Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Nasikia leo polisi wamemuita Mchungaji Mtikila na kumuonya aache maneno ya uchochezi

Polisi ni wazembe kabisa
Kwanini wanashindwa kudhibiti hii hali ya uvunjifu wa amani inayoletwa na huyu mchungaji,Nadhani wanasubiri watu wauwae ndo wachukuwe hatua.Si mara ya kwanza huyu mchungaji kusema maneno ya uchochezi kwenye majukwaa,anatumiwa na watu wachache kwa maslahi yao.
Huyu tumemstukia kuwa anavunja amani,anasubiri watu wafe ndo amwage upupu na kujipatia sifa za kutanganza habari za wafu.
Mara marehemu Kolimba(R.I.P) kauwawa,mara amkashifu baba wa Taifa(R.I.P),Mara aibue ya chacha (R.I.P)
Ya uchochezi wa kifo cha kolimba na ya kumkashifu baba wa Taifa pale Singida polisi walimsekwa lupango,kwa nini hili la Tarime bado wanamuacha anatanua????Manumba vipi?
Kwa nini Huyu mchungaji asiwalishe maelezo yake polisi wayafanyie kazi?nini kazi ya polisi huko Tarime?
 
Pole sana Mtikila,
Ulituletea Mgombea Binafsi.

Doubt Yangu ni kwa nini ulichukua million tatu mkopo kwa fisadiiiiiiii?????

Ungekuja kwangu ningekukopesha hata million 10 kwa ajili ya politics.

Mie sina chama, sijaamua niwe NCCR, CUF, Chadema au CCM.

Nataka kugombea mgombea Binafsi. Am Mp admire
 
Mtikila ameminywa kona mbaya maana kesi walimfutia lakini badala ya kufunguwa kesi ya kudai fidia kama alivyofanya Mrema...Yeye amekopeshwa milioni tatu na msharti kwamba aongee maneno ya uchochezi.
Na kwasababu yuko kwenye mtego mbaya na maisha yake pia yanaweza kuwa hatarini kwa pande zote...yani upande wa wananchi kama akiendelea na uchochezi na upande wa huko alikochukuwa huto tusenti tudogo sana na kuuza uhuru wake...Huko wataminya saana tu kwani keshakuwa kama kijitumwa flani hivi...Hana njia ya kukwepa kuwafanyia kazi waliomtuma na maisha yake kisiasa yamefikia pengine ukingoni.....Nachelea lisije kuwa neno zito...Lakini maneno yake na yeye ni mazito na yanaweza kupelekea vurugu kubwa sana.
Kwanini asiwaachie ccm na serikali hiyo kazi ya kuzungumzia kuhusu kifo cha Wangwe kama huyu mtu si PANDIKIZI HATARI?
 
Huko ni TARIME ,hao WAKURYA wana misimamo hawadanganyiki na propaganda kama hizo
Angalia usije ukafia huko
 

Msisitizo wangu uko kwenye highlights nyekundu...Ina maana kuwa sababu ya yeye kupigwa mawe ni chadema na JK....
Pia madai kuwa wapinzani wote wanakutana..Wapinzani wote minus chadema? Wanakutana na nani eti? Kuzungumzia usalama wa nani?
Na anajidai kuwa hana sapoti ya ccm na polisi na kuwa ana sapoti ya upinzani ambao wanakutana na mkurugenzi wa usalama wa NEC.
Huko Tarime ni hayo madini?
Na wanasiasa wameenda kupiga kambi kabisa...Kazi ipo.
Wakati Mtikila akisema kuwa amepigwa mawe kwa kusema ukweli kuhusu kifo cha Wangwe na chadema....Kamanda Tossi na yeye anadai kuwa alipigwa mawe kwa kusema JK na Ditopile walikumbatiana....
Kwahiyo hapo ina maana tunaweza ku assume kuwa Mtikila analipiza kisasi kwa JK dhidi ya chadema?
 
Mtikila is just crayz....u can see how ditopile akawa ana ushaidi wakati dito kafa kabla ya cha wangwe....very confused na ndio maana huwa anashida kesi zake mara kwa mara kwa kuwa watu hawa pay attension kwenye mazungumzo yake...check hapo alivyo changanya?

Yaani at the end of the day huwa hana la maana,na mbona hasema kuhusu mgombea wa udiwa ni tarime peter zakaria...huyu ndio balaa,sujui CCM watajifunza lini wewe mtu mfanya biashara(mabasi ya zakari,agent wa coca) .... lingine sisemi...then awe diwani...

AU ndio aongeze mchango katika mfuko wa ushindi...zamani mtu huyu alikuwa ameshika biashara zote wilaya ya tarime...hata mabasi wa wengine yalikuwa yanaishia musoma yeye yake ndio yanakwenda mpaka tarime ,sirari...leo hii ukitaka kuwa agent wa coca wilayani tarime na vijiji vingine..lazima upate kibali kwake(Zakari) na if fact huwezi pata kwa kuwa na yeye ni agent na swahiba wake Gachuma..huu si ufisadi.....hafai hata kuwa mwenyekiti wa nyumba kumi.
 
Na sasa Mtikila anasema anakwenda Mahakamani kwa sababu waliompiga anawajua
 
Basi hizi ni siasa za kitoto I may say. Pamoja na kuwa Mtikila anaweza kutofautiana nao CHADEMA sioni sababu ya wao kufurahia yeye kupigwa mawe.

Shame on their bones (whomever celebrates Mtikila's stoning).

🙁

Inv.... Mimi ningependa kuonyesha hisia zangu wazi wazi, kwa kweli kama kuna mtu atakayeninyooshea kidole na aninyoshee tu lakini ukweli ni kwamba

NIMEFURAHI SANA KWA HUYU JAMAA KUFANYIWA ALIVYOFANYIWA MAANA AM FEDUP NA SIASA ZAKE ZA KUWA KIBARAKA ALWAYS, HE DESERVSE KUWA HAPO ALIPO KWA SASA, SIONI SABABU YA KUMUONEA HURUMA MTU AMBAYE ANATUMIWA KUHATARISHA MAISHA YA WATU ZAIDI YA 100,000, WHO ARE HIM AONGEE MANENO YA KIIZUSHI TU NA WATU WAMUANGALIE WHILE WAMEISHA SAHAU.
NOTE:- WANGWE ALIKUWA ANAPENDWA SANA NA WANANCHI WA JIMBO LAKE YEYE LEO AENDE KUONGEA KUWA ALIULIWA NA WATU FULANI WHILE MJADALA ULISHAFUNGWA KWA POLISI KUTOA JIBU KUWA ILIKUWA NI AJALI TU, KAMA HAUAMINI HUYU MCHUNGAJI ANATUMIWA HEBU SIMAMA WEWE KAMA WEWE INVISIBLE ALAFU PAYUKA KUWA MBOWE AMEUWAWA NA WATU FULANI THEN UONE KAMA UTAENDELEA KUTANUA KAMA ANAVYOTANUA SASA.

Nashukuru nimesema lile ninalolifikiria maana always huwa sipenzi kudhulumu hisia zangu
 

sasa sijui ni nani atakayethibitisha kama ni wafuasi wa CHADENA waliofanya hizo vurugu. Pia nae ULIMI WAKE UMEMPONZA. Hivi mbona mtu mzima kama mtikila natumia kifo kama stepping stone ktk siasa bila kufikiria kwamba ni kiasi gani hadhira inakwazika na maneno au matendo yake?

Pia,nadhani watu makini wangweweza kufikiria mbele zaidi na kuona kwamba hata CCM wanweza kuwa wamefanya dili la kuandaa vijana ili kuichafua CHADEMA kwa kuanzisha vurugu huku wakijifanya wafuasi wa CHADEMA.


Pia, Inawezakana kukawa na watu ambao ni Neutral lakini hawataki kusikia siasa za kuchafuana na mbaya zaidi mtu kama Reginald Mengi anapohusishwa ktk mazingira ambayo hayaeleweki.Mengi nin mtu ambae amelisaidia sana taifa letu lakini inapotokea mtu anaropoka kwa maslahi yake tu,huwa hatuwezi kumuonea huruma sana maanake ni mtu mbinafsi asiyejali maslahi ya watanzania walio wengi.Kwa kawaida mimi sipendi hizi siasa za vurugu lakini haki inapohujumiwa basi hapo kikomo cha uvumilivu wangu ni hapo.
 
Hapana mleta habari kutupasha kwa mbwembwe kuwa Mtikila yamemkuta hayo baada ya kuhutubia kuwa Mbowe na Chadema ndio waliomuua Wangwe. Hapo by implication hao watakuwa ni mashabiki wa Chadema,,,

sijajua kama hapa jamvini tuna watu wenye akili nyembamba hivi.Uko shallow sana mzee.Duh!
 
sijajua kama hapa jamvini tuna watu wenye akili nyembamba hivi.Uko shallow sana mzee.Duh!

Ni haki yako kama ambavyo mimi ninavyoona wewe ni punguani mzee Duh!
 


Nadhani hiyo nguvu wanayotumia CCM huko tarime wangeweza kuitumia pia angalao nusu yake dhidi ya wahujumu uchumi wa taifa letu,naam Mafisadi wa EPA na Richmond.

Nadhani kama msekwa ni makamu mwenyekiti wa chama chenye nia nzuri na taifa letu,anekua tayari ameshatoa wito kwa Jk kuwashughulikia wahalifu wa BOT kama alivyoonyesha uzalendo wake ktk kuhimiza polisi kuwashughulikia wahalifu wa Tarim.Hope hata wewe mkuu unaona hivyo,au bado?
 
Ni haki yako kama ambavyo mimi ninavyoona wewe ni punguani mzee Duh!


Ndiyo,ni haki yangu kabisa wala hujakosea. Nadhani inabidi nielewe kwenye msafara wa mamba kenge nao wamo.Hayo mawazo yako mepesi usituambukize mzee,ni hatari kwa ustawi wa taifa letu maanke akili imedumaa mno.You are just here for clapping!
 
Ndiyo,ni haki yangu kabisa wala hujakosea. Nadhani inabidi nielewe kwenye msafara wa mamba kenge nao wamo.Hayo mawazo yako mepesi usituambukize mzee,ni hatari kwa ustawi wa taifa letu maanke akili imedumaa mno.You are just here for clapping!

The best u can do kila unapoona post yangu wewe usisome nisije "nakaku dumaza" na mawazo yangu myepesi.....
 


Mkuu,

Ungekua mgumu kudanganyika basi usingekua mgumu kuelewa namana hii.
 
Nashauri tuendelee na mjadala maneno na vijembe mnaweza kuanza mada yake .Hili la Tarime ni maisha ya watu tafadhali tuachieni mjadala
 
Lunyungu,

Mbali ya kukandiana. ukweli unakuja kuwa mtikila alikuwa anachochea maasi. HILI LIPO WAZI, labda rafiki yangu Masatu tu ndio halioni.

Mimi nimefurahia Mtikila kula kichapo toka kwa wananchi, at the same time nawalaumu POLISI. Ilitakiwa wamchukue akalale sero kwa USALAMA WAKE MWENYEWE.

Wananchi wamechoka na mahakama ambazo kesi inachukua miaka kuisha.

Mbali ya kupigwa Mtikila amejitakia mwenyewe.
 
Polisi wanasema waliompiga mawe Mch. Mtikila ni balozi wa nyumba kumi wa CCM na vijana 3 wa DP. Hakuna mhusika kutoka CHADEMA wala chama kingine cha siasa. Hapo utaona kwamba suala la Mtikila kupigwa halihusishi chama cha siasa bali uchochezi anaouhubiri kwa ujasiri bila aibu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…