...Tena nina wasi wasi na IQ ya huyu mzee maana wakati mwingine ukisikiliza anachozungumza utashindwa kuelewa kama alienda hata shule kidogo au ndio bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi...ha-ha-ha-hah!
Makamba sijui tumfananishe na nani.
.
[Source Tanzania Daima]
Vijana 30 wa CHADEMA waswekwa ndani
na Mwandishi Wetu, Tarime
ZAIDI ya vijana 30 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamekamatwa na polisi wilayani Tarime kwa kile kilichodaiwa kuwa ni operesheni kamata wazembe na wazururaji.
Operesheni hiyo ilianza jana asubuhi ambapo askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), walimwagwa katika mitaa yote ya mji mdogo wa Tarime, hususan katika vijiwe maarufu vya wafuasi wa CHADEMA.
Vijana hao ambao hadi sasa bado wapo ndani, walifikishwa katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Tarime ambapo Mkuu wa Kituo hicho (OCD), aliwataka viongozi wa chama hicho waliokuwa wakiwafutilia vijana hao, kuacha kumwingilia katika kazi zake.
Akizungumza katika mikutano mitatu ya kampeni katika vijiji vya Mrito, Karende na Kewanja, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema kitendo cha Serikali kumwaga polisi wengi katika jimbo hilo, kinawatisha wananchi.
Dk. Slaa ambaye alikuwa akimnadi mgombea wa CHADEMA, Charles Nyanguru, alilalamikia kauli za Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa na Katibu Mkuu, Yusuph Makamba, kwamba wametumwa na Rais Kikwete, kuangalia hali ya vurugu ili wamjulishe rais.
Kauli hiyo ni ya vitisho na kamwe hapaswi kutolewa na viongozi hao. Tunasema serikali ndiyo inayojenga mazingira ya hofu katika uchaguzi huu, wakati wananchi hawana mpango wa kuanzisha vurugu, alisema.
Dk. Slaa alisema katika mkutano huo kuwa ana ushahidi wa kikao cha Makamba cha Septemba 19 kwamba Jimbo la Tarime liwe mikononi mwa CCM kwani wana pesa na polisi, hivyo hawana sababu ya kushindwa.
Alisema kutokana na hali hiyo, ndiyo maana polisi mjini hapo, wamekuwa wakitekeleza maagizo ya CCM ya kuwakamata vijana wanaoonyesha alama ya vidole viwili, inayotumiwa na CHADEMA.
Dk. Slaa alisema serikali inataka kulifanya Jimbo la Tarime kama visiwa vya Zanzibar katika uchaguzi kwani matokeo wanayoyafanya, yanaonyesha ni jinsi gani wanataka kuleta vurugu.
Katika mkutano huo, Dk. Slaa, alimlaumu Rais Kikwete kuwa amekuwa bingwa wa kusuluhisha matatizo ya nchi jirani kama vile Kenya na Zimbabwe wakati Zanzibar ikibaki katika uhasama na sasa hali hiyo inataka kupandikizwa Tarime.
Aliwataka wananchi hao kuacha kumpigia kura mgombea wa CCM kwani hataweza kuwaletea maendeleo na badala yake wamchague mgombea wa CHADEMA ili kumalizia kazi iliyoachwa na marehemu Chacha Wangwe.
Naye mgombea CHADEMA, Nyanguru, aliwaahidi kuwatetea vijana, hasa katika operesheni za aina hiyo ambazo alisema ni za kinyanyasaji.
Uchaguzi katika jimbo hilo utafanyika Oktoba 12.
Oyaa,
Baada ya ile debate kati yangu nawe kwenye suala la Mtikila na maneno yote uliyotoa, ilibidi nichukue muda wa kutosha kukusoma ili nijue na-debate na mtu wa aina gani. So far nina very good picture of you kutokana na nilichosoma.
Yaani ndicho kinachofanyika - na ndicho baadhi ya watu waliojaribu kuuliza hili kule Nyamongo "walipatikana na hatia ya kuwa mgodini bila kibali". Ambacho bado sijakupata vizuri ni - unataka picha za matukio au unataka kujua kiasi kilichomwagwa? au unataka kujua siku ngapi kwa wiki inamwagwa, au data unazotaka hapa ni zipi hasa?
Asante
Nijuavyo mimi sio kawaida kwa rais kwenda ku kampeni kwenye chaguzi ndogo. Ninategemea kiongozi wa upinzani aende labda kuwe na sababu kubwa sana.
Pia Mbowe nilisoma hapa kwamba anapendwa sana Tarime, sasa kwa mtu anayependwa si ndiye anafaa kwenda kuongoza kampeni?
Hakuwepo wakati wa mazishi ya Wangwe, asipoenda kwenye kampeni, huhitaji kuwa genius kujua maana yake.
Kuna sehemu nilisoma kama Mbatia emeenda au anaenda. Sina taarifa kuhusu Lipumba, je CUF pia wameweka mgombea wao?
Hivi Mbowe, mwenyekiti wa CHADEMA ameenda Tarime kwenye kampeni?
Kwani ni Lazima? Kwa hiyo unataka tuwe kama CCM kuprleka chama chote kule? Mkuu hujajua tu kwamba CHADEMA ni tofauti sana na CCM? Hata rangi tu zinatosha kutofautisha kwi kwi kwi!
Btw: Dawa ya CCM kutumia Dola ni ndogo sana.Wao ndio hawajali kabisa damu ya wananchi,sina la kuwashamgaa maanke hata huo moyo wa huruma wangekua nao wasingelifilisi taifa hivyo.Nitakuja kuwaonyesha kwa vitendo kwamba Watanzania wanataka haki.
Idumu Nguvu ya umma
Inaelekea unao muda mwingi wa kupoteza maana kusoma postings >1000 sio mchezo, halafu bahati mbaya bado umeibuka na wrong conclussion. Sijui kwenye debate unaangalia sura au unajadili yaliyoandikwa. Shinda hoja kwa hoja lakini ukitaka ku-debate tu na mtu atakayesifu yale uliyoandika, basi mimi sio mmoja wao. Kwangu siangalii sura, naangalia maandishi. Tunaweza tukawa upande mmoja leo, halafu kesho tukapambana kwenye opposite sides.
Kumwaga maji ndani ya mto tokea mgodini sio kitu cha ajabu na sio kosa. Kosa ni kumwaga hayo maji yakiwa hayajasafishwa. Sasa kama unao ushahidi kuwa maji yanayomwagwa yana CN utufahamishe .
Kama uliwahi kuyafanyia test hayo maji wanayomwaga, au labda kuna watu/wanyama waliokufa au kujeruhiwa na hiyo sumu, hizo ndio shahidi unazotakiwa kutueleza kuwa unazo. Vinginevyo unayoongea ni porojo tu.
Mtu kama hana kibali cha kuingia ndani ya eneo la mgodi ni lazima akikutwa atakamatwa na hiyo sio kielelezo cha kuwepo kwa CN.
Ushahidi upo mkubwa sana wa hili, yote haya ni suala la muda tu kabla watu wa Tarime hatujachukua hatua zinazostahili.
.....Ndio maana nilikuuliza kama uko makini kwenye hili jambo kabla ya kuanza kukupa habari kamili. Inaonekana hata hujui inachukua muda gani na vitu gani kwa cyanide kufanya/kuleta madhara.
...........Inawezekana una imani zaidi kwenye system au unahitaji ajali kujua kinachoendelea Tarime na migodini Tanzania.
Haya ndiyo matatizo ya Mtikila, kwanini hakuacha Polisi wafanye kazi yao? I see, Mengi naye anamuunganisha kama mwanasiasa vile? Kaazi kwelikweliWananchi walipandwa na hasira na kuwaomba polisi wamkamate kwa kufanya uchochezi lakini polisi wakamuacha aendelee kusema na kugawa makaratasi yenye maneno yake kuwa Mbowe, Mengi, Ndesa, Slaa, Mnyika na Zitto ndio waliopanga na kumuua Chacha Wangwe kwa kutuma vijana wamchome Kisu na baadaye kumpiga na nyundo. Hapo ndipo wananchi wakamgeukia na kumpiga mawe
..............habarindiyohiyo
Si tulishasikia Mbowe mwenyewe alikimbizwa kwa mawe hukohuko Tarime? Hawa hawajatumwa na CCM wala CHADEMA, labda kuna zaidiWewe furahia tu siku watakapopigwa mawe Mbowe, Slaa, Zito au Mnyika usije kusema wametumwa na CCM.
Si tulishasikia Mbowe mwenyewe alikimbizwa kwa mawe hukohuko Tarime? Hawa hawajatumwa na CCM wala CHADEMA, labda kuna zaidi
Yule mchungaji matata anayeitwa Mtikila, hivi pundwe amepelekwa hospitali kulazwa na kushonwa nyuzi baada ya kupigwa mawe na wananchi wenye hasira. Mtikila alipata dhahama hiyo baada ya kuhutubia kuwa Mbowe na CHADEMA yake ndio waliomuua Chacha Wangwe.
.......ndiyohiyo