William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
Yale mabezo ya Helicopter yako wapi sasa? Hawa CCM kwa kula matapishi yao hawawezekani? Sasa kama Chama kikongwe kinafikia mahali kinadhani kunapoteza wapenzi na wapigakura kwa ajili ya helicopter na sio uongozi mbovu basi KWISHA KAZI.KIONDOKE TUU.
Kisingizio, Mkuu. Hizo barabara zimeanza kuwa mbovu leo? Kwani ni lazima hiyo mikutano mingi kwa siku moja lazima ihutubiwe na walewale? Mbona kwa wenzetu, wanagawana sehemu za kwenda na kuhutubia. Watasemaje wanajua machungu ya wananchi kama wanakwepa hizo barabara mbovu ambazo wanazitumia? Hapana, hizi ni zile zile siasa za Simba na Yanga. Zimejaa kutambiana zaidi kuliko substance. Heri wangepanda baiskeli angalau hivyo vitambi vingepunguka.
Hizi helikopta sio suala la kushabikia bali kusikitikia. Huu ni upungufu wa akili wa hao wanasiasa walioamua kuzitumia na kuwafanya wana Tarime kuwa wajinga wanaopiga kura kwa sababu ya kuona helikopta.
Ben, Nsanji Mpoki, Huduma n.k., acheni kuwa na fikira fupi za kushabikia kopta zisizowasaidia wanaTarime.
Hivi hao wanaoruka na helikopta watajua vipi shida za walioko ardhini kama hawasafiri na kuishi nao huko aridhini? Kama barabara ni mbovu, hao wanaoruka na Kopta watajuaje kuwa zinahitaji matengenezo wakati hawazitumii?
WanaTarime wanatakiwa wasizipigie kura CCM na CHADEMA kwani vyote hivi vyama vimeacha kushiriki nao kwenye shida zao za usafiri n.k., na badala yake wanawaona wao ni punguawani wanaotongozwa na helcopta ambazo hawataziona tena baada ya uchaguzi. Wakiwachagua moja kati yao, watakuwa ni wapumbavu wakubwa.
Kwanza,Mkamap nakuomba uje hapa utetee ule upuuzi wako uliokua unasema against CHADEMA kutumia helkopta
Hao wote uliotaja wewe kubwajinga wana fikra pevu kuliko fikra zako fupi kwa kufikiri matumizi ya helikopta ni anasa.
Bara bara mbovu ni matunda ya sera za sisiemu uliyochangia kuiweka madarakani.
Mchugaji wa kondoo wa bwana na mmiliki wa chama kiitwacho DP Christopher Mtikila amekaririwa akiunguruma kwenye kampeni za kumnadi mgombea wa wa chama chake huko Tarime kwa staili ya aina yake.
Mtikila aliwaambia wanatarime kuwa kama hawataki kumpigia kura mgombea wa chama chake basi wampigie kura mgombea wa CCM lakini siyo wa CHADEMA.Kwasasa Mtikila anayapatia majibu maswali tuliyokuwa tunajiuliza kumhusu yeye na chama chake.Kilichompeleka Mtikila Tarime siyo kutafuta ushindi wa chama chake bali kuchafua hali ya hewa na kuukosesha upinzani ushindi.
Kama kweli Mtikila ni kiongozi wa chama cha upinzani asingetoa kauli kama alizozitoa jana Tarime.Ameuthibitishia umma kuwa amepandikizwa na CCM kusudi atumike kuwapumbaza watu wa Tarime.Bahati mbaya sana DP naamini haina wanachama, pengine wakiwepo hawazidi ishirini pale Tarime hivyo CCM hawategemei kura za wana DP.Hazina kubwa aliyonayo Mtikila ni uwezo wake wa kuibua hoja za kupikwa na kuwaaminisha watu kuwa ni za kweli.Lakini hazina kubwa zaidi ni kuwa kwake tayari kutumiwa mahali popote kama inavyotokea Tarime.
CCM wanatumia mbinu walizotumia wakoloni Afrika hasa waingereza(INDIRECT RULE).Wanatanguliza vibaraka mbele na kuwakaririsha maneno ya kusema kusudi isionekane yanatoka kwao lakini ukweli ni kuwa wao(CCM) ndio wanoucheza mchezo wenyewe.
Kauli ya Mtikila kwa kweli inatufungua masikio zaidi kugundua ni kwa jinsi gani upinzani wa siasa Tanzania unavyogeuzwa na wachache kuwa mradi binafsi.
Katika hali ya kawaida hutegemei kiongozi wa chama cha upinzani kumpigia kampeni mgombea wa CCM dhidi ya wale wa vyama vingine vya upinzani.Huo ndio undumilakuwili na mchezo mchafu ambao refarii anaufumbia macho eti kwasababu ana hisa kwenye timu inayocheza rafu.
Ndugu yangu usiturudishe kwenye teknolojia ya kizamani,lazima ulimwengu wa sasa hivi unatakiwa upeleke mambo kwa kasi.Fikra hizo za kwako ndio zinazo umiza migongo wakulima wetu kwa kutumia jembe la mkono kwa tija ndogo.Mimi nimependekeza kule kyela wafanyabiashara wajiunge pamoja kuanzisha makampuni ya usafiri ya kwenda vijijini.Hiyo hatua itapunguza mda wa wananchi kutembea kwa miguu na kupoteza mda wa uzalishaji mashambani. Chukulia usafiri wa anga kuwa sio starehe ni kitu cha kuokoa mda,ili mwili uwe na nguvu ya kufanya kazi zingine.
Hizi
Hivi hao wanaoruka na helikopta watajua vipi shida za walioko ardhini kama hawasafiri na kuishi nao huko aridhini? Kama barabara ni mbovu, hao wanaoruka na Kopta watajuaje kuwa zinahitaji matengenezo wakati hawazitumii?
Je na hao wanaosafiri kila kukicha nje ya nchi wanajua kuwa kuna barabara mbovu,na wananchi wana umeme wa mgao?
wanaosema wanamfahamu mwita tangu akiwa daruso mnakosea sana, huwezi kumhukukkumu mtu kwa kuangalia maisha yake ya uanafunzi watu wanabadilika sana baada ya kutoka shuleni,akina mbatia na wengine wanayofanya sasa ni tofauti sana na yale waliyoamini wakiwa pale mlimani, hata akina lowasa nk.
halafu, kuna hili linalojitokeza kuwa upinzani ukiwa na nguvu mahali fulani, tunaanza kuzungumza na kuhofu kuchinjana, haitawezekana upinzani uwe hafifu kwa ajili ya hadithi za rwanda na burundi
Mbona hamjasema hizo fulana ambazo hata mbwa wamevalishwa pamoja na kanga na kapelo za kichwani zinazosambazwa ovyo kwa kila mtu kwamba ni ufujaji wa pesa za umma? mbona hii ni double standard?
Msimamo wangu uko pale pale.
CHADEMA wapuuzi kama walivyo CCM.
CHADEMA wanatumia fedha za posho kuruka na upuuzi mtupu wakati wapuuzi wengine CCM wanatumia EPA kuruka na chopper.
Tatizo lako Ben bado hujanielewa na hutokaa unielewe .
Msimamo wangu ni ule ule CHADEMA na CCM ni wote bomu hawana sera zozote na kuendelea kutegemea CHADEMA eti chama mbadala LABDA mbadala ktk kuendeleza ufisadi.
Hizi
Hivi hao wanaoruka na helikopta watajua vipi shida za walioko ardhini kama hawasafiri na kuishi nao huko aridhini? Kama barabara ni mbovu, hao wanaoruka na Kopta watajuaje kuwa zinahitaji matengenezo wakati hawazitumii?
Je na hao wanaosafiri kila kukicha nje ya nchi wanajua kuwa kuna barabara mbovu,na wananchi wana umeme wa mgao?
Mutua,
Hii ya kwako kali. Kwa hiyo kwa vile JK ana-Vasco Dagamisha, hivyo Mbowe naye lazima awe mzembe kama JK kwa kutokujali hali ya chama wala matatizo ya wananchi? Basi kama ni hivyo CHADEMA tuwaite CCM-B na kuwaachia utetezi wa wanachi CUF, NCCR n.k. Jitahidi kuwa mtu wa fikara na sio wa kupiga makofi tu.
huu ndio mwanzo wa mwisho wa hatma ya kisiasa ya mwita. Tamaa ya mali na uchu wa madaraka ndio vimemfanya ahamie chadema. hiyo ni njaa tuu ndio imemkimbiza. namfahamu alipokuwa kiongozi wa DARUSO. hakufanya lolote zaidi ya kujikomba komba kwa CCM. kwa CHADEMA, amepotea!.
Wote wanatakiwa watupatie gharama walizotumia kwenye huu uchaguzi na wapi walipata hizo pesa. I wish our foreign donors come forth and twist their hands to demand the breakdown of their shameless spendings. How come that our major parties spend lavishly in a minor election with no regard to the stinking poverty our people are facing?