa Serikali ya kijiji hicho.

Bw. Lwakatare amedai kuwa matokeo kamili ya uchaguzi huo wa uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Borenga, yameonyesha kuwa wananchi wamemchagua kwa kura nyingi Bw. Raphael Chacha Msembete wa CUF kuwa Mwenyekiti wa kijiji chao.

Taarifa hiyo ya Bw. Lwakatare kwa vyombo vya habari, imesema Mwenyekiti huyo alichaguliwa kwa kuzoa kura 437 katika uchaguzi ulioshirikisha vyama vya CCM, NCCR- Mageuzi na CHADEMA.

Akasema wakati mgombea wa CUF akishinda kwa kuzoa kura hizo, mgombea wa CCM Bw. Peter Dulla alipata kura 252 huku yule wa CHADEMA , Bw. Julius Sagi, akipata kura 54.

``Nawapongeza wanakijiji (wa Borenga) kwa kukikataa chama cha CCM baada ya kuona kimeshindwa kuwaletea maendeleo na kumchagua mgombea wa chama chetu,``akasema Bw. Lwakatare.

Pia akasema kuwa katika uchaguzi huo, wanakijiji waliwachagua wajumbe watatu kutoka CUF kati ya wajumbe sita, huku wengine wakiwa wakitoka CHADEMA, NCCR- Mageuzi na CCM ambayo nayo ilifurukuta na kuambulia moja.

Kwa matokeo hayo, Bw. Lwakatare akasema CUF inawapongeza wanakijiji wa Borengo kwa kutambua kuwa CCM imeshindwa kuwaletea mabadiliko ya maana katika maendeleo na maisha yao .

Akawataka Watanzania wengine kuiga mfano huo kwa kutambua kuwa CCM imeshindwa kukidhi matarajio yao na badala yake wakimbilie upinzani.

``Walichokifanya wananchi wa Borengo ni mfano wa kuigwa hasa kwa Chama ambacho hakijali wananchi wake kwa kutumia rasilimali na kodi za nchi kwa maslahi ya wachache waliopo madarakani,`` akasema Bw. Lwakatare.

My take

Hao Chadema wenyewe nao mdebwedo vile vile
 
Kitimutimu uchaguzi Tarime leo

2008-09-14 11:13:05
Na Abdallah Bawazir

Kinyang`anyiro cha kampeni za kuwania ubunge wa Jimbo la Tarime mkoani Mara, kinaanza kutimua vumbi leo, ambapo zitashuhudia wanasiasa kutoka vyama vyote vilivyosimamisha wagombea wakipigana vikumbo kuhakikisha wagombea wao wananyakua nafasi hiyo.

Tayari vyama vyote vimejigamba kuwa vitaibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika kujaza nafasi ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Chacha Wangwe, ambaye alifariki katika ajali ya gari maeneo ya Kongwa, nje kidogo ya mji wa Dodoma hivi karibuni.

Marehemu Wangwe, alikuwa Mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeeleo (Chadema).

Wakati kampeni hizo zikianza leo, katika siku za hivi karibuni kumekuwa kukishuhudiwa matukio mbalimbali ya kuelekea uchaguzi huo, ikiwemo vyama vya siasa kuteua majina ya wagombea wao watakaopambana kuwania nafasi hiyo.

Jingine ambalo limeshuhudiwa ni kusambaratika kwa ushirikiano wa vyama vya upinzani katika kusimamisha mgombea mmoja, mambo ambayo yataleta changamoto kubwa wakati wa kampeni hizo.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa kampeni za kuwania ubunge wa jimbo hilo huenda zikawa kali na za aina yake, kutokana na historia ya jimbo la Tarime pamoja na hali ya kisiasa jimboni humo na mazingira yaliyopelekea kifo cha Wangwe kwa ujumla.

Tangu kifo cha Wangwe kilichotokea Julai 28, 2008, kumekuwa na kampeni za chini kwa chini za vyama vya siasa kutumia kifo hicho kuchafuana kwa malengo ya kisiasa vikilenga zaidi kuwateka akili wapiga kura wa Tarime kuunga mkono vyama vyao.

Tukio la kipekee lililotokea ni pale mazishi ya Wangwe yalipoahirishwa Julai 31, 2008 kutokana na familia kutaka uchunguzi wa kujitegemea juu ya chanzo cha kifo cha Mbunge huyo machachari, hali iliyowagawa viongozi hao kwenye makundi mawili.

Chadema wamekuwa wakilaumu wenzao kwamba walitaka kutumia msiba huo kupata faida ya kisiasa Tarime na kukiangamiza chama chao, lawama ambazo pia zilielekezwa CCM.

Hali hiyo imeonekana kuwavuruga zaidi viongozi wa vyama vya upinzani ambao tangu kifo hicho kitokee wamekuwa katika `mgogoro baridi` unaowafanya hata washindwe kukaa meza moja kwa ajili ya kusimamisha mgombea mmoja mwenye nguvu dhidi ya wa CCM kama walivyokubaliana siku za nyuma.

Wachambuzi wa masuala ya kiasiasa wanasema kuwa hali hiyo inaipa afueni CCM kuweza kushinda kirahisi kiti hicho kwa kutumia udhaifu wa vyama hivyo pamoja na kutoaminiana kwao.

Masuala kadhaa huenda yakachukuwa nafasi kubwa wakati wa kampeni hizo ambazo zitachukua karibu mwezi mmoja, kila cha kikijaribu kadiri ya uwezo wake kuvuta hisia za wapiga kura.

Vyama vya upinzani huenda vikajikita zaidi katika masuala ya ufisadi ambao baadhi ya viongozi wa CCM na wa serikali wanatuhumiwa nao pamoja na mapigano ya yenyewe kwa wenyewe, hali duni ya maendeleo na matumizi ya rasilimali yakiwemo madini yanayopatikana jimboni humo.

Kwa upande wake CCM huenda ikatumia udhaifu wa vyama vya upinzani kushindwa kufikia maamuzi ya kuungana mkono kusimamisha mgombea mmoja, kikiwashawishi kuwa vyama hivyo siyo vya kuviamini kuvipa nafasi za uongozi kwani vyenyewe vinashindwa kutekeleza maamuzi yake pamoja na kujawa na migogoro ya mara kwa mara.

Kutokana na mwenendo unaoonekana sasa, si ajabu pia kampeni hizo zikashuhudia vyama vya upinzani vikishambuliana vyenyewe kwa vyenyewe, hali ambayo pia inaweza kusababisha hali tete endapo viongozi wa vyama hivyo hawatachukua tahadhari wakati wa kutoa hoja zao kwa wananchi.

Wakati huo huo, Anna Mrosso,kutoka Tarime anaripoti kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kushirikiana na chama cha wananchi CUF jana vimefanya maandamano makubwa wakati wa kumsindikiza mgombea wa ubunge kwa tiketi ya Chadema akirejesha fomu katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi huo mdogo jimbo la Tarime.

Maandamano hayo makubwa yakishirikisha wananchi wa kila rika kwa kutembea kwa mguu yalionyesha dalili za wazi kukiwashia indiketa chama tawala CCM ambacho pia jana kilifanya maandamano ya kumsindikiza mgombea wao kurejesha fomu hizo kwa msimamizi huyo wa uchaguzi.

Chadema kwa kushirikiana na CUF walisindikiza mgombea wao wa ``ndoa`` Charles Mwera, aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime kabla ya kujitosa katika kinyang`anyiro hicho na CCM walimsindikiza mgombea wao wa ubunge Christopher Kangeye, ambaye kabla ya uteuzi wake alikuwa ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) makao makuu.

Walianza CCM kufanya maandamano hayo yakiwa na magari zaidi ya 50 na wananchama wachache wengi kutoka mjini Musoma wakiongozwa na pikipiki na baiskeli kutokea katika ofisi za chama hicho Mtaa wa Sabasaba, Tarime kupitia barabara kuu hadi makao makuu ya ofisi za tume mjini hapa.

Katika hali ya kushangaza mitaa yote yaliopita maandamano hayo ya CCM wananchi walijitokeza kando ya barabara walionekana kuwa kimya huku wengine wakionyesha ishara ya vidore viwili pamoja huku nyimbo za msanii wa CCM kapteni John Komba zikiimbwa.

Hata hivyo wakati msafara huo ukirejea katika ofisi hizo za CCM majira ya saa 8.30 mchana katika maeneo ya darajani ukakutana na msafara wa Chadema na CUF hali ambayo kwa haraka ilitafsiriwa kungeweza kutokea umwagikaji wa damu lakini walipishana pamoja na kurushiana vijembe.

Wingi wa wafuasi hao wa vyama vya upinzani wakiwa kwa miguu na gari zisizozidi tatu, mikokoteni, pikipiki na baiskeli ilitisha kwa umma wa Tarime kwani watu waliojipanga kando walionekana kuwashangilia na kuonyesha vidole viwili kama ishara ya kuwaunga mkono.

Wafuasi hao walisikika wakiimba nyimbo za kudai hakuna nafasi kwa mafisadi jimbo la Tarime bali masikini mwenye kujua uchungu wa nchi na wilaya yake.

Zaidi ya wapiga kura 150,000 wanatarajia kupiga kura katika uchaguzi huo ambapo vituo 369 vimeandaliwa kwa ajili ya zoezi hilo wakati ulinzi mkali umewekwa kwa kuhusisha askari polisi zaidi ya 400 wakiongozwa na kamishina msaidizi wa polisi (DCP) Venance Tosi.
 
Sorry wakuu,SOURCE ya hiyo habari ni NIPASHE

Ben,

Naomba utambue kuwa Tarime ni sehemu yaTanzania, tena wilaya inayoingizia mapato nchi hii ila tumesaurika, tunataka tuwe chachu ya demokrasia hapa nchini,

Na pia salaam kwa mafisadi wote popote pale walipo wasijaribu kufanya kamchezo kokote hapa, wataona wasilotegemea.

Najua wanajua na hawawezi kufanya lolote lile.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom