Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Tulishasema huko nyuma kuwa Mtikila asemee hayo ya kifo cha Wangwe hukohuko Dsm akienda Tarime akitumia majukwaa kuyasema atapata matatizo hakuelewa.
Sasa yamemkuta,asifikiri watu hawaelewi kuwa hata mikopo badala ya kukopa benk siku hizi anakopa kutoka kwa wale waliotajwa kwa ufisadi. WATANZANIA WA SASA SIO MABWEGE, ajifunze.
 
Sipati picha kama dhahma hii ingemkuta Dr Slaa au Zitto nadhani wanamgambo wa Chadema hapa JF wangekuwa wananoa mapanga yao. Ama kweli mkuki mtam kwa nguruwe...

Ni kwa sababu ya udhaifu wa mawazo yao unaowafanya kutokuelewa kuwa ubora wa Demokrasia yetu ni muhimu kuliko uCHADEMA, uCCM n.k.
 
Mwanzoni nilifikri watu waliojiunga na JF ni watu makini ambao wanakerwa na hali ya mambo nchini na hawafurahii huko tunakoelekea. Nilifikiri humu ndani kungepatikana maoni huru ya kulikomboa taifa bila kujali itikadi wala imani. Nilifikiri wachangiaji humu ndani wangetanguliza maslahi ya watanzania wote kuliko utashi wa makundi katika jamii. Nilivutiwa na hiki chombo ambacho mwanzoni niliamini kina credibility kwa kulinganisha na vipeperushi vingi nchini.

OH, how wrong I was !! I now find myself spending less and less time on JF for the truth is JF is no longer my favorite blog. When objectivity is lost, sycophancy takes over and you can see this in most of the posts. You look at a name and you know exactly the content and context, what a pity !!
 
Sipati picha kama dhahma hii ingemkuta Dr Slaa au Zitto nadhani wanamgambo wa Chadema hapa JF wangekuwa wananoa mapanga yao. Ama kweli mkuki mtam kwa nguruwe...

of course huwezi kupata kwa sababu unaangalia suala hili kwa mwanga wa itikadi za chama badala ya kuona uhalifu uliotendeka na kuukataa. Ukishavuka huo mtazamo wa chama utaona kuwa uhalifu usizoelewe kukubalika, au hata kufafanuliwa bali ni lazima ushughulikiwe.

Mtikila hakustahili kipigo hicho na kama alivyosema na mimi niliashiria hapo juu ni kuwa Polisi wanawajibika moja kwa moja hasa kama alitoa taarifa za kuwa kuna mipango ya kitu kama hicho. Pamoja na hayo kila mtu awajibishwe kwa maneno yake na vitendo vyake, mtu akinitukania mama yangu kuna level ya matusi ambayo naweza kumuambia "bwana, mweke mama yangu pembeni" akiendelea nikimshindilia ngumi na kumvunja meno nitakuwa nimekosea; lakini atakuwa amejitakia kwa sababu nilishamwambia asinitukanie mama yangu.

Mambo ya kuchezea vionjo vya watu au hisia zao ni mabaya sana and should not be taken for granted. Tunaona jinsi gani Rwanda the flames of hatred were fueled by maneno ya kichochezi na kuita watu "cockroaches" n.k Tumeyaona maneno yakitumika kuwasha moto wa kisasi Iraq, Palestina, Israeli na hata katika historia ya Marekani during the civil rights movement.

Kama huoni uzito wa matumizi ya maneno na nguvu ya "spoken word' sijui itakutaje. Get over your politics na uone kuwa siasa za vitisho, uchochezi, hazina nafasi. Lazima watu warudi kwenye "hoja hujibiwa kwa hoja".

But, of course, huwezi kufanya hivyo kwa sababu kwako ni siasa na siasa tu.
 
Mtikila atakuwa alikwisha waandaa watu wa first-aid. He must have anticipated this reaction, and perhaps expected the worse




.
 

kwa hiyo wakati anasema Kolimba kauliwa na ccm alikua na conract na chadema??
 

tn over ten 10/10 ,huu ndio msimamo wangu

Chama tawala hovyooo wapinzani hovyooooooooo

Kaka safari bando ndefu
 

vipi leo lowasa nikimvamia nakumpa kibana na mahakamani nasema aliyenihamasisha nifanye hivyo ni DR SLAA kwasababu amenitia moli kwa kuniambia jamaa ni FISADI na ametuibia mabilioni ya fedha ??
 

You were wrong my dear and you are still wrong! do you expert a join a perfect group anywhere? hope JF is your favourite, the place we dare to talk openly. Mkuu akili ni nyele pia kila mtu anamalengo yake either kwa utashi wake au kutumwa. Believe me wapo wengi tu waliotumwa hapa wala hawaangalii maslahi ya Taifa.

Hata hivyo kwa suala kama hili la Mtikila, huwezi kutegemea kupata watu wa upande mmoja. Kwani Mch. Mtikila ametenda kosa kwa kumnadi Mchungaji mwenzake (sina chuki na wachungaji mimi ni Mkristo safi) kupitia hoja chafu yenye kuondoa amani. Polisi wanakosa kwa kumuacha Mtikila aendelee kuvunja amani akiwa jukwaani. waliompiga wanakosa kwa kuchukua sheria mkononi.

Kwa suala kama hili ulitegemea CCM na DP waseme nini? na CHADEMA na CUF pia wasemeje! Siasa za uchochezi hazifai. Mimi natega masikio yangu kwa Msajili wa vyama vya siasa, nadhani ni wakati wa kuifuta DP sasa.
 


kama Dr SLAA ana ushaidi wa EPA na Rirchmonduli aende mahakamani kwanini alisimama mwembeyanga?? jukwaani.
 
GM ... Mengi anamiliki vyombo vya habari ... na kuna wanasiasa ambao wanaona vyombo vyake vya habari vinawawekea kauzibe....

Pia anatofautiana na wadhamini wa ccm. Si mnafahamu wafanyabiashara kama kina YM? Muulize makamba atakueleza. Si ndio wanaompa visent Pastor!
 
..hiii njaa mbaya sana ..hadi mtikila anaenda kutoa matusi mahali ambapo anajua fika ni kuhatarisha maisha....waliomtuma kwanini hawakwenda wenyewe???
 
vipi leo lowasa nikimvamia nakumpa kibana na mahakamani nasema aliyenihamasisha nifanye hivyo ni DR SLAA kwasababu amenitia moli kwa kuniambia jamaa ni FISADI na ametuibia mabilioni ya fedha ??

hapana ukimvamia Lowasa na kumpa kibano nitakuwa wa kwanza kutaka utiwe pingu kwa kuvunja sheria!!
 
..hiii njaa mbaya sana ..hadi mtikila anaenda kutoa matusi mahali ambapo anajua fika ni kuhatarisha maisha....waliomtuma kwanini hawakwenda wenyewe???

wangeenda wenyewe polisi wangeingilia kati; na polisi hawakuwa na mpango wa kuingilia kati kwani Mtikila ni expendable!
 

Mag3,
Tulishiangiliwa na mamluki. Lakini hatutawaachia waiteke hii JF. Don't give up.
 
hapana ukimvamia Lowasa na kumpa kibano nitakuwa wa kwanza kutaka utiwe pingu kwa kuvunja sheria!!

kwa hiyo una maana DR SLAA anaposimama jukwaani nakuita watu mafisadi HUA hatii huchochezi kwa kuwafitisha the said wafisadi na wananchi??

Ama uchochezi ni pale tu chadema inapohusishwa??
 
kwa hiyo una maana DR SLAA anaposimama jukwaani nakuita watu mafisadi HUA hatii huchochezi kwa kuwafitisha the said wafisadi na wananchi??

Ama uchochezi ni pale tu chadema inapohusishwa??

umeuliza swali nimekujibu; anayevunja sheria anachukuliwa hatua hakuna excuse. Is this too hard to figure out?
 
Mtikila alistahili kupigwa mawe. Ni mchochezi asiye na lolote. Mchungaji gani mchochezi?
Akileta mchezo Tarime atarudi maiti. Period!
 
kama Dr SLAA ana ushaidi wa EPA na Rirchmonduli aende mahakamani kwanini alisimama mwembeyanga?? jukwaani.
Ushahidi upi unataka wakati ripoti ya ukaguzi na ya tume ya Mwakyembe ziko wazi? Ni wajibu wa vyombo husika kuwapeleka mahakamani wahusika. Dr. Slaa hajasema waitwe Scotland yard kuchunguza maana ushahidi tayari uko wazi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…