Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Mkuu weeee acha tu mambo ya ndoa haya na siasa mmmmmhh shemeji yenu nadhani yupo na akina Makamba ile sura ya Muungwana ilimchanganya, ana matenge na vilemba vya CCM ila huwa havai nadhani alipewa kwenye kampeni za 2005.....nadhani amegundua nadharia ya KASI MPYA, NGUVU MPYA NA ARI MPYA ni utopia....

Ataelewa tu kaka usihofu. all the best then
 
Usiendelee kuwa Kichwangumu, results ndivyo zilivyo.Zimethibitika.

Ndoto yangu imetimia, nuru imekuwa mwanga, kinjia kimekuwa barabara na matumaini yamepigwa jeki na sasa halali tena mtu mpaka kieleweke. Wenye nyumba hawalali tena kwa kuwa wapangaji wamecharuka na sauti zao zinamtoa hata nyoka pangoni. Makuwadi na wanafiki wamejikuta uchi na wanatafuta sehemu za kujisetiri. Manyang'au, wezi na wala rushwa wanakuna vichwa kwa kuwa kilichotendeka gizani pole pole kinaanza kumulikwa, watajificha wapi sasa.

Asante wana Tarime, nyie ni ma mura kweli kweli na mlichofanya ni ishara tosha wa kitakachofuatia muda si mrefu. Asanteni Chadema, pamoja na masimango na manyanyaso, mmeibuka kidedea na kutukumbusha kuwa penye haki hakuna nafasi kwa dhuluma na majigambo. Malaya wote wa siasa lazima wasome alama za wakati - zimwi lililotutafuna kwa miaka 40 litakufa kifo cha mende kama watanzania kwa ujumla wao watafuata nyayo za wana Tarime. Angalau sasa naweza kulala kulala kulala zzz zzz zzz. zzz......
 
asante sana poti, mafisadi lazima wakasirike sana!
eti ni jimbo la tarime tu ndo tunasoma bure kwa sababu chadema ndo wanaongoza halmashauri yetu, kwa nini majimbo mengine na nyie msichague chadema ili muache kulipa karo???
watoto wa mafisadi wote wanasoma majuu, na ada hawalipi, sababu wao ndo wenye neema tu ya kupata skolaship za bure!!
je sisi wa wakulima??
chadema oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!
Peter Zacharia ziiiiiiii, Gachuma, Vedastus Mathayo, Obetto, Lameck, Wasira, Mkono, Makongoro Nyerere, Dr Wanyancha poleni na aibu, sababu nyie ndo ilikuwa kamati ya kuiba kura! Mwenyekiti wenu Gachuma. Wanyacha ukitaka ubaki kuwa mbunge wa serengeti, ushauri wa bure hamia ccm!
 
Update: Kwa taarifa za kuaminika nilizozipata, Chadema wamefanya vizuri sana kwenye Kata ya Kemambo yenye vijiji: Nyangoto, kewanja, matongo, mrito na Kerende. Pia na Tarime mjini. Kwenye kata ya Kemambo, kwa mfano, Chadema wame-sweep kwa average ya 90%+. Nitazidi kuwapatia updates.
 
Kaka

kama unataka kutuharibia siku ulegeee. tumeshasahu huku tunasherehekea tu
 
safi sana Chadema........nilisali sana CCM wasishinde nina raha sana sasa......
 
Ama kweli maajabu ya Mussa haya!..
Nitawapongeza sana viongozi wa Chadema kwa kazi ngumu waliyoifanya kuhakikihsa ushindi umepatikana... Hongera..
Pia sina budi kumshukuru Kikwete na Utawala wake (ktk swala hili moja) kuchukua hatua moja mbele ktk kuhakikisha demokrasia inakomaa Tanzania kwani binafsi nilikuwa nasubiri habari za mauaji yatakayo fuata baada ya CCM kutangaza ushindi.
Itanichukua muda mrefu kuweza kumeza funda hili maanake domo langu wazi mwaaaaaa!
 
Muda mchache tu niliotoka hapa kwenye PC tayari kurasa kibao na matokeo juu! Hongera CHADEMA, sasa mmeshaona vita inavyopiganwa, hakuna kuweka silaha chini. Muendeee huvohuvo hadi afu iwii na ikumi!
Hongera!
 
Ama kweli maajabu ya Mussa haya!..
Nitawapongeza sana viongozi wa Chadema kwa kazi ngumu waliyoifanya kuhakikihsa ushindi umepatikana... Hongera..
Pia sina budi kumshukuru Kikwete na Utawala wake (ktk swala hili moja) kuchukua hatua moja mbele ktk kuhakikisha demokrasia inakomaa Tanzania kwani binafsi nilikuwa nasubiri habari za mauaji yatakayo fuata baada ya CCM kutangaza ushindi.
Itanichukua muda mrefu kuweza kumeza funda hili maanake domo langu wazi mwaaaaaa!

Mkandara,
Mimi sikushangaa hata kidogo, licha ya mchezo wa propaganda waliocheza CCM. Natumaini matokeo ya Tarime yatasaidia kuwafungua macho Watanzania kwinginepo kuwa CCM ni kapu ambalo limeanza kufumka kwenye makalio yake na kwamba siasa za usanii zina kikomo chake. Ziara ya mheshimiwa Mbeya pia inaleta matumaini. Huwezi kupambana na mafisadi huku unakumbatia mafisadi. Achague moja. Yuko upande wa wananchi au yuko upande wa mafisadi.
 
Mkidhania kuwa Chadema imeshinda Tarime kwa sababu ya kazi ngumu iliyofanywa na viongozi wake itakuwa mnamiss point nzima ya ushindi wa Tarime. Kilichofanywa na viongozi ni wazi kina nafasi kubwa na isiyoweza kuondolewa, lakini ushindi wa Chadema Tarime ulitokana na watu kuikataa CCM zaidi kuliko kuikubali Chadema zaidi.

Wana Tarime walikuwa na kila sababu ya kuikimbia Chadema na kuikana (kama ukizingatia habari na porojo zilizokuwa zimetengenezwa kwa muda). Kama wana Tarime wangesikiliza maneno ya "nani alimuua Wangwe" ni wazi kuwa wangeikimbia Chadema. Kama yale ya Mbowe nusura kupigwa kule Tarime wakati wa msiba yangekuwa ni ya kuaminika watu wangeona kweli Tarime wamechukizwa na Chadema. Ukizingatia mgongano wa maneno kati ya marehemu Wangwe na Mbowe na pia uongozi mzima wa Chadema ni wazi kuwa Tarime walikuwa na kila sababu ya kutoichagua Chadema na kuijaribu tena CCM. Hawakufanya hivyo. Why?
 
Hongereni sana CHADEMA!pongezi kwa wana tarime!

Vipi tena FL!!! hata wewe umewatema mafisadi!!!? Maana juzi niliweka article kuhusu fisadi Edward Hosea wa TAKUKURU kuchaguliwa mjumbe kwa TAKUKURU ya duniani. Ukaandika waliojaa wivu dhidi ya fisadi Hosea wajinyonge, kwa maana nyingine ulikuwa unamfagilia fisadi Hosea. Sasa upo kambi gani? kambi ya kupambana na mafisadi Tanzania au kambi ya mafisadi ikiongozwa na chama cha mafisadi? Inakuwa ngumu kukuelewa au wewe uko kama bendera? upepo unakovumia basi na wewe ndiyo huko huko? 🙂

Good day 🙂
 
Mwanakijiji,
Ndio maana nimesema kuwa watu wanaanza kutambua polepole kuwa CCM ni kapu ambalo limefumka kwenye makalio yake. I believe this is a harbinger of things to come.
 
Mwanakijiji,
Ndio maana nimesema kuwa watu wanaanza kutambua polepole kuwa CCM ni kapu ambalo limefumka kwenye makalio yake. I believe this is a harbinger of things to come.

CCM watakuwa wamepigwa na shock kubwa sana maana nguvu walizopeleka Tarime ikiwamo na pesa, polisi, FFU, helikopta mbili, Makamba, Msekwa, Ngeleja, pamoja na vipigo na vitisho walivyopata toka kwa polisi na FFU wana Tarime ambao ni wafuasi wa CHADEMA na kisha polisi na FFU kusifiwa na viongozi wa CCM kwa kutoa kipigo hicho, hazikuwa za kawaida. Kama hawakukaa chini na kutafakari namna ya kurudisha credibility ya chama hicho baada ya ushindi mkubwa wa CHADEMA basi sidhani kama CCM watabadilika tena, lakini 2010 Watanzania wengi watapoteza maisha yao katika uchaguzi huo kama hali itakuwa kama ilivyokuwa Tarime.
 
Mkidhania kuwa Chadema imeshinda Tarime kwa sababu ya kazi ngumu iliyofanywa na viongozi wake itakuwa mnamiss point nzima ya ushindi wa Tarime. Kilichofanywa na viongozi ni wazi kina nafasi kubwa na isiyoweza kuondolewa, lakini ushindi wa Chadema Tarime ulitokana na watu kuikataa CCM zaidi kuliko kuikubali Chadema zaidi.

Wrong analysis, again. Ushindi wa Chadema Tarime umechangikiwa kwa sehemu kubwa sana na utendaji mzuri wa serikali ya wilaya [inayoongzwa na Chadema] coupled with kazi nzuri ya viongozi wa Chadema [walioendesha campaign] kwa ku-articulate sera za Chadema na ku-outline mazuri waliyoyafanya kwa kipindi kifupi walichokuwa madarakani [i.e. kuwalipia wanafunzi wa secondary school fees n.k] So let's be clear on that.

Wana Tarime walikuwa na kila sababu ya kuikimbia Chadema na kuikana (kama ukizingatia habari na porojo zilizokuwa zimetengenezwa kwa muda). Kama wana Tarime wangesikiliza maneno ya "nani alimuua Wangwe" ni wazi kuwa wangeikimbia Chadema. Kama yale ya Mbowe nusura kupigwa kule Tarime wakati wa msiba yangekuwa ni ya kuaminika watu wangeona kweli Tarime wamechukizwa na Chadema. Ukizingatia mgongano wa maneno kati ya marehemu Wangwe na Mbowe na pia uongozi mzima wa Chadema ni wazi kuwa Tarime walikuwa na kila sababu ya kutoichagua Chadema na kuijaribu tena CCM. Hawakufanya hivyo. Why?

Baloney! Tarime voters are pretty sophisticated and knowledgable than you might think MMKJ. Ndio maana hata mwaka 1995, walimwambia Mchonga waziwazi kwamba, " tutampigia Mkapa kura, lakini siyo Kisyeri." It's sad kwamba CCM waliiba kura mwaka 1995. And I guarantee you hata kama hizo rumors za kwamba Mbowe amemuua Wangwe zingepikwa kitaalamu namna gani, still wanatarime wasinge fall kwenye hizo lies, na CCM bado ingenyweshwa maji tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom