JKT kuna mtu wa Musoma mmoja alizoea kusema kura nimekura pa kurara je? Musoma wana r tatizo ni kwenye l.
Kweli mkuu
Mimi hua sijui wapi niweke L ama R hua najiuliza sijui ni tatizo gani linasumbua na kwanini iwe hivyo?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
JKT kuna mtu wa Musoma mmoja alizoea kusema kura nimekura pa kurara je? Musoma wana r tatizo ni kwenye l.
Mbowe,Lunyungu,DK.slaa,Mvungi,zitto,mrema....na mkuu wa wilaya anajua hali halisi ziaidi ya siasa morali waliuyo nayo watu wa uku..uku kuna msema wanaume hawapigwi wote jamani...
Mtu asiye na kovu si mwanaume...lazima uwe na alama flani ya kukatwa ajari...kuonyesha umepitia hard time....mtu kwenda jela ni sifa...sasa wakati wa uchaguzi kuwaacha bila kuwa na hata picha ya askari...unataka kutengeneza nini...?
Mie naunga mkono askari kuwepo hapa kwa kulinda usalama hasa wakati huu wa uchaguzi....mabasi yote yatokayo nje ya tarime stand kuu ni tarime,si kila mtu anataka kupiga kula bwana...sasa kama zogo litazuka stand polisi hawapo..na unataka kwenda mwanza,sirari,kenya...si utakuwa victim...?
Kwanza uku hakuna anaye ongelea polisi hata kidogo ni sie kwenye mtandao....watu wanaongelea CCM kushidwa tu...hatakwa kuweka gogo...lipigiwe kula..kwa mwenye kupambanua..unawe jua ni nini hawa watu wako tiyari kufanya.
Ingekuwa usukumani wangesema doho tabu...tokwicha... wanaachana na uchaguzi.
Good day
Wakati mwingine mambo ya kipuuzi kama haya inabidi yakemewe kabisa hapa JF na kwingine kokote. Hii generalization na dharau dhidi ya watu wa Tarime imezidi sana hapa JF na kwenye vyombo vya habari.
Wewe Buswelu acha upuuzi na ujinga wa kusema kuwa watu wa Tarime asili yao ni ugomvi. Mimi nimezaliwa na kukulia Tarime na sijawahi kuona hayo ya ugomvi wa asili na uvivu kama unaotaka kuuweka hapa.
Ukome kabisa kutumia lugha chafu dhidi ya watu wa Tarime. Kusema kuwa wao wangekuwa wasukuma kusingekuwa na mapigano ni upuuzi mkubwa sana na unaofaa kukemewa kwa nguvu zote.
Yanayoendelea Tarime yanajulikana kwa wanatarime na namna migogoro ya kipuuuzi inavyoletwa na kukukuzwa na vyombo vya usalama na vya habari ili kuwatoa watu kwenye the main issue ya Tarime - deposit kubwa kabisa ya dhahabu ambayo bado haijaanza kuchimbwa.
Hao polisi wanachofanya kinajulikana na watu wa Tarime wanawaangalia tu kwa mshangao. Mimi ningewashauri wa usalama kuwa makini na wastaarabu sana dhidi ya watu wa Tarime au watanzania wowote kokote kule Tanzania. Haya mambo ya kipuuzi na generalization za kizembe kama hizi hazitapelekea kusolve matatizo ya watu wa Tarime au watanzania ambao wanaendelea kuwa masikini kila kukicha.
Nimetumia lugha kali kwa makusudi ili kukemea upuuzi na maneno yako yenye vijembe dhidi ya watu wa Tarime kwako Busweli. Natumaini utaacha upuuuzi huu na kuanza kuheshimu watu wa Tarime ambao wengi wao ni wastaarabu na watu wasiopenda fujo.
Asante
Hoja iliyo mbele yetu ni kwanini Tossi,Suleimani kova waje wakati huu...wa uchaguzi..kwa kisingizio cha kisiasa ambayo kila mtu aliye changia ame support kuwa ni makosa...lakini mie upande wangu ni kuwa hawa watu bila polisi hawaendi jamani...au historia ilikupita kushoto magabe soma vyema utajua walikuwa wanatumika kama nini wakati huo.
Buswelu acha kudanganya watu,halafu uache dharau yako hiyo ya kijinga.
manake nyie watu msiokuwa wazawa wa huku mnajifanya mnawafahamu sana wakurya.Hapa unataka kuongelea historia gani!?huwezi kuijua historia yetu kuliko sisi wenyewe, huo ni uongo uliokomaa, kwasababu tunawajua watu wa ccm ni kawaida yenu kudanganya na kuhadaa watu.Nyeupe mmezoea kudanganya watu kuwa ni nyekundu!
kama watu wa tarime bila polisi hawaendi hiyo miaka yote mbona huyo kova,tossi na hao askari 300 hawajawahi kuwepo na chaguzi zimekuwa zikifanyika?Kwa mara ya kwanza watu wamefariki tarime kutokana na vurugu za uchaguzi mwaka 2005, na hiyo ni baada ya ccm kuona kwamba wanashindwa,walikuwa wakiitisha mikutano ya kampeni inakosa wasikilizaji wakaamua kuanzisha mkakati wa kuwashambulia chadema kitu kilichopelekea vifo vya wananchi.
Wewe hata hiyo historia unayotaka 'kutufundisha' wakati hujui kuwa katika majimbo yote yenye mlengo tofauti na ccm lazima polisi wapelekwe kwa wingi kwa visingizio visivyokuwa na kichwa wala miguu.Pemba kwa mfano nako wanaishi wakurya?Manake kila uchaguzi polisi, wanajeshi n.k wanjazwa huko.
Au kiteto napo kuna wakurya?au historia unayoijua haikukumbushi jinsi wafuasi wa ccm walivyowashambulia viongozi wa chadema!?
Historia hiyo hiyo inatuonyesha jinsi polisi ilivyowashambulia na kuwazuia kuendesha mikutano ya kampeni, wafuasi wa aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo la musoma mjini kwa tiketi ya cuf, bw.mustafa wandwi mwaka 2000&2005,wewe unaijua historia gani?
ninayo mifano mingi sana ya kukufundisha hiyo historia unayotaka kutudanganya kwamba unaijua.
Wewe ulitaka waje wakati gani?? na kwanini huhoji hayo makabila kwanini yamepigana wakati huu?
Mbona unakurupuka ndugu yangu.
soma vizuri maelezo yangu.na isitoshe unaonekana huijui tarime unasimuliwa tu!ndio sababu unachojua ni kwamba wanapigana sasahivi!!
yaani wewe siku zote hizo vyombo vya habari vinatangaza mapigano ya tarime hujawahi kuyasikia?hadi mwanamuziki mmoja wa bongo fleva ameweka mstari wa anchari na anchoka kwenye wimbo wake lakini wewe unayejiona mjuaji hilo limekupita kushoto?
kujibu swali lako, mimi nilitaka waje from the first day mapigano yalipoanza.
wakati wote marehemu wangwe akiitaka serikali kuimarisha ulinzi tarime na kukomesha mapigano ya kikabila ndo nilitaka waje.
na hata hivyo kwanini wamekuja kujazana mjini tarime ambako hakuna ugomvi badala ya kwenda vijijini kwenye ugomvi?
why??? kwaninini????
hovyo! ufumbuzi sio huomsianze kutenganeza mazingira ili mkishindwa mpate kupiga kelele .mnaanza kutuandaa mtakaposhindwa mje na hoja za polisi.
Kama mnaona vipi wawakirishi ktk vituo vya kupigia kura wawekeni makomandoo wa chadema na wao baada ya matokeo watakua na copy za matokeo hivyo wakitoa matekeo siyo ,ninyi mtuletee facts hizo na si fact za ffu na polisi.
Mimi naona bora yatokee mapigano na sio kunyukuana nyukuana ,yatokee kikweli kweli aidha polisi V/S wananchi au Upinzani V/S CCM , yaani zipigwe kikweli kweli ,ili dunia itupie macho utawala wa Muungwana na udikteta unaoanza kuota kama magugu...............
Walichoamua waPemba ni kuichanganya Polisi na CCM kama kitu kimoja hivyo majibu waliyoyapata polisi ni kuhesabiwa kama tawi la CCM na upinzani walioupata polisi ni sawa na upinzani unaoikumba CCM huko Pemba...........Je wabara mnaweza kuihesabu polisi kama chombo cha CCM na kupambana nancho kifo kwa kifo ?
hovyo! ufumbuzi sio huo
Heshima mbele Mwiba!!...... Habari ndio hiyo. Tanzania imefikia pahali kama wabongo hatuta amua kutumia nguvu basi tusitegemee kupata haki yetu kwa kupitia kisanduku cha kura. Sio tu jeshi la Polisi lakini vilevile Tume ya uchaguzi ni part and parcel ya CCM. Wasimamizi wa vituo vya kura ni hao hao makada ya chama cha mafisadi.
Unatakiwa mkongoto wa hali ya juu hadi roho za watu ziondolewe. Unapombana mbwa koko kwenye kona na kumshambulia pasipo huruma akiona kipigo kinazidi atakung'ata tu ili atoke hapo. Akikuumiza huwezi kumlaumu kwani njia ya kusalimisha maisha yake ilibaki moja tu.
Hata kama wakurya wanaikataa kata kata CCM, bila mishale kutembea kama iliyokuwa mwaka 2005 kangoye atatangazwa mshindi tu hata kama sio chaguo lao. Msiwe naive, Kura haziibiwi siku ya uchaguzi. kuweka makomandoo kituoni kunasaidia lakini sio solution. Kura zinaibiwa mapema. Kiteto kadi za kupigia kura zilipanda bei siku moja kabla ya kupiga kura msekwa, mungai, makamba walikuwa wanazinunua kwa shilingi elfu 45. Tarime kuna watu wananjaa vilevile kadi zitauzwa mtindo mmoja.
Viongozi wa CCM wakishirikiana na serikali wanaiba kura kwa kuwatishia wananchi wenye uelewa mdogo. Hao wapo kila mahali na huwezi kukataa. Bila kuwajaza hofu hawa watawala wezi wataendelea na intimidation tactics zao. Dawa yao ni kuwachinja tu. CNN na Aljazeera wajazane pale ndipo uchaguzi utakuwa wa huru. Kwa kutegemea TBC1 na magazeti ya rostam hata boksi la kula likiibiwa mchana kweupe hatutajulishwa tutaambiwa mambo yote yalikuwa salama.
Ufumbuzi ni kupigia kelele polisi waondoke ili watu waendelee kuchapana mshile.Duuuuuu hiyo imetulia.
Wala usiwe na shaka wakwetu,
Hiyo ya kumwaga FFU ni kawaida ya CCM wanapohisi uwezekano wa kupata ushindi ni mdogo sana.Wanajua kuwa tarime ni vigumu wao kupata ushindi kihalali, kwahiyo lazima watumie mabavu ili kujitangazia ushindi.
Lakini hakuna haja ya kukata tamaa, muhimu ni kuendelea kuhamasishana na hatimaye siku ya uchaguzi watu wajitokeze kwa wingi kumchagua mwakilishi atakayekuwa na jeuri ya kutetea maslahi ya wanatarime.Kuchagua ccm ni kuchagua kuzika maslahi ya wanatarime.Mbunge kutoka ccm hawezi kuwakilisha maslahi ya wananchi,atawakilisha maslahi ya ccm.Kwani katiba yao (ccm) haiwaruhusu kutetea maslahi ya nchi bali mafisadi!
Ukitetea maslahi ya nchi wanaku-NAPE!eti kwa utovu wa nidhamu!
Mwana wasu,
wachamawe!!, tangu sasa badili jina lako tafadhali,
Mkama jina lako haliendani wa hapa nyumbani Mara,yaani unafanana na watu wa pwani mkuu.hebu kweli ni furaha gani uliyonayo hapa jamvini na sisi ndugu zako tunaumizwa na hawa CCM?
Tunajua ninyi ndugu zetu mlioko Dar, Arusha , Mbeya MNATUCHEKA SANA WANA MARA KWA KILE TUNACHOKIAMINI NDANI YA MIOYO YETU, sisi tunaamini kuwa CCM wameshindwa kuendesha nchii hii na hivyo tunaona kuwa sasa ni wakati wa kuwatosa.
Tunajua kuwa sisi kama wana Tarime hatuwezi kuleta mabadiliko kwa kiasi kikubwa ila tutakuwa CHACHU ya demokrasia hapa nchini, endeleeni kutuunga mkono na hakika tutafikia hilo lengo letu, acheni kutubeza na kutudharau.
Sisi wanatarime hatuoni shida hata kama Jeshi la police lote tz likaamia hapa sisi tu washindi watarijiwa na Mungu atusaidie.
Sio kweli kupigana sio suluhu.
Marehemu Chacha alitanganzwa mshindi hakua wa ccm..........
Marehemu Chacha alishinda baada ya mishale kutembea sana na road blocks kwa sana za kuzuia nyendo za usiku za kilaghai za mafisadi. Ninafahamu. sijahadithiwa Nilikuwepo. Wana wa Songea walijifunza hilo. Nchimbi na uwaziri wake alipewa house arrest na wapinzani hakuweza kugawa burungutu la fedha alizokuja nazo na diwani wa chadema akashinda kata ya Songea mjini mwaka huu.
.........Sio lazima kupigana lakini ni lazima nguvu tena ya ziada itumike ili kuwe na fair play. Bila hivyo itakuwa danganya toto kama Kiteto. huwezi kumnyanganya fisadi kula bila kumpiga nyundo ya uso.