Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Tufike mahali tuachane na mawazo ya kizamani, siku hizi uchaguzi ni uchumi pia,

katika process ya uchaguzi jimbo ni lazima lineemeke na uchumi wa uchaguzi huhitaji kuwa professor kuelewa hili, au?
 
Ni Mwita Mwikabwe, aliyeshtukia mchezo kuwa wamemtosa katika kugombea ubunge wa Tarime kama alivyotarajia, kwasababu ya fedha zilivyomwagwa.

Mbaya zaidi, hakutarajia kilichotokea, as alidhani watampa hata ukurugenzi wa kampeni huko Tarime, wakamtosa tena, wakampa Tambwe Hizza.

Kama hiyo haitoshi, Mwikabwe wetu akaanza kushambulia timu ya kampeni ya CCM jinsi ilivyokuwa ikitumia agenda ya kifo cha Wangwe kama nyenzo, akawaponda sana kama 'alivyoozoea kuongea wakati ule akihamasisha migomo pale UDSM'.

Wakamshtukia. Wakaona huyu anataka kuwa Nape Nauye, ndani ya hii hii miezi miwili, hapana! Wakaamua kucheza tena ka-game. Bosi wake, Nchimbi, akamwita na kumwambia aende makao makuu ya UVCCM, amepatiwa kazi ya kufanya huko, ahame sasa kutoka Tanga kama katibu wa umoja huo wa vijana.

Rais mstaafu huyo wa DARUSO akawashtukia, akagomea hiyo ofa, akisema ni sawa na kwenda kuwa mtumishi wa kumletea chai Nchimbi. Akasema yeye ni msomi, tena ana shahada ya ualimu kutoka chuo maarufu Afrika, na duniani pia.

Hapa tukashtuka. Tukaanza kushangaa kuwa Waitara kakumbuka leo kuwa ni msomi?!Alikuwa wapi!! Mbona hakwenda moja kwa moja kwenye ajitra yake alipohitimu, akaonja chungu wanayopata walimu! mafao hewa, mishahara ya chini, na kila aina ya rabsha zinazowafanya wapange migomo isiyotekelezeka hatahivyo kwa kutishiwa kila leo na ahadi hewa za serikali yetu 'smart'!

Sawa. Kama aliamua kwenda kuwapigania wanyonge kwa kutumia siasa tu na si taaluma yake(kutoenda kwenye ualimu hata akaanzia ukatibu wa wilaya wa CWT), kwa usomi wake huo kweli, hakuyakumbuka machungu ya pale chuoni, KWELI KWELI AKADHANI URAHISI NI KWENDA UVCCM?

Tuna mashaka na huo uamuzi. Tukisema alitaka madaraka na kujinufaisha binafsi bila kuonja chungu ya wapiganaji halisi kama kina:

-Mnyika-aliyepokonywa ushindi pale ubungo,
-Zitto-alieonja machungu ya kufukuzwa bungeni na mgomo wa UDSM wa 2003 kugomea kuanzishwa bodi ya mikopo-akiwa Secretary General(Waziri mkuu wa DARUSO) ulivyomtesa
-Tweve, aliyekuwa chachu ya mgomo wa 2003 pia, lakini ndo wameenda kusomeshwa na CHADEMA na kuwa nguzo ya propaganda za kupambana na ufisadi
-Mrema, aliyekuwa waziri mkuu hapo DARUSO wakati Mwita akiwa Rais, jinsi alivyoenda mapema CHADEMA, na ndio wapanga mikakati myema ya kuokoa nchi hii na ufisadi.

Si hao tu;Wapo kina Mdee, Suzan Lymo, huwezi amini wote hawa walikuwa wanafunzi wa Mwikabwe katika Siasa. Tuseme mwalimu wao huu aliwasaliti? kisa, tamaa ama! Sasa jana ndio KAINGIA CHADEMA RASMI na kukabidhiwa kadi na kamanda Mbowe, tuseme alichelewa ama? je atailipa nini jamii aliyochelewa kuitumikia? Je aiombe radhi?Ndio, yametimia, lakini alikuwa wapi?
Tuna wasiwasi na maamuzi yake haya!
 
Yale mabezo ya Helicopter yako wapi sasa? Hawa CCM kwa kula matapishi yao hawawezekani? Sasa kama Chama kikongwe kinafikia mahali kinadhani kunapoteza wapenzi na wapigakura kwa ajili ya helicopter na sio uongozi mbovu basi KWISHA KAZI.KIONDOKE TUU.

Afadhali umesama wewe Chakaza,
Mwaka 2005 CCM walichonga sana kuhusu matumizi ya helkopta yaliyofanywa na CHADEMA.Walibeza sana na kuita huo ni ufujaji wa fedha nk.

Leo hii tunapowaona nao wanatangaza kutumia helkopta mbili tunabaki kuwashangaa.Umefika wakati sasa CCM wanatapatapa hivyo kubakia kuangalia wanachofanya wenzao nao wanaiga.Huko ndiko kuishiwa sera na mikakati.Moto wa CCM ulikuwa wa mabua na sasa ndiyo yanazimikaaaaaa
 
Kisingizio, Mkuu. Hizo barabara zimeanza kuwa mbovu leo? Kwani ni lazima hiyo mikutano mingi kwa siku moja lazima ihutubiwe na walewale? Mbona kwa wenzetu, wanagawana sehemu za kwenda na kuhutubia. Watasemaje wanajua machungu ya wananchi kama wanakwepa hizo barabara mbovu ambazo wanazitumia? Hapana, hizi ni zile zile siasa za Simba na Yanga. Zimejaa kutambiana zaidi kuliko substance. Heri wangepanda baiskeli angalau hivyo vitambi vingepunguka.

Mkuu mbona sikuelewi?
yaani katika karne hii watu katika nchi yenye barabara mbovu kama nilivyozishuhudia watembee kwa baiskeli?
Naona haya ni mawazo ya ki sisiemu. Lakini hata wao wameshindwa.
Mbowe alibuni njia hii kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja. Huu ni ubunifu. Nashangaa sisiemu nao wameiga ingawa waliipinga sana njia hii miaka ya nyuma.
Naunga mkono watumie anga kama wanaona inafaa.
Mbona hamjasema hizo fulana ambazo hata mbwa wamevalishwa pamoja na kanga na kapelo za kichwani zinazosambazwa ovyo kwa kila mtu kwamba ni ufujaji wa pesa za umma? mbona hii ni double standard?
 
Hizi helikopta sio suala la kushabikia bali kusikitikia. Huu ni upungufu wa akili wa hao wanasiasa walioamua kuzitumia na kuwafanya wana Tarime kuwa wajinga wanaopiga kura kwa sababu ya kuona helikopta.

Ben, Nsanji Mpoki, Huduma n.k., acheni kuwa na fikira fupi za kushabikia kopta zisizowasaidia wanaTarime.

Hivi hao wanaoruka na helikopta watajua vipi shida za walioko ardhini kama hawasafiri na kuishi nao huko aridhini? Kama barabara ni mbovu, hao wanaoruka na Kopta watajuaje kuwa zinahitaji matengenezo wakati hawazitumii?

WanaTarime wanatakiwa wasizipigie kura CCM na CHADEMA kwani vyote hivi vyama vimeacha kushiriki nao kwenye shida zao za usafiri n.k., na badala yake wanawaona wao ni punguawani wanaotongozwa na helcopta ambazo hawataziona tena baada ya uchaguzi. Wakiwachagua moja kati yao, watakuwa ni wapumbavu wakubwa.
 
Mchugaji wa kondoo wa bwana na mmiliki wa chama kiitwacho DP Christopher Mtikila amekaririwa akiunguruma kwenye kampeni za kumnadi mgombea wa wa chama chake huko Tarime kwa staili ya aina yake.

Mtikila aliwaambia wanatarime kuwa kama hawataki kumpigia kura mgombea wa chama chake basi wampigie kura mgombea wa CCM lakini siyo wa CHADEMA.Kwasasa Mtikila anayapatia majibu maswali tuliyokuwa tunajiuliza kumhusu yeye na chama chake.Kilichompeleka Mtikila Tarime siyo kutafuta ushindi wa chama chake bali kuchafua hali ya hewa na kuukosesha upinzani ushindi.

Kama kweli Mtikila ni kiongozi wa chama cha upinzani asingetoa kauli kama alizozitoa jana Tarime.Ameuthibitishia umma kuwa amepandikizwa na CCM kusudi atumike kuwapumbaza watu wa Tarime.Bahati mbaya sana DP naamini haina wanachama, pengine wakiwepo hawazidi ishirini pale Tarime hivyo CCM hawategemei kura za wana DP.Hazina kubwa aliyonayo Mtikila ni uwezo wake wa kuibua hoja za kupikwa na kuwaaminisha watu kuwa ni za kweli.Lakini hazina kubwa zaidi ni kuwa kwake tayari kutumiwa mahali popote kama inavyotokea Tarime.

CCM wanatumia mbinu walizotumia wakoloni Afrika hasa waingereza(INDIRECT RULE).Wanatanguliza vibaraka mbele na kuwakaririsha maneno ya kusema kusudi isionekane yanatoka kwao lakini ukweli ni kuwa wao(CCM) ndio wanoucheza mchezo wenyewe.

Kauli ya Mtikila kwa kweli inatufungua masikio zaidi kugundua ni kwa jinsi gani upinzani wa siasa Tanzania unavyogeuzwa na wachache kuwa mradi binafsi.
Katika hali ya kawaida hutegemei kiongozi wa chama cha upinzani kumpigia kampeni mgombea wa CCM dhidi ya wale wa vyama vingine vya upinzani.Huo ndio undumilakuwili na mchezo mchafu ambao refarii anaufumbia macho eti kwasababu ana hisa kwenye timu inayocheza rafu.
 
Hao wote uliotaja wewe kubwajinga wana fikra pevu kuliko fikra zako fupi kwa kufikiri matumizi ya helikopta ni anasa.
Bara bara mbovu ni matunda ya sera za sisiemu uliyochangia kuiweka madarakani.
 
Kwanza,Mkamap nakuomba uje hapa utetee ule upuuzi wako uliokua unasema against CHADEMA kutumia helkopta

Msimamo wangu uko pale pale.
CHADEMA wapuuzi kama walivyo CCM.
CHADEMA wanatumia fedha za posho kuruka na upuuzi mtupu wakati wapuuzi wengine CCM wanatumia EPA kuruka na chopper.
Tatizo lako Ben bado hujanielewa na hutokaa unielewe .

Msimamo wangu ni ule ule CHADEMA na CCM ni wote bomu hawana sera zozote na kuendelea kutegemea CHADEMA eti chama mbadala LABDA mbadala ktk kuendeleza ufisadi.

Hizi posho ndizo zinaishia makao makuu kwa deni baada ya uchaguzi,mtaendelea lini.mkimaliza hapo mtalipa deni la helkopita hiyo mpaka 2010,Na 2010 mtakopa tena mpae na helkopita mkimaliza hapo mtalipa deni hadi 2015 na 2015 mtakopa tena.Mtakiendeleza lini ninyi hicho chama.
 
Hao wote uliotaja wewe kubwajinga wana fikra pevu kuliko fikra zako fupi kwa kufikiri matumizi ya helikopta ni anasa.
Bara bara mbovu ni matunda ya sera za sisiemu uliyochangia kuiweka madarakani.

m-fisadi,
Kwa viwango vyangu nilivyotumia basi na wewe pia ongezea jina lako kwenye hiyo list ya wenye fikira fupi.

Maana kama kutumia Kopta kwenye kajimbo kama Tarime sio anasa, basi tuwatafutie JK, Mama JK, Pinda n.k., kila mmoja kaKopta kake ili watupunguzie msongamano Dar. Wewe unaonaje?
 
Mchugaji wa kondoo wa bwana na mmiliki wa chama kiitwacho DP Christopher Mtikila amekaririwa akiunguruma kwenye kampeni za kumnadi mgombea wa wa chama chake huko Tarime kwa staili ya aina yake.

Mtikila aliwaambia wanatarime kuwa kama hawataki kumpigia kura mgombea wa chama chake basi wampigie kura mgombea wa CCM lakini siyo wa CHADEMA.Kwasasa Mtikila anayapatia majibu maswali tuliyokuwa tunajiuliza kumhusu yeye na chama chake.Kilichompeleka Mtikila Tarime siyo kutafuta ushindi wa chama chake bali kuchafua hali ya hewa na kuukosesha upinzani ushindi.

Kama kweli Mtikila ni kiongozi wa chama cha upinzani asingetoa kauli kama alizozitoa jana Tarime.Ameuthibitishia umma kuwa amepandikizwa na CCM kusudi atumike kuwapumbaza watu wa Tarime.Bahati mbaya sana DP naamini haina wanachama, pengine wakiwepo hawazidi ishirini pale Tarime hivyo CCM hawategemei kura za wana DP.Hazina kubwa aliyonayo Mtikila ni uwezo wake wa kuibua hoja za kupikwa na kuwaaminisha watu kuwa ni za kweli.Lakini hazina kubwa zaidi ni kuwa kwake tayari kutumiwa mahali popote kama inavyotokea Tarime.

CCM wanatumia mbinu walizotumia wakoloni Afrika hasa waingereza(INDIRECT RULE).Wanatanguliza vibaraka mbele na kuwakaririsha maneno ya kusema kusudi isionekane yanatoka kwao lakini ukweli ni kuwa wao(CCM) ndio wanoucheza mchezo wenyewe.

Kauli ya Mtikila kwa kweli inatufungua masikio zaidi kugundua ni kwa jinsi gani upinzani wa siasa Tanzania unavyogeuzwa na wachache kuwa mradi binafsi.
Katika hali ya kawaida hutegemei kiongozi wa chama cha upinzani kumpigia kampeni mgombea wa CCM dhidi ya wale wa vyama vingine vya upinzani.Huo ndio undumilakuwili na mchezo mchafu ambao refarii anaufumbia macho eti kwasababu ana hisa kwenye timu inayocheza rafu.

Na Bado tutasikia mengi
 
Wapendwa naomba kuhabarishwa FISADI JOHN KOMBA yuko wapi na TOT yake, au ile kashifa ya kikundi chake imewafanya mafisadi wasimuite kumpigia chapuo mwizi mwenzie???
Kama hii ni kweli basi JF tupige kambi Tarime kwa siku hilizo salia ili tuwamalize kabisaa hawa jamaa, kwani sasa kila kitu hakishikiki kwao.
 
Ndugu yangu usiturudishe kwenye teknolojia ya kizamani,lazima ulimwengu wa sasa hivi unatakiwa upeleke mambo kwa kasi.Fikra hizo za kwako ndio zinazo umiza migongo wakulima wetu kwa kutumia jembe la mkono kwa tija ndogo.Mimi nimependekeza kule kyela wafanyabiashara wajiunge pamoja kuanzisha makampuni ya usafiri ya kwenda vijijini.Hiyo hatua itapunguza mda wa wananchi kutembea kwa miguu na kupoteza mda wa uzalishaji mashambani. Chukulia usafiri wa anga kuwa sio starehe ni kitu cha kuokoa mda,ili mwili uwe na nguvu ya kufanya kazi zingine.

Kwani teknolojia ya helikopta ni ya kisasa? Hao wakulima wako Kyela wataanzisha makampuni ya usafiri wa anga ? Maana usafiri wa barabara ushasema ni teknolijia ya zamani. Pamoja na maneno mazuri ya wana siasa, matumizi ya helikopta yanatumika kuwazuga wananchi na si vinginevyo. Katika ka wilaya Tarime kweli kunahitajika helikopta mbili ili kuwatembelea wananchi? Ni yale yale ya kusifia utajiri wa nduguyo wakati wewe hauna kitu. Kwenye nchi iliyo katika nchi maskini za kutupwa hapa duniani kudai kuwa ni lazima tutumie helikopta ni ulimbukeni. Hao walioendelea walitambua umasikini wao kwanza, wakaupiga vita na ndiyo sasa wako walipo. Hakuna njia ya mkato. Kama baada ya miaka zaidi ya 40 ya uhuru mtu unahitaji helikopta kuzungukia kawilaya katarime basi hatuna cha kujivunia. Kupanda helikopta hakubadilishi hili bali ni kuwabeza wale ambao badala ya kuwajengea barabara tunafuja kodi zao kwa matumizi ya kujibalaghua. Kama tulivyofanya kwenye ndege ya Rais. Kama tulivyofanya kwenye rada. Tulifumbia macho umasikini wetu na kudhani kuwa kwa kununua hizo toys nasi tutaonekana tumeendelea. Sisi tunaochangiwa vyandarua!
 
Hizi

Hivi hao wanaoruka na helikopta watajua vipi shida za walioko ardhini kama hawasafiri na kuishi nao huko aridhini? Kama barabara ni mbovu, hao wanaoruka na Kopta watajuaje kuwa zinahitaji matengenezo wakati hawazitumii?

Je na hao wanaosafiri kila kukicha nje ya nchi wanajua kuwa kuna barabara mbovu,na wananchi wana umeme wa mgao?
 
wanaosema wanamfahamu mwita tangu akiwa daruso mnakosea sana, huwezi kumhukukkumu mtu kwa kuangalia maisha yake ya uanafunzi watu wanabadilika sana baada ya kutoka shuleni,akina mbatia na wengine wanayofanya sasa ni tofauti sana na yale waliyoamini wakiwa pale mlimani, hata akina lowasa nk.

halafu, kuna hili linalojitokeza kuwa upinzani ukiwa na nguvu mahali fulani, tunaanza kuzungumza na kuhofu kuchinjana, haitawezekana upinzani uwe hafifu kwa ajili ya hadithi za rwanda na burundi

kaka lazima tutumie historia and past record ili kumjudge mtu.... we are not saying tutakuwa accurate but it is the most acceptable means to predict in social issues.

huyu jamaa kwa ninavyo mjua ni opportunist na hana imani inayo tabirika juu ya siasa kwake yeye hesabu ya kwanza kwenye siasia ni kuwa atapata nini????

huyu jamaa alikuwa mpinzani kabla ya kuwa raisi then CCM wakamteka na kumlambisha pipi akahamia huko sasa ameona tanga hakuna maslahi kama yale aliyo kuwa akipata huku dare salaam kwa kugawa T shirts na kuandaa mikutano inayo ndo kaamua kukimbia
 
Mbona hamjasema hizo fulana ambazo hata mbwa wamevalishwa pamoja na kanga na kapelo za kichwani zinazosambazwa ovyo kwa kila mtu kwamba ni ufujaji wa pesa za umma? mbona hii ni double standard?

Helikopta, vitenge, vikofia, pilau vyote ni vile vile. Matusi kwa mwananchi ambae baada ya miaka 40 ya kujitawala vitu hivi ndiyo vimekuwa thamani ya kura yake. Wote wanaofanya hivi hawastahili kura zetu.
 
Msimamo wangu uko pale pale.
CHADEMA wapuuzi kama walivyo CCM.
CHADEMA wanatumia fedha za posho kuruka na upuuzi mtupu wakati wapuuzi wengine CCM wanatumia EPA kuruka na chopper.
Tatizo lako Ben bado hujanielewa na hutokaa unielewe .

Msimamo wangu ni ule ule CHADEMA na CCM ni wote bomu hawana sera zozote na kuendelea kutegemea CHADEMA eti chama mbadala LABDA mbadala ktk kuendeleza ufisadi.

Mkuu Mkamap,
Nakubaliana na wewe 100%. Marehemu Wangwe walimuona kuwa anaropokwa, lakini wenye akili timamu sasa wataona kwa nini alikuwa anapingana na Mbowe.

Kama CHADEMA wanatumia vipesa vyote walivyopata kwenye ruzuku kwa ajili ya kumrusha Mbowe ili asile vumbi, basi wasije wakalalamika chama kinapoishia kuwa na mizizi Kilimanjaro, Kigoma, Tarime na Arusha peke yake. Ni vipi huko mikoani watapata pesa ya kupanua chama kwa ufujaji wa aina hii?? Hivi marehemu Wangwe alipoinyakua Tarime alikuwa na Kopta??

WanaCHADEMA wanatakiwa kuacha ushabiki na kuwa wadadisi kama alivyokuwa marehemu Wangwe. RIP Wangwe.
 
Hizi

Hivi hao wanaoruka na helikopta watajua vipi shida za walioko ardhini kama hawasafiri na kuishi nao huko aridhini? Kama barabara ni mbovu, hao wanaoruka na Kopta watajuaje kuwa zinahitaji matengenezo wakati hawazitumii?

Je na hao wanaosafiri kila kukicha nje ya nchi wanajua kuwa kuna barabara mbovu,na wananchi wana umeme wa mgao?

Mutua,
Hii ya kwako kali. Kwa hiyo kwa vile JK ana-Vasco Dagamisha, hivyo Mbowe naye lazima awe mzembe kama JK kwa kutokujali hali ya chama wala matatizo ya wananchi? Basi kama ni hivyo CHADEMA tuwaite CCM-B na kuwaachia utetezi wa wanachi CUF, NCCR n.k. Jitahidi kuwa mtu wa fikara na sio wa kupiga makofi tu.
 
Kuweza kuhisi matokeo ya uchaguzi siyo kuangalia helikopta, mikutano ya watu n.k siri iko kwa nani atajitokeza kupiga kura. Turn out ya election kwangu ndiyo msingi wa mambo yatakavyokuwa.

a. Endapo turnout ya mjini Tarime itakuwa zaidi ya au karibu ya asilimia 50 ya wapiga kura na nje ya Tarime (vijijini) ikawa chini ya asilimia 40 na zaidi basi Chadema itashinda uchaguzi mzima kwa kati ya asilimia 60 na zaidi.

b. Endapo turnout ya mjini Tarime itakuwa karibu ya asilimia 50 lakini kule vijijini ikawa zaidi ya asilimia 50 vile vile CCM itaweza kushindwa kwa margin ndogo sana a little under 50.

c. Endapo hata hivyo vyama vingine vilivyosimamisha wagombea ukiondoa CCM na Chadema vikiweza kupata asilimia 10 ya kura zote (which I really doubt) basi CCM itashinda!
 
huu ndio mwanzo wa mwisho wa hatma ya kisiasa ya mwita. Tamaa ya mali na uchu wa madaraka ndio vimemfanya ahamie chadema. hiyo ni njaa tuu ndio imemkimbiza. namfahamu alipokuwa kiongozi wa DARUSO. hakufanya lolote zaidi ya kujikomba komba kwa CCM. kwa CHADEMA, amepotea!.

Tuweke kumbukumbu sawa, Mwita Mwikwabe alianzia NCCR -Mageuzi, akajakutoka kwenye chama hicho sababu mojawapo eti mwanachama mwenzake ambaye alikuwa pia ni mwalimu wake wa hesabu alimkamata (alimfailisha pale UDSM)

Kuhamahama vyama kuna tofauti ndogo na umalaya, au tofauti haipo kabisa, tena kwa style ya Mwita ndo kabisaa, huku kakimbia hesabu, kule kakimbia ukarani, ngoja tuone huko alikokwenda.

Kila chama kina itikadi yake
NCCR - Social democracy (umoja,haki,mageuzi)
CCM- ujamaa na kujitegemea
CHADEMA - Nguvu ya Umma

Sasa Mwita itikadi yake ni ipi, au yeye ni sawa tu na bendera inapouona upepo
 
Wote wanatakiwa watupatie gharama walizotumia kwenye huu uchaguzi na wapi walipata hizo pesa. I wish our foreign donors come forth and twist their hands to demand the breakdown of their shameless spendings. How come that our major parties spend lavishly in a minor election with no regard to the stinking poverty our people are facing?

Ruzuku ya CCM kwa mwezi ni million 999, ya CHADEMA million 66, ya NCCR million 1.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom