Ni Mwita Mwikabwe, aliyeshtukia mchezo kuwa wamemtosa katika kugombea ubunge wa Tarime kama alivyotarajia, kwasababu ya fedha zilivyomwagwa.
Mbaya zaidi, hakutarajia kilichotokea, as alidhani watampa hata ukurugenzi wa kampeni huko Tarime, wakamtosa tena, wakampa Tambwe Hizza.
Kama hiyo haitoshi, Mwikabwe wetu akaanza kushambulia timu ya kampeni ya CCM jinsi ilivyokuwa ikitumia agenda ya kifo cha Wangwe kama nyenzo, akawaponda sana kama 'alivyoozoea kuongea wakati ule akihamasisha migomo pale UDSM'.
Wakamshtukia. Wakaona huyu anataka kuwa Nape Nauye, ndani ya hii hii miezi miwili, hapana! Wakaamua kucheza tena ka-game. Bosi wake, Nchimbi, akamwita na kumwambia aende makao makuu ya UVCCM, amepatiwa kazi ya kufanya huko, ahame sasa kutoka Tanga kama katibu wa umoja huo wa vijana.
Rais mstaafu huyo wa DARUSO akawashtukia, akagomea hiyo ofa, akisema ni sawa na kwenda kuwa mtumishi wa kumletea chai Nchimbi. Akasema yeye ni msomi, tena ana shahada ya ualimu kutoka chuo maarufu Afrika, na duniani pia.
Hapa tukashtuka. Tukaanza kushangaa kuwa Waitara kakumbuka leo kuwa ni msomi?!Alikuwa wapi!! Mbona hakwenda moja kwa moja kwenye ajitra yake alipohitimu, akaonja chungu wanayopata walimu! mafao hewa, mishahara ya chini, na kila aina ya rabsha zinazowafanya wapange migomo isiyotekelezeka hatahivyo kwa kutishiwa kila leo na ahadi hewa za serikali yetu 'smart'!
Sawa. Kama aliamua kwenda kuwapigania wanyonge kwa kutumia siasa tu na si taaluma yake(kutoenda kwenye ualimu hata akaanzia ukatibu wa wilaya wa CWT), kwa usomi wake huo kweli, hakuyakumbuka machungu ya pale chuoni, KWELI KWELI AKADHANI URAHISI NI KWENDA UVCCM?
Tuna mashaka na huo uamuzi. Tukisema alitaka madaraka na kujinufaisha binafsi bila kuonja chungu ya wapiganaji halisi kama kina:
-Mnyika-aliyepokonywa ushindi pale ubungo,
-Zitto-alieonja machungu ya kufukuzwa bungeni na mgomo wa UDSM wa 2003 kugomea kuanzishwa bodi ya mikopo-akiwa Secretary General(Waziri mkuu wa DARUSO) ulivyomtesa
-Tweve, aliyekuwa chachu ya mgomo wa 2003 pia, lakini ndo wameenda kusomeshwa na CHADEMA na kuwa nguzo ya propaganda za kupambana na ufisadi
-Mrema, aliyekuwa waziri mkuu hapo DARUSO wakati Mwita akiwa Rais, jinsi alivyoenda mapema CHADEMA, na ndio wapanga mikakati myema ya kuokoa nchi hii na ufisadi.
Si hao tu;Wapo kina Mdee, Suzan Lymo, huwezi amini wote hawa walikuwa wanafunzi wa Mwikabwe katika Siasa. Tuseme mwalimu wao huu aliwasaliti? kisa, tamaa ama! Sasa jana ndio KAINGIA CHADEMA RASMI na kukabidhiwa kadi na kamanda Mbowe, tuseme alichelewa ama? je atailipa nini jamii aliyochelewa kuitumikia? Je aiombe radhi?Ndio, yametimia, lakini alikuwa wapi?
Tuna wasiwasi na maamuzi yake haya!